Suala la Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Vipengele kadhaa vya Kisheria

Suala la Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Vipengele kadhaa vya Kisheria

Kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi ya Taifa Na. 11 ya Mwaka 2008 kifungu cha 6(1) "basic tenure" ya CAG ni miaka mitano na sheria inasema anaweza (Shall) kutumikia vipindi viwili vya miaka mingine mitano.

CAG anaulinzi mkubwa kisheria na moja ya ulinzi wake ni kuwa akiwa katikati ya tenure yake hawezi kuondolewa hivi hivi bila masharti kadhaa kufuatwa, lazima utumie masharti ya Ibara ya 144(3) ya Katiba au yeye mwenyewe achukue hatua under subsestion 2 ya hiyo Sheria ya Ukaguzi niliyoitaja hapo juu. Lakini kwa ujumla anaweza kuondolewa, si ngumu. Nitaeleza.

View attachment 1253918

Matumizi ya neno "Shall" lililotumika katika Sheria ya Ukaguzi kwenye kifungu cha 6 .

Kwa heshima na taadhima, Sheria hapo haijakusudia ulazima na ndio maana sheria haifasiriwi kwa matakwa ya mtu bali sheria zenyewe zinavyokusudia kufasiriwa katika muktadha wa jambo husika na lengo la mtunga sheria.

Katika muradi wa sheria na taratibu za kiutawala (admimistrative law point of view) sheria zinajulikana kuwa zitajitafsiri zenyewe na msingi unaokubalika ni kuwa kila ambapo tenure inapomalizika na kuwepo kwa kanuni ya kuongezewa tena kipindi cha pili neno "Shall" halina maana kama ilivyo katika Sheria ya Kufasiri Sheria (The Interpretation of Laws Act), hapa maana huwa ya kimazingira zaidi (contextual meaning) na haiwi LAZIMA bali INAWEZA.

Na moja kwa moja ni kuwa kuongezewa kipindi cha pili Mtendaji yeyote mwenye vipindi viwili na hata Rais mwenyewe sio "automatic" lazima kuwe "subject to good performance."

Na anayeamua akuongezee tenure ya pili, hiyo sheria haijambana, ni yule yule mwenye mamlaka ya kuteua na kukutengua.

Rais anapewa mamlaka hayo kwa CAG na watendaji wengine Serikali aliowateua kwa sheria yoyote kwa mamlaka aliuonayo katika Ibara ya 36. Tena 36(3) ndio inampa mamlaka ya jumla zaidi ya kudeal na tatizo lolote kwa nia ya kuweka utulivu katika utumishi kwa kuweza kumtengua mtu yeyote aliyemteua.

View attachment 1253920

Ukifasiri neno "shall" katika Sheria ya Ukaguzi ili kumtetea CAG Assad kwamba ilikuwa lazima aendelee miaka mitano ya pili ni kuleta dhahama kubwa nchini inayoweza kushawishi hata Uchaguzi Mkuu wa Mwakani usifanyike. Najua utashangaa!!!

Ndio, tafsiri ya Zitto na wenzake ni ya hatari zaidi kwa nchi kwani ukisoma Ibara ya 40 ya Katiba inapozungumzia Rais aliyeko madarakani kwa kipindi cha miaka mitano ya mwanzo kuwa anaweza kuchaguliwa tena kwa miaka mingine mitano ya pili na ya mwisho neno lililotumika ni "shall."
View attachment 1253921

Kama tafsiri SISISI na "#shallow" ya ACT ni ya kufuatwa basi kwa muktadha wa neno "Shall" pia katika Ibara ya 40 ya Katiba, Rais Magufuli naye mwakani hakuna haja ya kupimwa utendaji wake kwa kurudi katika sanduku la kura, aendelee tu, kusiwe na uchaguzi, aapishwe moja kwa moja kuendelea na Urais maana "shall" ina maana ya LAZIMA.

