Suala la Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Vipengele kadhaa vya Kisheria

CAG ameongea kutafuta huruma ya Wananchi kama kawaida yake ili aonekane ameonewa wakati mkataba wa kazi ni miaka mitano

Kila mtanzania mwenye sifa alistahili kuwa CAG,professor Asad aache uswahili

Tumheshimu Rais wa Nchi anafanya kazi kubwa
 
  • Thanks
Reactions: Dua
Kwa hiyo sheria inalazimu CAG afanye kazi yake kwa miaka 10 na si miaka mitano mitano?

Well, naona maneno ni mengi mno kwenye hili suala.

Kama Shivji alikosea awali, hata sasa anaweza akawa kakosea pia.

Recourse ni kwenda mahakamani tu.

Lakini hata huko watu wataenda wakiwa tayari mitazamo yao iliyo prejudiced.

Kama masuala mengine yaliyotangulia, hili nalo litaishia kuwa litigated mtandaoni tu.

Bottom line, shall be eligible for renewal is not the same as shall be renewed.

Katiba inatambua namna mbili tu za CAG kuachia madaraka. Kustaafu ama kuondolewa kwa taratibu ambazo zimeanishwa kwenye Ibara 144 (2_3).

Hiyo sheria ya Renewable contract sijajua inaingiaje hapo kwenye Ibara tajwa hapo juu.

Hii inshu ningependa ifike mahakamani ili ufafanuzi upatikane.
 
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria

Kama wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata hati chafu ya ubadhirifu wa pesa
Kwa nini unahusisha masuala ya upinzani kwenye masuala muhimu ya kitaifa kama hili? Hivi watz tukoje basi tumuombe Mungu sana aturehemu!
 
Pongezi kubwa kwa Prof. Assad kwa utumishi uliotukuka, ijapokuwa weledi na maadili yako ulikuwa mwiba kwa wengine. Kwa hakika historia yako imeandikwa kwa wino wa dhahabu, ambapo si ajabu ukaaminiwa na IMF ama WB na kukabidhiwa nafasi mpya unayostahili.

Aidha, pongezi pia kwa CAG mteule, mtangulize Mola mbele kwa nafasi hii mpya ulioaminiwa na kukabidhiwa kwa maslahi mapana ya uzalendo na taifa letu, hilo ni kama zigo la misumari endapo utaweka maadili na weledi kando ili upate kufuraisha watu fulani, haswa kwa yale yenye makandokando mengi.
Tayari nasikia keshapata mkataba na serikali ya Sweden. pacemaker itachomoka safari hii
 
Kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi ya Taifa Na. 11 ya Mwaka 2008 kifungu cha 6(1) "basic tenure" ya CAG ni miaka mitano na sheria inasema anaweza (Shall) kutumikia vipindi viwili vya miaka mingine mitano.

CAG anaulinzi mkubwa kisheria na moja ya ulinzi wake ni kuwa akiwa katikati ya tenure yake hawezi kuondolewa hivi hivi bila masharti kadhaa kufuatwa, lazima utumie masharti ya Ibara ya 144(3) ya Katiba au yeye mwenyewe achukue hatua under subsestion 2 ya hiyo Sheria ya Ukaguzi niliyoitaja hapo juu. Lakini kwa ujumla anaweza kuondolewa, si ngumu. Nitaeleza.

144.jpg

Matumizi ya neno "Shall" lililotumika katika Sheria ya Ukaguzi kwenye kifungu cha 6 .

Kwa heshima na taadhima, Sheria hapo haijakusudia ulazima na ndio maana sheria haifasiriwi kwa matakwa ya mtu bali sheria zenyewe zinavyokusudia kufasiriwa katika muktadha wa jambo husika na lengo la mtunga sheria.

Katika muradi wa sheria na taratibu za kiutawala (admimistrative law point of view) sheria zinajulikana kuwa zitajitafsiri zenyewe na msingi unaokubalika ni kuwa kila ambapo tenure inapomalizika na kuwepo kwa kanuni ya kuongezewa tena kipindi cha pili neno "Shall" halina maana kama ilivyo katika Sheria ya Kufasiri Sheria (The Interpretation of Laws Act), hapa maana huwa ya kimazingira zaidi (contextual meaning) na haiwi LAZIMA bali INAWEZA.

Na moja kwa moja ni kuwa kuongezewa kipindi cha pili Mtendaji yeyote mwenye vipindi viwili na hata Rais mwenyewe sio "automatic" lazima kuwe "subject to good performance."

