Suala la Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Vipengele kadhaa vya Kisheria

Suala la Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Vipengele kadhaa vya Kisheria

Hawa jamaa wanajiita wasomi lakini nashangaa anatafsiri shall kisheria huku akinyamaza kuhusu eligibility.

Kitu wanachosahau hata kwenye urais maneno hayo hayo yametumika lakini iko siku rais atatawala miaka mitano watu watasema katiba imevunjwa.

Shall ina maana hiyo hiyo popote pale.

Haibadiliki maana itumiwapo kwenye fani tofauti.

Hata ikitumiwa kwenye neurology, maana yake ni ile ile tu. Ni modal verb inayoelezea ulazima.

Sijawahi ona popote pale ambapo shall ina maana tofauti.
 
Mbaya zaidi, hawatoi ufafanuzi wa matumizi ya neno SHALL kwa mujibu wa sheria zetu! Nimelazimika kuanzisha uzi huu ili kuondoa mapungufu yote hayo.
Nina imani kabla ya kuandaa uzi huu, ulipitia uzi huu kwanza.
Hasa kipengele hiki
Rais anapewa mamlaka hayo kwa CAG na watendaji wengine Serikali aliowateua kwa sheria yoyote kwa mamlaka aliuonayo katika Ibara ya 36. Tena 36(3) ndio inampa mamlaka ya jumla zaidi ya kudeal na tatizo lolote kwa nia ya kuweka utulivu katika utumishi kwa kuweza kumtengua mtu yeyote aliyemteua.

Ukifasiri neno "shall" katika Sheria ya Ukaguzi ili kumtetea CAG Assad kwamba ilikuwa lazima aendelee miaka mitano ya pili ni kuleta dhahama kubwa nchini inayoweza kushawishi hata Uchaguzi Mkuu wa Mwakani usifanyike. Najua utashangaa!!!

Ndio, tafsiri ya Zitto na wenzake ni ya hatari zaidi kwa nchi kwani ukisoma Ibara ya 40 ya Katiba inapozungumzia Rais aliyeko madarakani kwa kipindi cha miaka mitano ya mwanzo kuwa anaweza kuchaguliwa tena kwa miaka mingine mitano ya pili na ya mwisho neno lililotumika ni "shall."

Kama tafsiri SISISI na "shallow" ya ACT ni ya kufuatwa basi kwa muktadha wa neno "Shall" pia katika Ibara ya 40 ya Katiba, Rais Magufuli naye mwakani hakuna haja ya kupimwa utendaji wake kwa kurudi katika sanduku la kura, aendelee tu, kusiwe na uchaguzi, aapishwe moja kwa moja kuendelea na Urais maana "shall" ina maana ya LAZIMA.

Lakini hapana, muradi wa "shall" katika masuala ya utawala sio kama inavyotumika katika sheria za kawaida, hapa bado dhana ya mhusika kuwa "subjected to good performance" kwa kutazamwa utendaji wake kama unaridhisha mamlaka ya uteuzi (kwa kesi ya CAG) na kwa kurudi kuomba kura tena kwa wananchi (kwa kesi ya Rais) ndio utaratibu kabla ya kulamba awamu ya pili.

Maoni yangu ya kitaalamu ni kuwa CAG anayemaliza muda wake kesho hakuonewa na kama ni kuonewa au aliyemteua ana nia mbaya angeweza kuondolewa hata kabla hajamaliza miaka hii mitano.

Ibara ya 144(2) inampa madaraka Rais kumuondoa CAG kwa sababu ya utendaji mbovu, maradhi au sababu nyingine yoyote.

Nimeona wengi wanasema Rais hawezi kufanya hivyo mpaka aunde Tume, si kweli. Watanzania tuachane na kasumba ya kutosoma kwa umakini.

Tuzisome sheria vyema na tunaposhindwa kuelewa tuwatafute wataalamu sio wanasiasa.
 
Kimsingi sheria ilipotamka

The Controller and Auditor-General shall hold office for the fixed term of five years and shall be eligible for renewal for one term only.

Lengo la kifungu hiki cha kililenga kumzuia Rais kumteua CAG kwa zaidi ya vipindi viwili.

Kifungu hiki hakikutaka kumpa Rais uwezo wa kuamua kumpa CAG kipindi kimoja cha miaka 5 au vipindi viwili, kama CAG hajafikisha umri wa ukomo.
 
