Suala la Achraf Hakimi na Mke wake: Watu ni wepesi kuongea, hawataki kufanya reasoning

Kweli hawa watu hawafai, Kim ana utajiri wa zaid ya dola bilion 1 kibongo bongo ni trionea.. hajadai kugawana mali kwasababu na yeye ana mali ila angekuwa hana utajiri huo Kanye angekomeshwa
Kabla ya ndoa kuhusu mali walishaweka sawa. Hadi wanaachana mali ambazo zilikuwa za familia ni 70$mil.

Na kuna huyu mwamba mwingine ye siku ya ndoa aliamua kuacha kuoa kabisa sababu ya maswala ya mali. Isome https://www.basketballnetwork.net/o...iancé-after-she-didnt-want-to-sign-the-prenup
 
Baba mlevi hela yote nilikuwa napeleka kwenye kvant na valuu
 
Mahaba yanakusumbua hakuna kiti kinaitwa mali ya familia . Mali ni ya mtu na sheria inamruhusu kutumia anavyopenda. Tofautisha,mali ya urithi na mali ya mtu aliye hai. Ndio maana mtoto hawezi kuhoji baba yzke akiamua kuuza nyumba au kuweka wakfu mali yake. Kuna watu hata hapa Bongo pesa zao nyimgi wanapeleka makanisani. Huko ulaya na Marekani matajiri kadhaa wanatoa mabilioni ya pesa zao kwa charity na hawajawai kuhojiwa. Ukiamua kumjengea nyumba au kumnunulia gari hawara na ikajulikana waziwazi huwa sio kosa ndio maan haihojiwi.

Huyo mama mzazi hawezi pata shida yeyote ya kuitwa mahakamani ikiwa kesi hiyo itaendelea, mtu anaweza kuhojiwa uhalali wa mali zake kwenye tuhuma za jinai za kujipatia mali kiharamu sio kupewa na mtu.

Kama wewe mali yako ni ya familia ni wewe tu sio kila mtu wengine mali ni zao binafsi hadi watakapokufa ndipo zitarithiwa.
 
Ngoja nikuulize kistaarabu tu, hivi unadhani wale ambao mali zao hugawanywa ni sababu wao hawakuwa wakifanya kazi?
Unagawanya kitu ambacho kipo in mume au mke’s name. Utagawanyaje kitu, mtu alimpa baba ake au mama ake? Huwa mnatumia nini kufikiria?
 
unaonekana ni mbobezi kwenye sheria kwanini hukwenda au usiende kumsaidia emmanuel eboue?
 
Aisee, ahsante mtaalam
 
Unagawanya kitu ambacho kipo in mume au mke’s name. Utagawanyaje kitu, mtu alimpa baba ake au mama ake? Huwa mnatumia nini kufikiria?
Tatizo mnajenga hoja katika msingi wa kesi hii ambayo imekwishaamuliwa. Hamtaki kuangalia kama madai yataletwa kivingine
 
Nafikiri hapa tunapenda kuweka sana uwazi katika kutetea kuliko uhalisia.

Tofauti na wenzetu, ndoa ni mkataba na si kuingia kwenye ndoa ndipo mkataba uanze.
Unapotaka kuoa,jambo la Kwanza wanaweka masharti Kama ifuatavyo:-
1: mali za mke kama zipo ziwe za kifamilia au ikiwa watatengana, wanaweza gawanaje?au hizo zote zigawanywe kwa watoto kwa mfumo ambao mama atapenda. Na mume hivyo hivyo ataweza kuweka wazi mali zake ziweje.

2: je mali hizi zitakazopatikana kutokana na ndoa yao,wakitengana zinaweza gawanaje.
Tatizo lipo hapo kwa ngozi nyeusi maana kutokana na kuwa ni wajinga wa mapenzi,ndipo hapo akina Ebou ndipo alikula za kichwa. Mke alisema mali zote atakazopata yeye ni zake na za mshkaji ziwe zake. Bahati mbaya mshkji alikuwa anampa mke hela anunue vitu, mke anaandika jina lake.

3: huenda jamaa alikubali mali wagawane nusu kwa nusu, lakini wakati anafunga mikataba yake,alikuwa bado ni mdogo hivyo Mama ndie alieteuliwa kuwa analipwa na kwa kuwa wenzetu huwa na mikataba ya muda mrefu,hichi ndicho mke wa mshkji hakujua.
Wenzetu wana mikataba ya muda mrefu na hata ukinunuliwa,bado kuna % fulani huenda kwenye academy,kuna kulika kodi,kuna timu iliyomuuza nayo itapata kiasi Fulani mpaka labda timu mbili au 3 ndipo mkataba unaweza fika mwisho na yeye Sasa ndipo anaweza anza kulipwa kama yeye mwenyewe.
Mfano mnakumbuka ishu ya mchezaji wetu huyu MBWANA SAMANTA kuhusu uhamisho wake kwenda TP MAZEMBE na pia genk, timu zote hizi zina % zake pindi akiuzwa hadi hapo genk wakimuuza ndo mwisho wa mkataba, Sasa timu yoyote itakayoingia nae mkataba basi atakuwa free from all contracts na anachukua hela yeye mwenyewe.

Huenda HAKIMI ndio mikataba yake ilivyo na hivyo Mama yake ataendelea kulipwa hadi yeye na Mama yake wakubaliane. Hapa mtoto wa kike hakujua hilo na ndipo mshkji kaponea hapo.

Nakumbuka hata huyu kocha aliekuwa wa Simba JULIO, ana watoto wake wanacheza Quatar, ila kwa kuwa Wana miaka chini ya 18, yeye ndo anaingia mikataba na hela zinaingia kwake na yeye ndo anawapa hela Sasa watoto wake. Je wakioa?kabla ya mkataba wao kuwa bado unaendelea wa Baba yao?mke akileta ujinga anaumia hivi Hivi kama ya Huyu mchezaji.
 
wanaume tunahangaika ,tunajinyima af mtoto wa mtu anajitegesha ,baadae pasu kwa pasu .hii haikubaliki kama watoto waachwe wakalelewe na mama hakimi
 
Hamna lolote wivu tu...mamaza sijui wakoje?
 
Mimarioo ya kibongo nayo inazungumza na kushabikia alichokifanya Hakimi jamani?

Nimeona hata insta kwa Hakimi, imejaa huko eti inamsifia, mengine yanaandika kiswahili kabisa! Ovyoo sana
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kweli kabisa mkuu. Jamaa yangu ilishamkuta hiyo na mzazi wake alipiga stop aliposikia mwanae ana mahusiano na binti fulani akaamua kufanya udadisi na kilichofuata ni kumwambia kijanawe apige chini huyo mwanamke ingawa jama alikuwa akimsomesha demu,anakaa naye geto na hapo alishaanza kuhudumia familia yake kwa kiasi cha juu.hakika jamaa hajawahi kujuta zaidi ya kushukuru hilo na kumuoa mtu mwingine ambapo ni full amani tu zaidi ya miaka 5 sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…