Sukari madukani hamna, tatizo ni nini wakati tayari kuna bei elekezi toka Serikalini?

Ni ngumu na haitekelezeki kwa kuwa wauzaji wa Jumla wanauza zaidi ya bei elekezi ya serikali, sasa mfanyabiashara gani kichaa anunue sukari ambayo atakuja kuiuza kwa bei ya hasara, walichofanya wafanyabiashara ni kuacha kununua mzigo mpya na wale wachache walio nao bado wanauza kwa bei ambayo itawapa faida ambayo ni tofauti na ile bei elekezi ya Serikali
 
Nashukuru nilikuwa na msafiri kutoka Zenji ameniletea mfuko wa kilo 5 ambo alininunulia kwa 9000.

"رمضان كريم وصوم مقبول"
 
Huku kwetu, walipotangaza tu bei elekezi, wauzaji wakashusha bei ghafla. Agizo linatekeleza bila shuruti
 
Hai baada ya doria ya mkuu wa wilaya sasa sukari imepotea kabisa na ukiuziwa ni mpk mtu awe anakujua kama hakujui sukari ni hakuna.
Source Fb page ya redio Bomang'ombe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…