Baada ya Mahakama kutamka kuwa Hakimi hamiliki pesa wala mali yoyote, Hakimi akaanza ku trend mitandaoni. Watu wakampatia sifa zenye rangi, harufu na maumbo yote.
Ikumbukwe kwamba, suala hili halijaisha wakati ndiyo kwanza game ipo mapumziko.
Inathibitishika kuwa Hakimi ni muajiriwa, hivyo basi chini ya jina lolote ambapo hela na mali zake zinaenda kuhifadhiwa inakuwa ni salama kwa masuala mengine ya kisheria lakini si kwa mke wake.
Kesi itakayofuata, Hakimi anaweza akahitajika kutoa maelezo ni wapi ambapo pesa na mali alizozipata kutokana na kazi yake amekuwa akizipeleka, maana pesa ile ni mali halali ya familia yake, inakuwaje familia ijikute haina umiliki wa kitu chochote kile?
Vyovyote itakavyokuwa, kesi itakayofuata itamuweka Hakimi mahala pabaya zaidi. Mama yake atahitajika kuelezea chanzo cha mapato cha pesa na mali zilizo chini ya jina lake.
Hii kesi ya kwanza imeishia hapo na ndiyo ina-trend kwa sasa, ila kesi ya pili nabashiri itakuwa mbaya zaidi na huenda Hakimi akajikuta mahala pagumu kuliko Emmanuel Eboue.
Nafikiri hapa tunapenda kuweka sana uwazi katika kutetea kuliko uhalisia.
Tofauti na wenzetu, ndoa ni mkataba na si kuingia kwenye ndoa ndipo mkataba uanze.
Unapotaka kuoa,jambo la Kwanza wanaweka masharti Kama ifuatavyo:-
1: mali za mke kama zipo ziwe za kifamilia au ikiwa watatengana, wanaweza gawanaje?au hizo zote zigawanywe kwa watoto kwa mfumo ambao mama atapenda. Na mume hivyo hivyo ataweza kuweka wazi mali zake ziweje.
2: je mali hizi zitakazopatikana kutokana na ndoa yao,wakitengana zinaweza gawanaje.
Tatizo lipo hapo kwa ngozi nyeusi maana kutokana na kuwa ni wajinga wa mapenzi,ndipo hapo akina Ebou ndipo alikula za kichwa. Mke alisema mali zote atakazopata yeye ni zake na za mshkaji ziwe zake. Bahati mbaya mshkji alikuwa anampa mke hela anunue vitu, mke anaandika jina lake.
3: huenda jamaa alikubali mali wagawane nusu kwa nusu, lakini wakati anafunga mikataba yake,alikuwa bado ni mdogo hivyo Mama ndie alieteuliwa kuwa analipwa na kwa kuwa wenzetu huwa na mikataba ya muda mrefu,hichi ndicho mke wa mshkji hakujua.
Wenzetu wana mikataba ya muda mrefu na hata ukinunuliwa,bado kuna % fulani huenda kwenye academy,kuna kulika kodi,kuna timu iliyomuuza nayo itapata kiasi Fulani mpaka labda timu mbili au 3 ndipo mkataba unaweza fika mwisho na yeye Sasa ndipo anaweza anza kulipwa kama yeye mwenyewe.
Mfano mnakumbuka ishu ya mchezaji wetu huyu MBWANA SAMANTA kuhusu uhamisho wake kwenda TP MAZEMBE na pia genk, timu zote hizi zina % zake pindi akiuzwa hadi hapo genk wakimuuza ndo mwisho wa mkataba, Sasa timu yoyote itakayoingia nae mkataba basi atakuwa free from all contracts na anachukua hela yeye mwenyewe.
Huenda HAKIMI ndio mikataba yake ilivyo na hivyo Mama yake ataendelea kulipwa hadi yeye na Mama yake wakubaliane. Hapa mtoto wa kike hakujua hilo na ndipo mshkji kaponea hapo.
Nakumbuka hata huyu kocha aliekuwa wa Simba JULIO, ana watoto wake wanacheza Quatar, ila kwa kuwa Wana miaka chini ya 18, yeye ndo anaingia mikataba na hela zinaingia kwake na yeye ndo anawapa hela Sasa watoto wake. Je wakioa?kabla ya mkataba wao kuwa bado unaendelea wa Baba yao?mke akileta ujinga anaumia hivi Hivi kama ya Huyu mchezaji.