Lakini hapana, muradi wa "shall" katika masuala ya utawala sio kama inavyotumika katika sheria za kawaida, hapa bado dhana ya mhusika kuwa "subjected to good performance" kwa kutazamwa utendaji wake kama unaridhisha mamlaka ya uteuzi (kwa kesi ya CAG) na kwa kurudi kuomba kura tena kwa wananchi (kwa kesi ya Rais) ndio utaratibu kabla ya kulamba awamu ya pili.

Kitaalamu ni kuwa CAG aliyemaliza muda wake hakuonewa na kama ni kuonewa au aliyemteua ana nia mbaya angeweza kuondolewa hata kabla hajamaliza miaka hii mitano.

Ibara ya 144(2) inampa madaraka Rais kumuondoa CAG kwa sababu ya utendaji mbovu, maradhi au sababu nyingine yoyote.

View attachment 1253922

Nimeona wengi wanasema Rais hawezi kufanya hivyo mpaka aunde Tume, si kweli. Watanzania tuachane na kasumba ya kutosoma kwa umakini.

Tuzisome sheria vyema na tunaposhindwa kuelewa tuwatafute wataalamu sio wanasiasa.

Katika Ibara ya 144(3) Rais ataunda Tume (If) kwa maana ya "kama" ataona kuchunguza sababu hizo za kumuondoa CAG kunafaa kuchunguzwa. Maana yake akijiridhisha hana haja ya kuunds Tume.

View attachment 1253923

Kisheria na Kikatiba, namsifu sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk Magufuli na wataalamu wake wa sheria, hakika ni wabobezi, wanazisoma sheria zetu kwa utulivu na kuzifasiri kwa mujibu wa viapo vyao.

Naamini Rais Mhe. Dk Magufuli hakuwa na jambo baya la kutaka kumfukuza CAG isipokuwa "subject to good performance" anahitaji kasi zaidi katika eneo hilo na utulivu zaidi na kuaminika zaidi kwa kiongozi wa muhimili huo ambako Assad alishafeli kwa kufikia hatua ya kugombana na mhimili wa Bunge.

Kwa uchambuzi huu kudai Rais kavunja Sheria ni uchochezi mkubwa usiofaa kufumbiwa macho.

/chanzo Wakili wa Kujitegemea fb
Mimi sio mwanasheriari lakini hiyo ibara ya 40(1) aliyoitumia huyo 'wakili ' kakosea nasema Mimi 'mpima ardhi ' kwamba maneno "shall be eligible for reelection for that office " haimaanishi kwamba rais atakuwa na haki ya kuwa rais Kwa kipindi kingine bila ya kupigiwa kura na wananchi ndiyo maana ya neno "reelection " yaani utafanyika uchaguzi mwingine kumchagua rais na siyo automatic anaendelea kuwa rais ni lazima kuwe na uchaguzi Mkuu!
Neno "shall " maana yaken ni lazima "mandatory " ndiyo maana katiba ikasema kuwa "shall be eligible for reelection "
 
Unakomaa na kuteseka kupata reference

Tatizo siku hizi kuna watu mnajua mno.....na mnaona wengine wajinga

CAG MPYA anajulikana

Pia unatumia wrong version
Ccm in secrecy
Ndio umeandika nini sasa
Chambua vifungu sio blah blah
 
Angalia mwaka public audit act iliyochomeka utata wa miaka 5
Hakuna mtu aliyeleta balaa kwenye nchi hii kama jk
Yule mk.were ovyo kabisa
 
Naona wanasheria bado hamkubaliani kwa kitu mlichosomea!
Ndio maana mnajiita wanasheria wasomi.
Lissu anasemaje makamanda hii ishu?
Sisi tumefunga mjadala. Shall be eligible for renewal IS not the same as SHALL BE RENEWED..
Hutaki acha...

Wengine wanadai eti kuwa ‘shall’ katika legal parlance ina maana tofauti.

Si kweli hata kidogo.

Maana yake ni ile ile.

‘Shall’ doesn’t become a different part of speech with a totally different meaning just because it’s used in legalese.

Muhimu ni muktadha ambao neno limetumiwa.

