Suala la mwanaume kuoa miaka hii ni gumu, labda mtu ujilipue tu

Suala la mwanaume kuoa miaka hii ni gumu, labda mtu ujilipue tu

Ndoa ni mradi qa kumfaidisha mwanamke mwishoni na si eneo ambapo mwanaume atapata upendo wa dhati na kupendwa kwa yeye kama yeye. Mwanamke anatazama wewe unampatia nini. Akitokea mwanaume wa kumpa anachotaka wewe ni wa kazi gani tena kwake.

Sasa huo si ni upuuzi. Me nikae napiga goti kuomba upuuzi. Hapa watapata dudu mali kila mtu atafute zake. Imesha hiyo.
NAKAZIA
 
Wanofaidi ndoa ni wale watu pori , kiukweli ndoa za mjini mwanaume usiwe mjuaji , oa tuu ili kujenga familia basi wanawake wa mjini ni pasua kichwa haswaa...hata hvyo ni hao hao tuu unakomaa nao , hawa viumbe ni dynamic sana , unaweza kuwa nyakat fulani mnafurahaia ndoa kabisa , nyakat fulan anakuzingua ile ile , ukimuona mwamba mjini ameoa npe saluti sana
Hahahahah ndoa ni fumbo la imani.
 
Shida baadhi ya wanaume mnataka wanawake perfect wasiokosea. Swala la kujiuliza are you perfect?

Yeyote ambaye yupo kwenye ndoa anajua kuna siku vurumai inaweza tokea ndani na mkanuniana kutwa nzima na maisha yakaendelea. Hakuna mkamilifu kwenye maisha ya ndoa muhimu ni kuyajua mapungufu ya mwenzio na kuyaishi.

Lakini sio kutwa kunyooshea wanawake vidole kua sisi tu ndio wenye shida kwenye ndoa.
 
Shida baadhi ya wanaume mnataka wanawake perfect wasiokosea. Swala la kujiuliza are you perfect?

Yeyote ambaye yupo kwenye ndoa anajua kuna siku vurumai inaweza tokea ndani na mkanuniana kutwa nzima na maisha yakaendelea. Hakuna mkamilifu kwenye maisha ya ndoa muhimu ni kuyajua mapungufu ya mwenzio na kuyaishi.

Lakini sio kutwa kunyooshea wanawake vidole kua sisi tu ndio wenye shida kwenye ndoa.
Sijazungumzia kupata mtu perfect kwasababu hayupo, ila kwa mfano wewe ni mwanaume, ukikutana na mdada mwenye tabia nlizoorodhesha kwenye huu uzi wangu, tena mwanzoni mwa mahusiano kwenye kufahamiana, utakomaa nae tu Mrs Van
 
Si huwa mnasema, hawa wanawake ni kuwazalisha tu na kuwaacha, ili wabaki single mothers hakuna kuwaoa

Halafu ninyi mkitaka ngono mtanunua hata malaya, sasa uzeeni mwanamke atabaki na watoto wake, wewe utabaki na hao malaya wako simple tu

Na uzuri ni kwamba hiyo kauli ya fainali uzeeni wanaoongoza kuisema ni wanaume wenyewe, tena wengi ni wale ambao waligoma kuoa wakafanya starehe zote, na kujifanya eti wako busy kutafuta pesa

Sasa wamekuwa watu wazima ndio wamejua ukweli kwamba walikuwa wanapoteza muda tu, maana hata hizo pesa zenyewe walizojifanya wanatafuta hawafanyii mambo ya maana, asilimia kubwa wanaishia kuhonga hivyo haziwasaidii sana huko uzeeni

Msidhani msipooa mnawakomoa wanawake mnajikomoa wenyewe, nimekuja kugundua tofauti ya mwanamke asiyeolewa na mwanaume asiyeoa ni kwamba, mwanamke atatukanwa ujanani ila uzeeni atafarijiwa na wanaye

Lakini mwanaume atasifiwa ujanani ila uzeeni itakuwa zamu yake naye kutukanwa na kuitwa mtu mzima hovyo, hasa asipokuwa na pesa na hawa ndio wengi tulionao kwenye jamii zetu, maana kumbuka si kila mwanaume atafika uzeeni akiwa kama Mo au Bakhresa

Tuache kujidanganya ndoa ni muhimu kwa jinsia zote unaposema ndoa ni muhimu kwa mwanamke ila siyo kwa mwanaume hiyo haimake sense, sababu mwanamke anaolewa na huyo huyo mwanaume tendo linalohusisha jinsia mbili haliwezekani kuwa na maana tofauti kwa kila jinsia, hayo mengine ni imani tu ambazo jamii zetu imetengeneza kumsifia mwanaume na kumkandamiza mwanamke hata pale ambapo unaona kabisa hakuna uhalisia
Sawa mkuu nimekuelewa, lakini je, ni kweli unachosema kwamba mtu asipooa/kuolewa anadharaulika....
 
Back
Top Bottom