Suala la ardhi Zanzibar: Askofu Augustino Shayo apiga msumari wa moto mbele ya Rais Mwinyi

Suala la ardhi Zanzibar: Askofu Augustino Shayo apiga msumari wa moto mbele ya Rais Mwinyi

hakuna watu wana roho mbaya kwa wabara kama wazanzibari. ukienda kule wanakubagua kwa kuangalia kichogo. ukiingia marikiti bei anouziwa mzanzibari si sawa na wewe mwenye chogo kwa bidhaa ileile.
 
Mhashamu Askofu Augustino Shao wa Zanzibar ametimiza Jubilei ya miaka 25 katika utumishi wa kanisa la Roman Catholic huko Zanzibar.


Kwenye sherehe zilizohudhuliwa na wananchi mbalimbali wakiwemo viongozi wa kidini, askofu Shao kwenye salamu zake kwa Rais wa Zanzibar, amezungumzia mambo mbalimbali aliyokumbana nayo akiwa katika utumishi wa kanisa, moja au baadhi ni Usafirishaji haramu wa watu kwenda nje ya nchi na uhamiaji wanatumika kutoa pasipoti pasipo utaratibu.

Amesema watu wanasafirishwa nje kwa kuhadaiwa kazi nzuri lakini mbele wanabadilishiwa kile walicho aidiwa na kwenda kufuga nguruwe au kazi za hatari.

Kwa upande mwingine ameongelea kuhusu aridhi ambapo ni tatizo kubwa Zanzibar, yaani mkristo kupata aridhi ni haiwezekani, hasa ukifahamika kutoka bara kama yohana upewi.

"Siyo kila mkristo anakuja kujenga kanisa, kanisa halijengwi na familia bali na taasisi kama madhehebu, alisema askofu Shoo.

Aliiomba Serikali ifikilie wanapopima viwanja waweke kipaumbele pia kwa mashirika na taasisi za kidini, sababu kanisa linatizama mbele na si kuwapa kiwanja size ya 20x20.

Aliongeza kuwa "katiba inatoa nafasi kwa raia kuwa na usawa,haiwezekani ukienda bara unachukua aridhi ila ukija zanzibar upewi, ifike mahari tuangalia usawa, ukipenda kula vya mwenzako na wewe kubali kuliwa vyako".
Walioona faida ya huu muungano wameondoka, mimi sioni hata kidogo.
 
Mimi siwezi kuchangia kwa sababu amesema ukweli kuwa Mtanganyika ukiwa Zanzibari hutambuliwa kama mgeni kutoka nje ya nchi (zamani ilikuwa ni lazima uwe na passport) ila mzenji akija Tanganyika anajulikana kuwa ni Mtanzania mwenzetu.

Ni mkweli kuwa wakristu Zanzibar huonekama kama ni mashetani ingawa siyo kwa wazi wazi sana, lakini swala la utanganyika na Uzanzibari liko wazi sana.
 
Mhashamu Askofu Augustino Shao wa Zanzibar ametimiza Jubilei ya miaka 25 katika utumishi wa kanisa la Roman Catholic huko Zanzibar...
Vipi kuhusu mkristo kuwa rais Zanzibar? Yaani Tanganyika inaweza kuwa na rais mzanzibari ila Zanzibar kuwa na rais kutoka bara ni marufuku( strictly prohibited)
 
hii ndio sababu mojawapo inayonifanya nione kichefuchefu kwenye muungano...na nikikutana na mzanzibari nisiwe na moyo wa kushirikiana naye. mtaniwia radhi kwa kusema ukweli ulioko moyoni mwangu. kwasababu hata kwa raia wa kawaida achana na institutions...
Na viongozi wa ccm wanona ni kawaida kabisa. Na wanaimba ngojera kila siku muungano ni imara na hauna shida

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Kinachonikera ni kuitusi dini ya kiislamu kwa ajili ya zanzibar basi.

Zanzibar sio dini,
Wanaofanya hayo ni wazanzibar na sio uislam,
Dini ni imani na wazanzibar ni binadamu tu,
Mimi mwenyewe nakerwa na wazanzibar kwenye vipengele vya ajira,n.k
Wabara wanatengwa sana kule ila wazanzibar huku wanaennoy maisha,
Kiufupi HAKUNA USAWA

Sent from my PBBM00 using JamiiForums mobile app
 
Mhashamu Askofu Augustino Shao wa Zanzibar ametimiza Jubilei ya miaka 25 katika utumishi wa kanisa la Roman Catholic huko Zanzibar...
Hivi ukienda Moshi unaweza kupata hata inchi moja ya ardhi?
 
Back
Top Bottom