Na anayeamua akuongezee tenure ya pili, hiyo sheria haijambana, ni yule yule mwenye mamlaka ya kuteua na kukutengua.

Rais anapewa mamlaka hayo kwa CAG na watendaji wengine Serikali aliowateua kwa sheria yoyote kwa mamlaka aliuonayo katika Ibara ya 36. Tena 36(3) ndio inampa mamlaka ya jumla zaidi ya kudeal na tatizo lolote kwa nia ya kuweka utulivu katika utumishi kwa kuweza kumtengua mtu yeyote aliyemteua.

to Remove.jpg

Ukifasiri neno "shall" katika Sheria ya Ukaguzi ili kumtetea CAG Assad kwamba ilikuwa lazima aendelee miaka mitano ya pili ni kuleta dhahama kubwa nchini inayoweza kushawishi hata Uchaguzi Mkuu wa Mwakani usifanyike. Najua utashangaa!!!

Ndio, tafsiri ya Zitto na wenzake ni ya hatari zaidi kwa nchi kwani ukisoma Ibara ya 40 ya Katiba inapozungumzia Rais aliyeko madarakani kwa kipindi cha miaka mitano ya mwanzo kuwa anaweza kuchaguliwa tena kwa miaka mingine mitano ya pili na ya mwisho neno lililotumika ni "shall."
No need for Presidents  Election.jpg

Kama tafsiri SISISI na "#shallow" ya ACT ni ya kufuatwa basi kwa muktadha wa neno "Shall" pia katika Ibara ya 40 ya Katiba, Rais Magufuli naye mwakani hakuna haja ya kupimwa utendaji wake kwa kurudi katika sanduku la kura, aendelee tu, kusiwe na uchaguzi, aapishwe moja kwa moja kuendelea na Urais maana "shall" ina maana ya LAZIMA.

Lakini hapana, muradi wa "shall" katika masuala ya utawala sio kama inavyotumika katika sheria za kawaida, hapa bado dhana ya mhusika kuwa "subjected to good performance" kwa kutazamwa utendaji wake kama unaridhisha mamlaka ya uteuzi (kwa kesi ya CAG) na kwa kurudi kuomba kura tena kwa wananchi (kwa kesi ya Rais) ndio utaratibu kabla ya kulamba awamu ya pili.

Kitaalamu ni kuwa CAG aliyemaliza muda wake hakuonewa na kama ni kuonewa au aliyemteua ana nia mbaya angeweza kuondolewa hata kabla hajamaliza miaka hii mitano.

Ibara ya 144(2) inampa madaraka Rais kumuondoa CAG kwa sababu ya utendaji mbovu, maradhi au sababu nyingine yoyote.

144.jpg

Nimeona wengi wanasema Rais hawezi kufanya hivyo mpaka aunde Tume, si kweli. Watanzania tuachane na kasumba ya kutosoma kwa umakini.

Tuzisome sheria vyema na tunaposhindwa kuelewa tuwatafute wataalamu sio wanasiasa.

Katika Ibara ya 144(3) Rais ataunda Tume (If) kwa maana ya "kama" ataona kuchunguza sababu hizo za kumuondoa CAG kunafaa kuchunguzwa. Maana yake akijiridhisha hana haja ya kuunds Tume.

144.jpg

Kisheria na Kikatiba, namsifu sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk Magufuli na wataalamu wake wa sheria, hakika ni wabobezi, wanazisoma sheria zetu kwa utulivu na kuzifasiri kwa mujibu wa viapo vyao.

Naamini Rais Mhe. Dk Magufuli hakuwa na jambo baya la kutaka kumfukuza CAG isipokuwa "subject to good performance" anahitaji kasi zaidi katika eneo hilo na utulivu zaidi na kuaminika zaidi kwa kiongozi wa muhimili huo ambako Assad alishafeli kwa kufikia hatua ya kugombana na mhimili wa Bunge.

Kwa uchambuzi huu kudai Rais kavunja Sheria ni uchochezi mkubwa usiofaa kufumbiwa macho.

/chanzo Wakili wa Kujitegemea fb
 
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria

Kama wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata hati chafu ya ubadhirifu wa pesa

CAG pumzika acha kutumika na wanasiasa walioishiwa hoja
 
We ni mwongo kajifunze english, toka lini na neno SHALL likatafsiriwa kwa anaweza? Na neno MAY tutalitafsiri vipi? acha upotoshaji.
 
Aaaagh, CAG, CAG, CAG. Imetosha, hata mrundike mivifungu elfu, ndo ishakuwa hiyo.
 