Shall be eligible for renewal na shall be renewed ni sentensi mbili zenye maana tofauti kabisa licha ya kwamba zote zina neno ‘shall’.

Muktadha muktadha muktadha.
 
Tuseme uko sawa
Turudi kwenye katiba inataka astaafu na miaka 60 na hakuna sehemu katiba imetamka bunge litunge kipengele cha miaka mitano...bunge limepewa fursa ya miaka tu ambapo waliongeza hadi miaka 65
Hicho kipengele cha miaka mitano mitano ni batili ab initio
 
Sio ‘tuseme’ niko sawa.

Ni kwamba, nipo sawa.

Shall be eligible for renewal si sawa na shall be renewed.

End of story.
 
Tumtakie CAG Mstaafu, Prof. Mussa Assad kustaafu kwema na amestaafu kwa heshima na kwa mujibu wa sheria na sio kwa hoja zozote za vitatange na vibirifitina, jina lake litaandikwa kwenye kile kitabu cha mashujaa wa kweli wa taifa wetu kwasababu ameacha Legacy.

Karibu CAG Mpya, Charles Kicheere, tunakutakia kazi njema.
Paskali
Kaka Paskali,
Mjibu mtoa mada kwa hoja... ulichoandika hapa ndo utatange wenyewe...
Mwenzio kaanisha na vimeeleweka... wewe umepiga blah blah na utatange tu

Ngali K
 
Kwa hiyo sheria inalazimu CAG afanye kazi yake kwa miaka 10 na si miaka mitano mitano?

Well, naona maneno ni mengi mno kwenye hili suala.

Kama Shivji alikosea awali, hata sasa anaweza akawa kakosea pia.

Recourse ni kwenda mahakamani tu.

Lakini hata huko watu wataenda wakiwa tayari mitazamo yao iliyo prejudiced.

Kama masuala mengine yaliyotangulia, hili nalo litaishia kuwa litigated mtandaoni tu.

Bottom line, shall be eligible for renewal is not the same as shall be renewed.
Vifungu vya katiba vinavyosema kwamba CAG kuondolewa, hata kama ni baada ya miaka mitano tu, ni lazima awe mgonjwa, katimiza miaka 65 au kafanyiwa impeachment tribunal viko clear kabisa.

Magufuli hakutakiwa kumuondoa CAG bila kufuata katiba. Magufuli amevunja katiba kwa mara nyingine tena.
 
There you are tuna wapinzani vilaza sijapata kuona.
Ila kuna vifungu vingine vya katiba vinavyomtaka Magufuli kuunda impeachment tribunal ili kumuondoa CAG ambaye hajafikisha umri wa kuondoka na wala hana maradhi ya kumfanya asiweze kazi yake.

Hivyo ndivyo vifungu vya katiba alivyovunja Magufuli.
 
Nafahamu kwamba watu wengi wameanzisha threads wakijaribu kuelezea suala la CAG Kisheria! Hata hivyo, wengi wao kama sio wote walichofanya ni kurundika vifungu vya kisheria bila kutoa ufafanuzi!

Mbaya zaidi, hawatoi ufafanuzi wa matumizi ya neno SHALL kwa mujibu wa sheria zetu! Nimelazimika kuanzisha uzi huu ili kuondoa mapungufu yote hayo.

Tuendelee.

Bila kujaza vifungu vingi, Katiba yetu Ibara ya 144 (1) inasema wazi kwamba:-
Kwamba, CAG ATALAZIMIKA kuachia ofisi akifikisha miaka 60 au umri mwingine wowote utakaotajwa na sheria zilizotengenezwa na Bunge!

SWALI 1: Je, Profesa Mussa Assad amefikisha miaka 60?! Jibu HAPANA kwa sababu kumbukumbu zinaonesha amezaliwa Oktoba 06, 1961... kwa maana nyingine, atafikisha miaka 60 Oktoba 5, 2021.

SWALI 2: Je, Bunge limetaja huo UMRI MWINGINE WOWOTE?!