Neno "shall" lina mandatory meaning yaani lazima au "permissive meaning" yaani ruhusa.

Mfano, sheria ikisema "appeal shall be within 60 days unless the Court directs otherwise". Hapa maana yake ni permissive meaning kwamba rufaa ikatwe ndani ya siku 60 ila mahakama ikielekeza vinginevyo basi itakuwa vinginevyo.

Kuhusu CAG, sheria imesema " CAG shall be eligible to removal after 5 years maana yake ni kwamba baada ya 5 years mamlaka teuzi inaweza kutengua au isitengue uteuzi wa CAG baada 5 years. Na hapa neno "shall" linakuwa na maana sawa na neno "may".

Ingekuwa tofauti kama ingesema "shall be removed after 5 years". Yaani " mandatory " lazima.

Rejea case ya DPP v Freeam A. Mbowe.

Kwenye hii case sheria ilisema " appeal shall be accompanied with written court proceedings unless the court directs otherwise ". Hapa mahakama ya Rufaa ilisema kuwa neno " shall" lilitumika as "permissive" but not mandatory.
 
Tatizo Raisi amefanya haya kwa Mihemko, Kudanganywa na Kujidanganga, Kushauriwa vibaya na Kujishauri vibaya na On top of that Kwa CHUKI binafsi.

Raisi amevunja Katiba ALIYOAPA kuilinda huku akimtaja MUNGU anayedai kumtanguliza mbele'
Jiwe hakumtaka toka mwanzo katuma watu kupika zengwe, job mpambe tu
 
Shall ina maana hiyo hiyo popote pale.

Haibadiliki maana itumiwapo kwenye fani tofauti.

Hata ikitumiwa kwenye neurology, maana yake ni ile ile tu. Ni modal verb inayoelezea ulazima.

Sijawahi ona popote pale ambapo shall ina maana tofauti.


Na nimehoji endapo kisheria shall inamaanisha must, si wangeweka hiyo must tujue moja? Sasa wasomi wanatuandikia shall na kutuachia kazi ya kuitafsiri tena shall kisheria.

Iko siku utaambiwa ukiwa US shall inamaanisha hivi, ukiwa Lagos inamaanisha kitu kingine na ukiwa Mtwara kitu kingine
 
Tumtakie CAG Mstaafu, Prof. Mussa Assad kustaafu kwema na amestaafu kwa heshima na kwa mujibu wa sheria na sio kwa hoja zozote za vitatange na vibirifitina, jina lake litaandikwa kwenye kile kitabu cha mashujaa wa kweli wa taifa wetu kwasababu ameacha Legacy.

Karibu CAG Mpya, Charles Kicheere, tunakutakia kazi njema.
Paskali
Kwahiyo mkuu Mwl. Wako Prof.Shivji kachemka katika comments yake aliyosema procedure hazikufuatwa.
 
asa mtu kamaliza muda wake na kale alikuwa anakafanya kama ka mhimili mpaka anakuwa mbishi muacheni akacheze mdako huko na wenzie
 
Let me ask you this...

Shall be eligible for renewal and shall be reappointed for another 5 year term.

Which one of those expresses a necessity and which one expresses a possibility?

I feel like I’m back to being an English teacher again [emoji1787]
Hizo habari za shall be eligible kwanza zinazungumzia term limits, kwamba asiwe renewed zaidi ya mara moja, mwisho wa CAG kutumikia ni terms mbili.

Kwa hiyo hicho kifungu hakihusiani na Rais ku renew au kuto renew mkataba sasa. Hicho kifungu kingehusika 2024 kama Assad angekuwa CAG bado, rais asingeweza kum renew kuwa CAG.

Magufuli inaonekana kavunja katiba, lakini si kwenye kifungu hicho.

Kuna kofungu kingine kinasema CAG kuondolewa, hata kama ni baada ya miaka mitano, ni lazima aundiwe imoeachment tribunal.

Inaonekana kazi ya CAG kama hujawa imoeached na tribunal unafanya terms mbili, na iki kuishia term moja inabidi upatikane na makosa na imoeachment tribunal.

Profesa Shivji pia ali tweet akiomba radhi na kusahihisa maneno yake ya awali, akasema katiba imeweka process ya kumuindoa CAG.

Inaonekana Magufuli kajiamulia tu bila kufuata impeachment tribunal.
 
