Hiyo tovuti Nani administrator? Kama aliajiri IT mbugila akashindwa ku upload?Siku hizi umeishiwa kabisa ufahamu mkuu, yaani kwenye tovuti ya Serikali kuna picha za CAG's wote tangu Uhuru, tangu wazungu hadi Utoh wa juzi, lakini Assad wa Jana hayumo na wewe unapelemba kuunga mkono upuuzi!!?
Hivi Mkuu huwa tunasoma between the line? Kwa mantiki hiyo hata hiyo kumi haihitajiki kwani umri wa kustaafu ni miaka 65 kwa mujibu wa sheria. sio mitano, kumi wala kumi na tano.Hawa jamaa hawana logic wanaendeshwa na emotions, swali zuri hilo, kama ni automatic kwa nini waweke hiyo miaka 5 na wasiseme 10?
Assad asingekubali kuficha ufisadi wa ATCL lakini huyo wa leo kichere anaenda kukagua hesabu zao kisha kuleta majibu ambayo yatamuuzi mpaka Nyerere kawawa wakiwa kaburiniATCL umefanyika uhuni mkubwa sana.
Watu wamekataza CAG asikague vitabu, halafu wakatangaza faida ya dola milini 14!
Sasa kwa msimamo wa Assad uchafu kama huu kuficha mwaka baada ya mwaka ingekuwa tabu.
Assad inatakiwa apewe kazi nje ya Tanzania, halafu afunguke kimetokea nini mpaka katolewa.
Magufuli kavurugwa na washauri wake ingawa sidhani kama mama samia na waziri mkuu wamo kwenye list ya washauri wabaya kwa magufuliKatiba na sheria naona zimevunjwa na kusiginwa Kabisaaaaaaa openly bipolar disorder ugonjwa mbaya sana.
Nafahamu kwamba watu wengi wameanzisha threads wakijaribu kuelezea suala la CAG Kisheria! Hata hivyo, wengi wao kama sio wote walichofanya ni kurundika vifungu vya kisheria bila kutoa ufafanuzi!
Mbaya zaidi, hawatoi ufafanuzi wa matumizi ya neno SHALL kwa mujibu wa sheria zetu! Nimelazimika kuanzisha uzi huu ili kuondoa mapungufu yote hayo.
Tuendelee.
Bila kujaza vifungu vingi, Katiba yetu Ibara ya 144 (1) inasema wazi kwamba:-
Kwamba, CAG ATALAZIMIKA kuachia ofisi akifikisha miaka 60 au umri mwingine wowote utakaotajwa na sheria zilizotengenezwa na Bunge!
SWALI 1: Je, Profesa Mussa Assad amefikisha miaka 60?! Jibu HAPANA kwa sababu kumbukumbu zinaonesha amezaliwa Oktoba 06, 1961... kwa maana nyingine, atafikisha miaka 60 Oktoba 5, 2021.
SWALI 2: Je, Bunge limetaja huo UMRI MWINGINE WOWOTE?!
Jibu linapatikana kwenye Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma, yaani Public Audit Act ya mwaka 2008, Ibara ya 6(2)(a) inayosema:-
Kumbe, Bunge likatunga sheria kwamba badala ya miaka 60, hatimae CAG ATALAZIMIKA kuachia ofisi akifikisha miaka 65. Tumeona Prof Assad ndo kwanza ana miaka 58.
SWALI 3: Nini hutokea CAG akimaliza miaka 5 ya kwanza?!
Hapa tena jibu linapatikana kutoka Public Audit Act 2008 Ibara ya 6 (1) inayosema:-Hapo kwenye neno SHALL ndipo panapozua mgogoro!!
Watetezi wa uamuzi wa Rais wanasema neno SHALL sio shuruti! Kwa bahati mbaya sana, tafsiri yao wanaitoa kichwani na sio kwa mujibu wa sheria zetu!
Kwa mujibu wa sheria zetu, na kwa kuangalia Interpretation of Laws Act Ibara ya 53 (1&2) inasema kwamba:-
Kumbe, kwa mujibu wa sheria zetu, pasipo na SHURUTI hutumika neno MAY lakini linapotumika neno SHALL, hiyo ni SHURUTI!
Kwa maana nyingine, Public Audit Act inaposema "...and shall be eligible for renewal for one term only. Hapo suala la renewal ni SHURUTI kama ilivyosema Interpretation of Laws Act 53 (2).
