Suala la Madini: Serikali ya Magufuli haikutueleza ukweli wote

"Mimi sishauriki, ukinishauri ndiyo naharibu kabisaaaa" - Jiwe-2016
Hapo ulitaka Mama afanyeje ndugu Taga?
 
SSH ana wenge anataka kuuza kila kitu, hivi mkataba wa zamani wa Barrick na wa saivi upi bora? Hapo ameshawakaribisha wa gesi Mtwara LNG waje tu atawaruhusu kwa masharti yoyote, Hellium mbugani, huyu anataka kuuza kila kitu, hizo kwake ndio akili.

Ningekuwa mimi ningeanza kuwauza Mataga wote nikianza na wewe, sijui kwanini Mama anawalea sana
 
Mama alinisikitisha sana jana kutokana na kauli zake. Hana power ya ku negotiate huyu. Na angekuwa ni Rais toka mwanzo hata hiyo 16% tusingeipata. Mimi najua ugomvi uliobaki na Barick ni kipengele cha kodi ambayo serikali inasema inawadai Barick. Sikuona haja ya kusema maneno aliyoyasema hapo. Ni kweli Business ni win win situation lakini kwa kusema hadharani eti sisi tuwanyenyekee kwasababu tunawahitaji zaidi ilifanya niumie kama Mtanzania. Unaweza ukakubaliana nao ukasema hili la kodi za nyuma tunalifuta na tunaanza upya full stop na si kuwapa wale jamaa viburi. Kila nchi Mungu amewapa rasilimali zao, wakitumia vizuri zinawatoa na kuwaaidisha. Serikali ya Hayati Magufuli anagalau walipata USD million 300 (zaidi ya Billion 700 toka Barick na tukaunda Kampuni ya pamoja ya Twiga.

Changamoto zipo lakini mama aangalie yapi ya kusema kwenye media. Mimi kwasasa kama Mtanzania nitabaki mtazamaji kwanza mpaka nimuelewe mama Philosophy yake ni ipi. Nikasikia tena juzi nilishinda mtandaoni naaangalia vitu nikasema tatizo jingine linakuja. Anaweza wasahau wengi kwa manufaa ya wachache. Uzuri hesabu hazidanganyi na Muda ni tabibu mzuri. Tusubiri tuone. Ila namtakia kila la heri. Akifanikiwa katika kazi yake wamefanikiwa kama watanzania, akiyumba tunayumba wote.

Tuanze kupambania Katiba Mpya, Reforms za Mahakama, Bunge, Sheria za Vyombo vya habari n.k. Ninatamani sana kuiona Tanzania yenye neema na iliyo mfano kwa dunia Nzima kuanzia Uchumi, Demokrasia, Usawa wa kijinsia, haki za binadamu, Siasa za Kistaarabu na enye tija kwa nchi na Uzalendo wa kuipenda nchi yetu na kulinda Rasilimali zetu. Home Sweet Home Tanzania.
 
Hisia hizi japo zinaweza kuwa kweli, nakupa 50/50.
 
Kuna mmoja alijenga International Airport kijijini kwake akidhani ndiyo uchumi, Mataga zamu hii lazima mtage kabisa, hama nchi mkuu
 
Usijigeuze msemaji wa Rais, wacha hoja mezani ijadiliwe.
 
SSH ana wenge anataka kuuza kila kitu, hivi mkataba wa zamani wa Barrick na wa saivi upi bora? Hapo ameshawakaribisha wa gesi Mtwara LNG waje tu atawaruhusu kwa masharti yoyote, Hellium mbugani, huyu anataka kuuza kila kitu, hizo kwake ndio akili.
Unaropoka ndugu, kuna mahali amesema anataka kuvunja mkataba? Alichokisema kuna mambo ya Kodi hayako sawa inawezekana tunalipwa midogo au kuna mkanganyiko wa kulipa kodi
 
Nyie Sukuma Gang mulishindwa mkaendekeza ukanda ukabila pamoja ba limbukeni zenu sasa munaanza kupiga lamuli duh....kweli ndani ya wiki tatu unataka Mama atekeleze nini? Mumeibia nchi wee kwa kujificha nyuma ya mgongo wa kizalendo eti munasaidia wanyonge.......ila Mungu sio Osman Meko kaanga dunia
 
"Mimi sishauriki, ukinishauri ndiyo naharibu kabisaaaa" - Jiwe-2016
Hapo ulitaka Mama afanyeje ndugu Taga?
Actually ni ufinyu wa mawazo kumuita "taga" au "nyumbu" yeyote aliye na mtazamo tofauti na wa kwako. Huu ni ugonjwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…