Kimsingi sheria ilipotamka

The Controller and Auditor-General shall hold office for the fixed term of five years and shall be eligible for renewal for one term only.

Lengo la kifungu hiki cha kililenga kumzuia Rais kumteua CAG kwa zaidi ya vipindi viwili.

Kifungu hiki hakikutaka kumpa Rais uwezo wa kuamua kumpa CAG kipindi kimoja cha miaka 5 au vipindi viwili, kama CAG hajafikisha umri wa ukomo.
Kuna vifungu ambavyi Magufuli kavunja, lakini si hiki.

Hiki kifungu ni irrelevant kwa mjadala wa sasa, kwa sababu ni kifungu cha term limits ambacho umuhimu wake ungeonekana 2024 kama Assad angeendelea kuwa CAG.

Kifungu hiki kingemzuia rais ku extend tenure ya Assad kuwa CAG beyond 2024.

Kwa sasa kifungu hiki ninoff topic.

Magufuli kavunja katiba, lakini kifungu hiki kwa sasa hakihusiki.

Magufuli kavunja katiba kwa sababu kumtoa CAG, hata baada ya miaka mitano, inabidi kufanya impeachment tribunal.

Magufuli hakufanya, kamtoa kiholela tu.
 
Hizo habari za shall be eligible kwanza zinazungumzia term limits, kwamba asiwe renewed zaidi ya mara moja, mwisho wa CAG kutumikia ni terms mbili.

Kwa hiyo hicho kifungu hakihusiani na Rais ku renew au kuto renew mkataba sasa. Hicho kifungu kingehusika 2024 kama Assad angekuwa CAG bado, rais asingeweza kum renew kuwa CAG.

Magufuli inaonekana kavunja katiba, lakini si kwenye kifungu hicho.

Kuna kofungu kingine kinasema CAG kuondolewa, hata kama ni baada ya miaka mitano, ni lazima aundiwe imoeachment tribunal.

Inaonekana kazi ya CAG kama hujawa imoeached na tribunal unafanya terms mbili, na iki kuishia term moja inabidi upatikane na makosa na imoeachment tribunal.

Profesa Shivji pia ali tweet akiomba radhi na kusahihisa maneno yake ya awali, akasema katiba imeweka process ya kumuindoa CAG.

Inaonekana Magufuli kajiamulia tu bila kufuata impeachment tribunal.

Kwa hiyo sheria inalazimu CAG afanye kazi yake kwa miaka 10 na si miaka mitano mitano?

Well, naona maneno ni mengi mno kwenye hili suala.

Kama Shivji alikosea awali, hata sasa anaweza akawa kakosea pia.

Recourse ni kwenda mahakamani tu.

Lakini hata huko watu wataenda wakiwa tayari mitazamo yao iliyo prejudiced.

Kama masuala mengine yaliyotangulia, hili nalo litaishia kuwa litigated mtandaoni tu.

Bottom line, shall be eligible for renewal is not the same as shall be renewed.
 
asa mtu kamaliza muda wake na kale alikuwa anakafanya kama ka mhimili mpaka anakuwa mbishi muacheni akacheze mdako huko na wenzie
Kamaliza wapi mda wake? Mmeogopa akifika ATCL mtaumbuka kama mlivyoumbuka kwa zile tilion 1.5 mmeamua kumkimbiza haraka kabla hajawaumbua mkatapa Aibu , mdako upi akacheze? Kwa uadilifu wake hatakosa kazi ya kufanya na maisha kuendelea kama kawaida
 
Mkuu pale inaposema and shall be eligible for renewal of on term only ina maana gani hasa hilo neno shall
Anaweza kuteuliwa kwa term moja nyingine. Usiangalie neno shall pekee, angalia pia neno eligible. Eligible imepunguza nguvu ya neno shall kuwa lazima
 
Pongezi kwa prof. Assad kwa kazi iliyonyooka,hukuwahi kutetereka wala kutetemeka ukiwa ofisini kama CAG na wakati wote wa kutekeleza wajibu wako.
CAG wa mfano ambae taifa limewahi kumpata,nakutakia mapumziko mema.
 
Kuondolewa kwa CAG Prof. Musa Assad ni jambo ambalo kama Taifa litahitaji mjadala mpana ili kuwa na uhakika kuwa katiba na sheria vimefuatwa au vimekiukwa.