Wanasiasa wanalazimisha jambo amabalo halina mjadala, hakuna kipengele chochote kwenye katiba kunacho lazimisha CAG apewe muhula wa pili. Hata kama kazi yake ni nzuri au mbaya, cha msingi mwenye mamlaka ya kuteuwa CAG mpya ana uwezo wa kuteuwa mwingine pindi muhula wa CAG aliyeko madarakani umekwisha. (Na muhula wa CAG ni miaka mitano)
 
Wabongo katika ubora wa ujuaji wetu, pale ukumbinj kulikuwa na majaji na mavazi yao mekundu.
Lakini ni kama wote wale sheria hawazijua ila members humu ndani ndio wenye kujua kila kitu.
 
Hahahaaa!

Humu mitandaoni watu wengi wana ‘solution’ ya maendeleo [kinadharia tu, of course].

Lakini ukiwapa majukumu wayageuze mawazo yao kuwa vitendo, ni bure tu!!
 
Mbona kuna nguvu nyingi sana inatumika kutetea hili swala? Mwenzio anakwambia ata mwaka mmoja anakuondoa.

Tukubali tu Magufuli anapenda kuvunja katiba.
 
Hahahaaa!

Humu mitandaoni watu wengi wana ‘solution’ ya maendeleo [kinadharia tu, of course].

Lakini ukiwapa majukumu wayageuze mawazo yao kuwa vitendo, ni bure tu!!
Tunatumia nguvu kubwa katika kuyaongelea mambo ambayo kiuhalisia tulipaswa kuelimishwa na wenye fani zao.

We argue about issues which we partially know of.
 
Kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi ya Taifa Na. 11 ya Mwaka 2008 kifungu cha 6(1) "basic tenure" ya CAG ni miaka mitano na sheria inasema anaweza (Shall) kutumikia vipindi viwili vya miaka mingine mitano.

CAG anaulinzi mkubwa kisheria na moja ya ulinzi wake ni kuwa akiwa katikati ya tenure yake hawezi kuondolewa hivi hivi bila masharti kadhaa kufuatwa, lazima utumie masharti ya Ibara ya 144(3) ya Katiba au yeye mwenyewe achukue hatua under subsestion 2 ya hiyo Sheria ya Ukaguzi niliyoitaja hapo juu. Lakini kwa ujumla anaweza kuondolewa, si ngumu. Nitaeleza.

View attachment 1253918

Matumizi ya neno "Shall" lililotumika katika Sheria ya Ukaguzi kwenye kifungu cha 6 .

Kwa heshima na taadhima, Sheria hapo haijakusudia ulazima na ndio maana sheria haifasiriwi kwa matakwa ya mtu bali sheria zenyewe zinavyokusudia kufasiriwa katika muktadha wa jambo husika na lengo la mtunga sheria.

Katika muradi wa sheria na taratibu za kiutawala (admimistrative law point of view) sheria zinajulikana kuwa zitajitafsiri zenyewe na msingi unaokubalika ni kuwa kila ambapo tenure inapomalizika na kuwepo kwa kanuni ya kuongezewa tena kipindi cha pili neno "Shall" halina maana kama ilivyo katika Sheria ya Kufasiri Sheria (The Interpretation of Laws Act), hapa maana huwa ya kimazingira zaidi (contextual meaning) na haiwi LAZIMA bali INAWEZA.

Na moja kwa moja ni kuwa kuongezewa kipindi cha pili Mtendaji yeyote mwenye vipindi viwili na hata Rais mwenyewe sio "automatic" lazima kuwe "subject to good performance."

Na anayeamua akuongezee tenure ya pili, hiyo sheria haijambana, ni yule yule mwenye mamlaka ya kuteua na kukutengua.

Rais anapewa mamlaka hayo kwa CAG na watendaji wengine Serikali aliowateua kwa sheria yoyote kwa mamlaka aliuonayo katika Ibara ya 36. Tena 36(3) ndio inampa mamlaka ya jumla zaidi ya kudeal na tatizo lolote kwa nia ya kuweka utulivu katika utumishi kwa kuweza kumtengua mtu yeyote aliyemteua.

View attachment 1253920

Ukifasiri neno "shall" katika Sheria ya Ukaguzi ili kumtetea CAG Assad kwamba ilikuwa lazima aendelee miaka mitano ya pili ni kuleta dhahama kubwa nchini inayoweza kushawishi hata Uchaguzi Mkuu wa Mwakani usifanyike. Najua utashangaa!!!

