Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani sukari ina umuhimu gani katika maisha? Iuzwe hata elfu 10 kilomojaKilo ya sukari Tz imefika Tshs.5,000/, nadhani serikali inatakiwa itoe tamko kutupatia walaji mwongozo wa kufuata kutoka kwenye anguko hili.
Sababu tunayopewa ni dhaifu kwamba mashamba ya miwa yamefurika maji wakati TMA ilitoa tahadhari miezi 2 kabla ya mvua kushuka. Nadhani ni Tz pekee ambako mvua na jua ni laana isiyokoma kwa kilimo, umeme, maji, mifugo, uvuvi nikitaja kwa uchache.
Aidha, viwanda vya sukari vya Magereza vilivyojengwa kwa kasi ya mwanga hatujui vimefikia wapi baada ya kutumia fedha za umma kwenye ujenzi huo kama machinjio ya kisasa ya Vingunguti, Kibaha, Simiyu na Manyara vilivyobaki kuwa makumbusho ndani ya nchi ambayo ni ya pili kwa idadi kubwa ya mifugo barani Afrika?
Tz sukari haijawahi kushuka kwa miaka 23 mfululizo tangu Julai 2001 licha ya mashamba ya miwa kuongezeka na viwanda vipya kujengwa Morogoro na Bagamoyo pamoja na uingizaji wa sukari ya nje ya nchi.
Tz sukari ni miongoni mwa bidhaa na huduma ambavyo vimekuwa vya kidemokrasia vikiwemo Korosho, Mafuta ya mitambo, Mafuta ya kula, Katani, Umeme na Maji.
Nchi kubwa, hali ya hewa ya kitropiki, mitambo ipo, rasilimaliwatu rahisi wapo, soko la ndani lipo lakini tumeshindwa hata kwenda kujifunza Uganda tu hapo namna ya kuendesha sekta ya sukari.
Ni kama vifuatavyo vyote 4 vimefeli jumla kwenye sekta ya sukari:-
1. Sheria ya Taifa ya Sukari 2001 (National Sugar Act 2001).
2. Taasisi ya Sukari Tz (National Sugar Institute).
3. Shirika la Maendeleo ya Sukari (Sugar Development Corporation SUDECO).
4. Makampuni ya Sukari (Sugar Factories).
NB.
1. Tz ina makampuni 5 ya sukari kwenye mikoa 4.
2. Kenya ina makampuni 16 ya sukari.
3. Uganda ina makampuni 14 ya sukari.
4. Zambia ina kiwanda cha sukari kikubwa kuliko vyote barani Afrika tangu 1964.
Uganda ina sukari kuzidi mahitaji ya ndani na hawajui wapeleke wapi ziada hadi waliwahi kuiomba Tz ichukuwe sukari yao hata kwa mkopo ili maghala yao yawe wazi kupokea uzalishaji mpya maana hawawezi kumwaga ziada ziwani.
Sasa mapapa wa biashara ya sukari wanapiga jaramba ili serikali iruhusu uagizaji toka nje ya jamhuri. Nadhani kwa spirit ya EAC serikali ichukuwe sukari ya Uganda ambayo nayo pia itapunguza bei kwa sababu ni jirani nasi kuliko kutoa sukari ng'ambo ya bahari. Let us think over and handle this matter strategically, progressively and proactively.
Bei ya sukari ikipanda vifuatavyo navyo vinapanda kwa sababu kuna aina nyingi za sukari zinazotengeneza bidhaa mbalimbali:-
1. Bei ya Soda kufuatia kupanda bei ya sukari.
2. Bei ya vitafunwa (mikate, maandazi, vitumbua, keki nk) kufuatia kupanda bei ya sukari.
3. Bei za madawa ya syrups kufuatia kupanda bei ya sukari.
4. Bei za sharubati kufuatia kupanda bei ya sukari.
5. Bei za sweets kufuatia kupanda bei ya sukari.
6. Bei ya wanzuki (inayotumia sukariguru) kufuatia kupanda bei ya sukari. Whatnot?
NB.
Miili yetu inapokea sukari kwa 99% ya vitu tunavyokula na kunywa hivyo sukari ni maisha (Sugar is Life)
Sir Richard Gordon Turnbull GCMG hakukosea kutumia viboko kutawala Tanganyika.
anaupiga mwingi halafu eti aongezewe mitano...... kilo laki mbiliViongozi mko wapi mbona mmenyamaza kimya juu ya upandaji holela wa bei ya sukari nchini
Hatari sanaaaanaupiga mwingi halafu eti aongezewe mitano...... kilo laki mbili
Machawa yanasifu kwa nyimbo na mapambioHahhaha... Machawa wa mama wanaumbuka!
Hapo yalipo yalikuwa yanamlaumu Magu ila mama yao sasa ndio anavunja rekodi
Usipokunywa chai utakufa?Viongozi mko wapi mbona mmenyamaza kimya juu ya upandaji holela wa bei ya sukari nchini
Acha ubwege sasa sukari inatumika kwenye chai tu?Usipokunywa chai utakufa?
Inatumika na kwenye uji kwani wewe mgonjwa Hadi unywe uji?Acha ubwege sasa sukari inatumika kwenye chai tu?
Bado hujakua kiakili na kimwili usikute unaishi kwa wazazi wako umozoe kuletewa mezani siku ukinza kujitegemea ndo utaelewa tunazungumza ninInatumika na kwenye uji kwani wewe mgonjwa Hadi unywe uji?
Naona taratibu , pumzi ya kumtetea bi mkubwa inaanza kukata.Usipokunywa chai utakufa?
Ndoto za mchana. Ujamaa ulishashindwa huoKweli mkuu, wanaweza hata kuhonga viwanda visizalishe ili wasipate ushindani wa bei kwa shehena zao za kutoka nje ya nchi.
Dunia inakoelekea kuna dalili zote kuwa Marxism inarudi. Tayari BRICS (wafuasi wa Marxism) pekee imeishateka 17.% ya eneo la sayari ambapo wanachama waanzilishi pekee wana soko la walaji lenye ukubwa wa watu 3.27 bl sawa na 41.13% ya watu wa dunia. BRICS inatarajia kumiliki uchumi wa dunia ifikapo 2050 miaka 26 tu ijayo.