Wanaosema kuwa CAG ameondolewa kwa kufuata katiba na wale wanaosema ameondolewa kwa kukiuka katiba, wote wanaegemea kwenye Katiba kifungu 144 (1), kinachosema:

Controller and Auditor-General of the United Republic shall be obliged to vacate office upon attainaing the age of sixty or any other age which shall be prescribed by a law enacted by Parliament.

Na Public Audit Act 6 (2) (a) inayosema

Unless the question of removal becomes the subject of investigation in terms of Article 144(3) of the Constitution, the Controller and Auditor-General shall vacate office upon attaining the age of sixty five years

Na Public Audit Act 6(1) kinachosema

The Controller and Auditor-General shall hold office for the fixed term of five years and shall be eligible for renewal for one term only.

Kifungu cha kwanza na cha pili, kimsingi havibishaniwi na pande zote mbili. Kifungu kinachobishaniwa ni hicho cha tatu.

Katika kutafsiri vifungu hivi kisheria ni lazima kuvitazama katika kusudio la sheria. Makusudia ya sheria hizi ni:

1) Kupunguza uhuru wa Rais wa kuteua na kumfukuza CAG

2) kumlazimisha Rais aina ya mtu wa kumteua

4) kumzuia CAG kukaa kwa muda mrefu zaidi ya kusudio la sheria

5) kumzuia Rais kumteua au kumkalisha CAG kwenye nafasi hiyo akiwa na umri zaidi ya miaka 65.

Kwenye kifungu cha katiba ibara ya 144(1), katiba imetoa nafasi kwa sheria nyingine kubadilisha umri wa mwisho wa CAG kukaa kwenye nafasi yake kutoka ule wa miaka 60 uliotamkwa.

Sheria wakati wote huweka lengo kuu na kisha huweka mipaka ya hilo lengo kuu. Kwenye katiba 144 (1) lengo kuu ni CAG akishateuliwa ashike nafasi hiyo, Rais asiwe na uwezo wa kumwondoa.

Na pia kwenye Public Audut Act 6(1) sheria imelenga kutokuwa na CAG ambaye anaweza kukaa kwa muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa katika lengo kuu. Hivyo sheria ikaweka ukomo. Na ukomo huu ulitazama zaidi pale ambapo CAG akawa ameteuliwa na umri mdogo, na hivyo kukalia kiti cha CAG kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10. Hivyo sheria imezuia uwezekano wa kuwa na CAG anayekalia nafasi hiyo kwa zaidinya miaka 10 hata kama umri wake bado unamruhusu kwa kadiri ya Katiba

Katika vifungu vyote hivyo katiba na sheria, vinamtaja CAG mwenyewe na siyo aliyemteua. Ibara ya 144 (1) ya katiba inamtaka CAG ..... shall vacate, na siyo kuondolewa. Na hata kile kifungu cha kuongeza fixed one term, nacho kinamtaja CAG mwenyewe kuwa ... shall be elligible, na siyo aliyemteua.

CAG akishateuliwa, akifikisha umri wa miaka 65, ni yeye ndiye anayestakiwa kumjulisha Mh. Rais kuwa anaondoka kwa kuwa amefikisha umri wa mwisho kisheria.

Na hata pale anapohudumu term ya pili akamaliza au wakati akihudumu akafikisha umri wa mwisho, ni yeye anayetakiwa kumjulisha mh. Rais kuwa amemaliza kipindi chake kwa mujibu wa sheria na katiba.

Kilichofanyika siyo sahihi. CAG anaweza asifanye kitu, na sisi pia tunaweza tusifanye kitu, siyo kwa sababu Rais yupo sahihi kwa mujibu wa Katiba na sheria bali kwa sababu tumeamua kukubaliana na uvunjifu wa katiba kama ilivyowahi kutokea kwa mambo mengine.

Lakini tusisahau kuwa uharibifu huanza taratibu. Mataifa mengi yalianza hivi hivi wakapuuza. Mambo yalipofika kilele, hawakuweza kurekebisha zaidi ya kushuhudia uharibifu na kusambaratika kwa mataifa yote.

Nchi ni lazima iendeshwe kwa misingi ya katiba, hata kama kutakuwa na kiongozi mzuri namna gani, ni lazima afuate katiba.
 
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria

Kama wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata hati chafu ya ubadhirifu wa pesa
 
Back
Top Bottom