Sukuma liwe kabila tambulishi la mtanzania

Sukuma liwe kabila tambulishi la mtanzania

Kiufupi ni watu poa sana, nimeishi nao sana hawana fujo mpaka umchokoze
Kuna jamaa mmoja ana duka la vipodozi huwa anawauzia airfresh km mbadala wa spray na wanazipenda sababu ni makubwa[emoji23] akili zao wanazijua wenyewe hao watu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Jamani kwema?

Mambo yasiwe mengi ngoja niende kwenye Jambo lenyewe,Katika hekaheka nazopewa na mwalimu ulimwengu wiki hii nimejikuta nipo usukumani ndani kabisa,nimekutana na kina Ngosha original achana na Hawa kina Ngosha wa mjini kina Shimba ya Buyenze ,kiukweli nimefurahi Sana kufika huku nikaona hivi kwa Nini watanzania wote tukiwa nje ya nchi si tujiite tu WASUKUMA?
Nimejifunza vichache kwa siku mbili nilizokuwapo hapa

1.WAKARIMU SANA
Hawa watu wanahitaji kuolewa hongera,imagine nimefikia nyumba ya wageni,kufika saa moja usiku nijiandaa nitoke nikatafute chakula Nasikia nagongewa mlango,kufungua namkuta dada aliyetupokea na sahani mkononi ananikabidhi, nikamwambia hapana utakuwa umekosea sijaagiza chakula akaniambia hapana nimepika nimekuletea mgeni wali na "sansa"nikajiuliza hiyo sansa itakuwa nyama ya porini ngoja nipokee,kufungua nikakuta mboga ya majani imeungwq karanga kuonja hakika ilikuwa tamu Sana,Asubuhi nataka kutoka kaniambia dada Subiri unywe uji na matobolwa,nikajua hayo matobolwq yatakuwa sijui ni maandazi,nikasema ngoja Nile tu,nikazugazuga nikasema sawa basi nikapewa uji na viazi vitamu Ila vimeandaliwa tofauti vilikuwa vitamuu kumbe ndio mabolwa,,basi nikala nikasema huyu hajui watoto wachalamila kwa Ganda la ndizi...Ila kesho nikiondoka nitampa wekundu mmoja nimependa ukarimu wake

2.WANASHANGAA SANA
Jamani Hawa watu wanashangaa kuliko kawaida,Yaani wanashangaa Hadi na Mimi nikaanza kujishangaa

3.WANAPENDA LUGHA YAO
Yaani watu wanapenda lugha yao hatari,eti wananisalimia kingosha[emoji849][emoji849][emoji849] mimi najua Sasa nabaki natoka macho tu

4.WANAPENDA BAISKELI
Jamani na miongo yangu kadhaa hapa duniani nilikuwa sijui baiskeli Zina matajiri ya kila rangi,jamani kina baiskeli huku Zina matajiri mekundu,ya Njano,ya kijani,ya purple ya blue,hizo baiskeli zimepambwa na maua,usiku zinawakawaka Kama Xmas tree na zimefungwa redio... baiskeli huendeshwa na watu wa rika na jinsia zote

5.REDIO ZA MKONONI
Jamani Kila mtu kabeba kiredio mkononi kinaimba kisukuma,sijajua hao wasanii wa hizo nyimbo zao wako wapi..huku sijasikia Amelowa Wala Salome yaani unaeza dhania hauko Tanzania

6.WADADA
Ama kiukweli wadada zao wanaushirikiano Sana,timu niliyoongozana nayo kikazi na furaha sana maana wameambiwa wajisikie nyumbani [emoji1751][emoji1751][emoji1751]yaani huku ningekuja na swahiba wangu bwana mzabzab angelowea huku

7.WAKAKA
Sijui ni wapenzi Sana wampira au lah,Kila kijana kavaa jersey,Kuna jezi za kika Ligue huku kuanzia la Liga,bundesliga,CAF Hadi za wale waliovunja uwanja juzi,yaani kwenye Vijana 20 wasiovaa watakuwa watatu
8.MAJI
Jamani bunge la bujeti mwaka hii lielekeze fedha za kutosha kwenye wizara ya maji ndugu zetu wapate maji safi na Salam,kweli huku Kuna maji hayana tofauti na chai ya maziwa.
9.UTANI
Jamani Hawa watu wanataniana jamani ukisikia na Ile lafudhi yao utacheka mpaka machozi

Jamani Wana mambo mengimengi Sana,nashauri raisi ajae awe tu NGOSHA maana ni taifa kubwa
Maswalj atajibu huyo ndugu yao hapo juu Sina mtandao
Thòleo Mayo...Naghene sana...
Tukwibhona....

Cc Shimba ya Buyenze
 
Wao wenyewe wakifika Dar, hawataki kujulikana kama ni Wasukuma. Sembuse sisi Taifa tujitambulishe kama Wasukuma? 😅😅

Kuna msukuma mmoja alipendaga t shirt niliyokuwa nimevaa. Akaniuliza nimeinunua wapi, nikamtajia sehemu pamoja na bei (ilikuwa 14k). Jamaa akaenda direct mpaka pale akamwambia muuzaji "Naomba ile t shirt ya elfu 14" 😅😅


NB: Sipo serious jamani, kina Ngosha msije wangu wangu 😅😅
Huwajui Wasukuma wewe! Hujawahi kukutana nao katikati ya Kariakoo wanapiga Kisukuma?
 
8.MAJI
Jamani bunge la bujeti mwaka hii lielekeze fedha za kutosha kwenye wizara ya maji ndugu zetu wapate maji safi na Salam,kweli huku Kuna maji hayana tofauti na chai ya maziwa.
Uko Kishapu nini? Nitafute hapa Shinyanga wakati unarudi!😁😁😁
 
Wasukuma ni kabila kubwa kuna wachache wao sijui wanatokea Bariadi au wapi wana changamoto sana. Nimeishi na Wasukuma na ni watani zangu nawapenda ila hata wao wenyewe wanajuana wapi ni wa kuishi nao kwa makini. Ukweli ni kwamba hawatabiriki.

Fanya utafiti mdogo JF, Clouds, EATV na kwingineko wapi taarifa za mauaji ni nyingi. Shinyanga, Geita, Mwanza na Mara, hapo kasoro mkoa wa mwisho ndio Wasukuma sio dominant. Na mikoa yao ndio ilikuwa inaua albino na vikongwe.

Wanawake wao wana rekodi nzuri kasoro mwaka jana ndio kesi kubwa zilikuwa ni zao.
Hakuna kabila ni perfect ila ukijua changamoto zake inakupunguzia matatizo.
Kw hiyo unapima matukio kwenye mwdia houses?
Geita wala hupajui na nikwambie hakuna sehemu tamu ya kuishi kama ile hata Mwanza haifui dafu (sina maana ya uzuri wa mazingira)
 
Yaani mi mtu akinipa offer anigeuze niwe msukuma then anipe million 50, siwezi kukubali nitakataa......... Badala yake ntamwomba anigeuze niwe andazi alafu nimpe yeye million 50 ili awe na million 100 kabisa
 
Ukienda Umasaini usisahau pia kutuandikia kauzi kama haka...

Tambua tu kwamba kuna mtu na kuna m'maasai...
 
Ushagoo yoyote ukienda ambayo watu wanaongea lugha zao, ikitokea tu ukaongea Kiswahili tarajia yafuatayo...

1. Utaonekana una dharau
2. Utauziwa bidhaa bei juu
n.k
walinichukulia hivyo. Huo ni ubinafsi
 
Back
Top Bottom