Jibu linapatikana kwenye Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma, yaani Public Audit Act ya mwaka 2008, Ibara ya 6(2)(a) inayosema:-

Kumbe, Bunge likatunga sheria kwamba badala ya miaka 60, hatimae CAG ATALAZIMIKA kuachia ofisi akifikisha miaka 65. Tumeona Prof Assad ndo kwanza ana miaka 58.

SWALI 3: Nini hutokea CAG akimaliza miaka 5 ya kwanza?!

Hapa tena jibu linapatikana kutoka Public Audit Act 2008 Ibara ya 6 (1) inayosema:-Hapo kwenye neno SHALL ndipo panapozua mgogoro!!

Watetezi wa uamuzi wa Rais wanasema neno SHALL sio shuruti! Kwa bahati mbaya sana, tafsiri yao wanaitoa kichwani na sio kwa mujibu wa sheria zetu!

Kwa mujibu wa sheria zetu, na kwa kuangalia Interpretation of Laws Act Ibara ya 53 (1&2) inasema kwamba:-
Kumbe, kwa mujibu wa sheria zetu, pasipo na SHURUTI hutumika neno MAY lakini linapotumika neno SHALL, hiyo ni SHURUTI!

Kwa maana nyingine, Public Audit Act inaposema "...and shall be eligible for renewal for one term only. Hapo suala la renewal ni SHURUTI kama ilivyosema Interpretation of Laws Act 53 (2).

Itakuwa sio SHURUTI either kama ameshafikisha miaka 65, au kama ambavyo 2008 Public Audit Act Ibara ya 6(2)(a) inavyosema kwamba:-Kwa maana nyingine, kwavile Prof Assad hajafikisha miaka 65, hapo tafsiri yake ni kwamba AMETUMBULIWA na sio kwamba muda wake umeisha!!

Na CAG atatumbuliwa "...Unless the question of removal becomes the subject of investigation in terms of Article 144(3) of the Constitution."

Hiyo Ibara ya 144(3) ya Katiba yetu inasemaje? Jibu ni hili:-If the President considers that the question of the removal of the Controller and Auditor-General from office under the provisions of this Article needs to be investigated, then the procedure shall be as follows:Kama tulivyoona hapo juu, CAG atalazimika kuachia ofisi endapo atakuwa amefikisha miaka 65, kinyume chake anaweza KUTUMBULIWA kabla ya huo umri ikiwa ametenda jambo linalohitaji investigation.

Hivyo basi, ni ama Rais atengue uamuzi wake wa awali wa kuteua CAG mwingine, au tuone akiunda Tume ya Kijaji ya Kumchunguza CAG kwa kosa analojua yeye na timu yake!!

CAG akiongezewa miaka mingine 5, ataimaliza akiwa na umri wa miaka 63... umri halali kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma ya mwaka 2008!!

Zaidi soma:

[/QUOTE]
Mtaalamu wa sheria hebu tusaidia kifungu cha 40 (i) cha Katiba inasema hivi:
40.-(1) Subject to the other provisions of this Article, any person who holds office as President shall be eligible for re-election to that office. (2) No person shall be elected more than twice to hold the office of President.

Hapo "SHALL" inamaana kama ulivyoeleza hapo juu??!!
 
Wengine wanadai eti kuwa ‘shall’ katika legal parlance ina maana tofauti.

Si kweli hata kidogo.

Maana yake ni ile ile.

‘Shall’ doesn’t become a different part of speech with a totally different meaning just because it’s used in legalese.

Muhimu ni muktadha ambao neno limetumiwa.

Shall be eligible for renewal na shall be renewed ni sentensi mbili zenye maana tofauti kabisa licha ya kwamba zote zina neno ‘shall’.

Muktadha muktadha muktadha.