Ndio, tafsiri ya Zitto na wenzake ni ya hatari zaidi kwa nchi kwani ukisoma Ibara ya 40 ya Katiba inapozungumzia Rais aliyeko madarakani kwa kipindi cha miaka mitano ya mwanzo kuwa anaweza kuchaguliwa tena kwa miaka mingine mitano ya pili na ya mwisho neno lililotumika ni "shall."
View attachment 1253921

Kama tafsiri SISISI na "#shallow" ya ACT ni ya kufuatwa basi kwa muktadha wa neno "Shall" pia katika Ibara ya 40 ya Katiba, Rais Magufuli naye mwakani hakuna haja ya kupimwa utendaji wake kwa kurudi katika sanduku la kura, aendelee tu, kusiwe na uchaguzi, aapishwe moja kwa moja kuendelea na Urais maana "shall" ina maana ya LAZIMA.

Lakini hapana, muradi wa "shall" katika masuala ya utawala sio kama inavyotumika katika sheria za kawaida, hapa bado dhana ya mhusika kuwa "subjected to good performance" kwa kutazamwa utendaji wake kama unaridhisha mamlaka ya uteuzi (kwa kesi ya CAG) na kwa kurudi kuomba kura tena kwa wananchi (kwa kesi ya Rais) ndio utaratibu kabla ya kulamba awamu ya pili.

Kitaalamu ni kuwa CAG aliyemaliza muda wake hakuonewa na kama ni kuonewa au aliyemteua ana nia mbaya angeweza kuondolewa hata kabla hajamaliza miaka hii mitano.

Ibara ya 144(2) inampa madaraka Rais kumuondoa CAG kwa sababu ya utendaji mbovu, maradhi au sababu nyingine yoyote.

View attachment 1253922

Nimeona wengi wanasema Rais hawezi kufanya hivyo mpaka aunde Tume, si kweli. Watanzania tuachane na kasumba ya kutosoma kwa umakini.

Tuzisome sheria vyema na tunaposhindwa kuelewa tuwatafute wataalamu sio wanasiasa.

Katika Ibara ya 144(3) Rais ataunda Tume (If) kwa maana ya "kama" ataona kuchunguza sababu hizo za kumuondoa CAG kunafaa kuchunguzwa. Maana yake akijiridhisha hana haja ya kuunds Tume.

View attachment 1253923

Kisheria na Kikatiba, namsifu sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk Magufuli na wataalamu wake wa sheria, hakika ni wabobezi, wanazisoma sheria zetu kwa utulivu na kuzifasiri kwa mujibu wa viapo vyao.

Naamini Rais Mhe. Dk Magufuli hakuwa na jambo baya la kutaka kumfukuza CAG isipokuwa "subject to good performance" anahitaji kasi zaidi katika eneo hilo na utulivu zaidi na kuaminika zaidi kwa kiongozi wa muhimili huo ambako Assad alishafeli kwa kufikia hatua ya kugombana na mhimili wa Bunge.

Kwa uchambuzi huu kudai Rais kavunja Sheria ni uchochezi mkubwa usiofaa kufumbiwa macho.

/chanzo Wakili wa Kujitegemea fb
Assad ana kile kiburi cha kisomi. Na JPM hakutaka kuwa upande tofauti na Spika.
 
Naona wanasheria bado hamkubaliani kwa kitu mlichosomea!
Ndio maana mnajiita wanasheria wasomi.
Lissu anasemaje makamanda hii ishu?
Sisi tumefunga mjadala. Shall be eligible for renewal IS not the same as SHALL BE RENEWED..
Hutaki acha...
 
Tunatumia nguvu kubwa katika kuyaongelea mambo ambayo kiuhalisia tulipaswa kuelimishwa na wenye fani zao.

We argue about issues which we partially know of.
Wenye fani yao hawana jibu sahihi. Fani moja wana majibu yanayotofautiana kuhusu ishu moja.
 
CAG ameongea kutafuta huruma ya Wananchi kama kawaida yake ili aonekane ameonewa wakati mkataba wa kazi ni miaka mitano

Kila mtanzania mwenye sifa alistahili kuwa CAG,professor Asad aache uswahili

Tumheshimu Rais wa Nchi anafanya kazi kubwa

CAG aliyeondolewa ndio alikuwa anaficha uchafu wa the Trio kule NSSF. One of the trio Zito Kabwe alikuwa anabweka sana na mwisho wake ndio umepamba moto sasa.
 
Back
Top Bottom