Pre GE2025 Stephen Wasira amrithi Kinana nafasi ya Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara

Pre GE2025 Stephen Wasira amrithi Kinana nafasi ya Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wata
Wasira aliyezaliwa Julai Mosi, 1945 wilayani Bunda Mkoa wa Mara, kwa zaidi ya nusu karne amejijengea heshima kutokana na mchango wake mkubwa katika siasa, uchumi na maendeleo ya jamii.
Duh,
Sasa an̈agonga 80.
Watakuwa wamehitaji mtu kutoka "Kanda Maalum", ikawa hakuna mwingine ila ni yeye tu yupo
 
Duuuu kuna shida mahali aseee Wasira? Wanataka afie kwenye kwenye chama? Daaaa
lile zee ni babe kwa lissu, lissu akiwa mwenyekiti wa chadema tayari kawekewa mbabe wake. Wale wakiitwa studioni kufanya kipindi watenganishwe, zee lina hasira sana lile, linaweza kumrushia ngumi lissu
 
😂😂😂😂🤣🤣🤣🤣😂😂😂😂🤣
Niliwahi kutabiri hii ishu mwanzoni mwa mwaka jana

Erythrocyte
Screenshot_20250118-125619.png


The Evil Genius
Screenshot_20250118-125551.png
 
Samia hapa kadondokea pua.
siokweli. wassira yupo vizuri sana. ndio waliku wazee muhimu sana kwenye serikali ya kikwete.kama unakumbuka kipindi cha jk alikua na uwezo wa kudili hadi na wageni wanaokuja kutoka nje jk alimuamini sana alikua akiwapokea kuishauli utawala kitugani cha kufanya dhidi mgeni huyo. hapa nazungumzia wageni muhimu kwenye nchi na sio hawa wa kawaida.
wassira ni jasiri.nafasi hiyo inamfaa hasa.
 
Wajumbe pigeni kura za hapana. Mzee wa watu apumzike tafuteni damu changa nyenye mawazo chanya, vinginevyo chama kinazidi kudhoofu mtasaisiwa hadi lini wakati wa chaguzi ndugu zangu.
Hapa ndipo Chadema mmefeli, makamu mwenyekiti wa ccm ndio anaongoza kamati ya usalama na maadili.

Chadema pia kikatiba Lisu ndio mamlaka ya nidhamu lakini hana nidhamu yeye mwenyewe na ameshindwa kusimamia nidhamu.

Ccm imewapa funzo kubwa sana watu wa miemko kwamba kuna nafasi zinahitaji watu matured na wenye utulivu wa akili.

Ccm kwa hili wapo sahihi kwa 100%.
 
Chama Cha Mapinduzi kimempendekeza Ndugu Stephen Masatu Wassira kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasilisha jina la mwanasiasa mkongwe nchini
Stephen Wassira kwa wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM wa Taifa unaofanyika Jijini Dodoma, kwa ajili ya kupigiwa kura kuwa Makamu Mwenyemiti wa CCM Bara.

Wasira aliyezaliwa Julai Mosi, 1945 wilayani Bunda Mkoa wa Mara, kwa zaidi ya nusu karne amejijengea heshima kutokana na mchango wake mkubwa katika siasa, uchumi na maendeleo ya jamii.

Wasira ni miongoni mwa wana CCM waliowahi kutangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Ni mmoja wa viongozi wakongwe wenye ushawishi mkubwa ndani ya CCM, ambapo tangu mwaka 2007 amekuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM tangu mwaka 2011.

Rekodi yake ya uongozi na uchapakazi wake, imemuweka kuwa katika nafasi nzuri ya kuonekana kama nguzo muhimu ndani ya CCM.

View attachment 3205242


Shetani kumchagua zimwi ni yaleyale mambo ya uchawini
 
CCM ina wenyewe na wenyewe ndio hawa kina Wasira, Kinana, Mwinyi, Makamba, Makala, Kikwete. Vijana tutafute kazi za kufanya, wenye chama chao bado wana uwezo wa kuongoza na familia zao. CCM na familia zao mbele kwa mbele, CCM ni ile ile!
 
Back
Top Bottom