Umesoma subsection 3 hii ya sheria iliyoundwa kuelezea utaratibu wa kurenew mkataba wa CAG? :Soma hii hapa Chini:

Img-1572853035577.jpg

Then kutokana na Profesa Shivji kusoma kipengele hicho naye akasema yafuatayo:

IMG-20191104-WA0057.jpg

kutokana na kifungu hicho subsection 3

Ni dhahiri kwa mujibu wa sheria, Sheria inataka kuwa CAG aliyemaliza muhula wake wa kwanza LAZIMA aongezewe miaka mingine mitano isipokuwa tu kama Rais hataki kuendelea naye basi yapaswa kufuata mchakato wa kumtoa kama ilivyoelekezwa na ibara ya 144 ya katiba.

JPM Kavunja sheria kwenye hili suala, Ameteua CAG mpya kinyume cha sheria
 
Vifungu vya katiba vinavyosema kwamba CAG kuondolewa, hata kama ni baada ya miaka mitano tu, ni lazima awe mgonjwa, katimiza miaka 65 au kafanyiwa impeachment tribunal viko clear kabisa.

Magufuli hakutakiwa kumuondoa CAG bila kufuata katiba. Magufuli amevunja katiba kwa mara nyingine tena.

Well, kama ni hivyo basi Assad aende mahakamani.

Manake kama ni dhahiri namna hiyo kama ulivyowasilisha, the whole thing should be a slam dunk open-and-shut case.

Pia nimeona kuna tatizo kubwa sana la uelewa wa lugha ya Kiingereza.

Suala la ‘shall be eligible for renewal’ ni suala jepesi sana lisilohitaji hata mabishano.

Ila sasa sishangai kwa nini hata baadhi ya watu walikuwa wana cite hicho kipengele kuwa ndiyo kimevunjwa!
 
Kuna vifungu vya katiba vinavyomtaka Magufuli kuanzisha impeachment tribunal kabla ya kumuondoa CAG.

Hivi vifungu Magufuli hakuvizingatia as far as we know, na ndivyo vinavyomfanya awe kavunja katiba.
Mkuu hiyo ni interpretation yako tu!
Na hii je?
40.-(1) Subject to the other provisions of this Article, any person who holds office as President shall be eligible for re-election to that office. (2) No person shall be elected more than twice to hold the office of President.

Dadavua SHALL pia hapa!!
 
Umesoma subsection 3 hii ya sheria iliyoundwa kuelezea utaratibu wa kurenew mkataba wa CAG? :Soma hii hapa Chini:

View attachment 1254017

Then kutokana na Profesa Shivji kusoma kipengele hicho naye akasema yafuatayo:

View attachment 1254021

kutokana na kifungu hicho subsection 3

Ni dhahiri kwa mujibu wa sheria, Sheria inataka kuwa CAG aliyemaliza muhula wake wa kwanza LAZIMA aongezewe miaka mingine mitano isipokuwa tu kama Rais hataki kuendelea naye basi yapaswa kufuata mchakato wa kumtoa kama ilivyoelekezwa na ibara ya 144 ya katiba.

JPM Kavunja sheria kwenye hili suala, Ameteua CAG mpya kinyume cha sheria

Sikubaliani na lugha iliyotumika kwenye hiyo sec 3.

Haipo definitive. Hakuna haja ya kuandika shall be eligible.

Andika tu ‘shall be renewed’ na hakuna ubishi.
 
Well, kama ni hivyo basi Assad aende mahakamani.

Manake kama ni dhahiri namna hiyo kama ulivyowasilisha, the whole thing should be a slam dunk open-and-shut case.

Pia nimeona kuna tatizo kubwa sana la uelewa wa lugha ya Kiingereza.

Suala la ‘shall be eligible for renewal’ ni suala jepesi sana lisilohitaji hata mabishano.

Ila sasa sishangai kwa nini hata baadhi ya watu walikuwa wana cite hicho kipengele kuwa ndiyo kimevunjwa!

Nyani Ngabu.
The issue is not about "shall be eligible", that is not a problem at all because eligibility does not imply "A must get something"

The Place where Magufuli made a mistake is in violating the following subsection:

Img-1572853035577.jpg
 
Back
Top Bottom