Itakuwa sio SHURUTI either kama ameshafikisha miaka 65, au kama ambavyo 2008 Public Audit Act Ibara ya 6(2)(a) inavyosema kwamba:-Kwa maana nyingine, kwavile Prof Assad hajafikisha miaka 65, hapo tafsiri yake ni kwamba AMETUMBULIWA na sio kwamba muda wake umeisha!!
Na CAG atatumbuliwa "...Unless the question of removal becomes the subject of investigation in terms of Article 144(3) of the Constitution."
Hiyo Ibara ya 144(3) ya Katiba yetu inasemaje? Jibu ni hili:-If the President considers that the question of the removal of the Controller and Auditor-General from office under the provisions of this Article needs to be investigated, then the procedure shall be as follows:Kama tulivyoona hapo juu, CAG atalazimika kuachia ofisi endapo atakuwa amefikisha miaka 65, kinyume chake anaweza KUTUMBULIWA kabla ya huo umri ikiwa ametenda jambo linalohitaji investigation.
Hivyo basi, ni ama Rais atengue uamuzi wake wa awali wa kuteua CAG mwingine, au tuone akiunda Tume ya Kijaji ya Kumchunguza CAG kwa kosa analojua yeye na timu yake!!
CAG akiongezewa miaka mingine 5, ataimaliza akiwa na umri wa miaka 63... umri halali kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma ya mwaka 2008!!
Mimi naona nyinyi ndiyo mna mihemko maana mnalazimisha kutafsiri sheria mnavyotaka nyieTatizo Raisi amefanya haya kwa Mihemko, Kudanganywa na Kujidanganga, Kushauriwa vibaya na Kujishauri vibaya na On top of that Kwa CHUKI binafsi.
Raisi amevunja Katiba ALIYOAPA kuilinda huku akimtaja MUNGU anayedai kumtanguliza mbele'
Tatizo la wa TZ hatusomi na kutafakari. Rudia tena kusoma na kutafakari uzi wa mleta madaMleta mada unahangaika na neno shall unasahau neno eligible !! Kuteuliwa Soo automatic kunategemea eligiblity pia .Chukulia CAG labda ni kibaka kwa hiyo.umuongezee muda tu kwa ku base neno shall !!!
Bila ku consider eligible?
Pili hata Kama angepewa ingeleta usumbufu usio na sababu.Katiba inasema umteue kwa miaka mitano na anatakiwa kustaafu akiwa na miaka 60 ina maana Raisi angempa U CAG angevunja Katiba sababu anampaje mtu miaka mitano anayejua kabisa miaka 60 anatakiwa kuondoka .Akimpa mitano kavvunja Katina kampa mtu ambaye hastahili sababu ya umri na katiba haisemi apewe u CAG kwa miaka miwili.Raisi angempa angekuwa kavunja katiba
Umri wa CAG Assad kuteuliwa kikatiba ulikuwa umefikia ukomo
Tuangalie sheria na mantiki.
Tusiandike kwa hisia zinazoongozwa na jazba za kisiasa.
Magufuli anavunja katiba, sana tu.
Mfano, kupiga marufuku mikutano ya kisiasa ni kuvunja katiba wazi.
Katiba inatoa "right to assembly" wazi kabisa.
Hatuhitaji kutunga uongo kwamba Magufuli kavunja katiba kwenye suala la CAG.
Kutunga uongo kwenye hili kutafanya hata tunaposema kweli Magufuli anapovunja katiba kweli, tuonekane tunazusha uongo.
Hajafanywa kitu.Kwahiyo alipovunja katiba kwenye mikutano ya kisiasa kafanywaje kama aliapa kuilinda na sasa kaivunja tuanzie hapo kwanza maana hajavunja jana tangia 2016
Mleta mada unahangaika na neno shall unasahau neno eligible !! Kuteuliwa Soo automatic kunategemea eligiblity pia .Chukulia CAG labda ni kibaka kwa hiyo.umuongezee muda tu kwa ku base neno shall !!!
Bila ku consider eligible?
Pili hata Kama angepewa ingeleta usumbufu usio na sababu.Katiba inasema umteue kwa miaka mitano na anatakiwa kustaafu akiwa na miaka 60 ina maana Raisi angempa U CAG angevunja Katiba sababu anampaje mtu miaka mitano anayejua kabisa miaka 60 anatakiwa kuondoka .Akimpa mitano kavvunja Katina kampa mtu ambaye hastahili sababu ya umri na katiba haisemi apewe u CAG kwa miaka miwili.Raisi angempa angekuwa kavunja katiba
Umri wa CAG Assad kuteuliwa kikatiba ulikuwa umefikia ukomo
Nimekuelewa kama ambavyo kila tasnia wanatafsiri zao za maneno kutokana na kada yao. Mfano wauguzi, watu wa teknohama, wahandisi, wanasheria n.k.
Sasa kama alivyosema Kiranga na mimi nimeuliza hicho kitu jana. Kulikua na ugumu gani kuweka moja kwa moja kwamba ni muhula mmoja wa miaka kumi?
Nyani Ngabu rais wangu tumejitahidi kutaka kupata maelezo kuhusu hili, kwa bahati mbaya hakuna aliyeweza kuja na kitu chenye mashiko.
Niliishia kusema basi katiba yenyewe itakua ya hovyo kuliko wanaoivunja.
Kwamba neno eligible limewekwa tu halina uzito au maana yeyote? Ikiwa ni hivyo kwanini basi na neno shall lisiwe limewekwa tu?
Mkanganyiko unaanzia kwenye Katiba yenyewe.
The problem umetumia general English use kwenye masuala ya kisheria!
Katiba yetu Ibara ya 144 (1) inasema wazi kwamba:- kwamba ATALAZIMIKA kuachia office akishafikisha miaka 60! Je, Profesa Assad aliyezaliwa Oktoba 6, 1961 ameshafikisha miaka 60?!
Na hiyo phrase yako uliyotumia, kutoka Public Audit Act 2008 Ibara ya 6 (1) inasema:-Hilo neno SHALL umelitafsiri kwa Kiingereza na sio kwa lugha ya kisheria!!
Pasipo na shuruti, katiba na sheria zetu zinatumia neno MAY na sio SHALL kama inavyoelezwa kwenye Interpretation of Laws Act Ibara ya 53 (1&2) kwamba:-
Sasa kwa kuangalia tarehe ya kuzaliwa ya Prof Assad, ni kwamba atatimiza miaka 60 Oktoba 6, 2021!
Je, hawezi kuongezewa miaka mingine 5 kwa sababu hadi miaka 5 kwisha atakuwa amevuka miaka 60?! Jibu ni kwamba, katiba imesema wazi kwamba:- "upon attaining the age of sixty or any other age which shall be prescribed by a law enacted by Parliament."
Je, Bunge limetunga sheria yoyote kuhusu hiyo ANY OTHER AGE?!
Jibu ni NDIYO, 2008 Public Audit Act Ibara ya 6(2)(a) inasema:-
Summing up, unless kama CAG kafanya jambo la litakalosababisha kuwa under investigation, he shall be eligible for renewal. Na mkataba wake ukiwa renewed, atamaliza miaka 5 mingine mwaka 2024 ambapo atakuwa na umri wa miaka 63!
So, unless kama wameshamtengenezea kesi, jambo ambalo kwa utawala huu hakuna kinachoshindikana, kinyume chake, Rais amevunja sio tu katiba bali pia Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma ya mwaka 2008!
Hivi ili rais akifuata hicho kifungu cha utaratibu wa kumuondoa CAG lazima atangaze? Sasa nyinyi nyote mnaopiga porojo kwamba katiba imevunjwa mna uhakika gani kwamba hajaunda hicho chombo kwa mujibu wa ibara mnayoizungumzia? Labda niletewe kifungu kinachoonyesha kwamba rais akiwa anatekeleza hiyo ibara ya 144 ya katiba ni lazima atangaze. Lakini kama hakipo, basi wanaoamini kwamba rais kavunja katiba wanatakiwa wareverse pia akili yao waamini kwamba rais hajavunja katiba. Rais kasema 'Duniani ukipewa mamlaka ya kuteua, unapewa pia mamlaka ya kutengua' nimeipenda sana hii na ndo uhalisia. Mtu akuteue alafu ashindwe kukutengua.
...can be removed for misbehaviours...
Let me ask you this...
Shall be eligible for renewal and shall be reappointed for another 5 year term.
Which one of those expresses a necessity and which one expresses a possibility?
I feel like I’m back to being an English teacher again 🤣