Sumaye: Kinana anapiga dili za meno ya Tembo

Sumaye: Kinana anapiga dili za meno ya Tembo

Hivi hata ukiacha hilo la Tembo inakuwaje katibu mkuu wa ccm amiliki mameli ya kibiashara? Hii haileticmgongano wa kimaslahi! Si atapendelewa katika kupewa tenda na mambo ya kodi? Yaani huko ccm kila mtu anapewa sehemu ya kufanyia ulaji! Msekwa maye alipewa uenyekiti wa bodi ya Tanapa. Unashangaa twiga kupanda ndege? Mkapa kajiuzia kiwira! Pathetic!
 
kama kinana ndo kipimo cha maadili ya chama,mm ntakua malaika:sumaye,
 
Kazi kweli kweli, wamemwaga ugali sasa kazi ni kumwaga mboga. Lazima na wao wajibu kuhusu Tembo wetu.

Mwaka huu magamba wamechokoza moto, Haya maneno yao waliyaanza wenyewe sasa mwaiona ngondo mwavunja milango, ngondo igwa iyo mama hiyi.
 
Hili swala la meno ya tembo tunalichukulia poa sana,tunaitia aibu nchi yetu kwa mambo kama haya wanayofanya akina kinana,na kama kinana kahusika na hili anatakiwa aeleze uma,zile nyara zilikua za nani?
 
Jana kwa mara nyingine waziri Mkuu mstafu Ndg. F. Sumaye alimlipua katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi A. Kinana na kusema katibu mkuu huyo kwa muda mrefu amekuwa akijihusisha na uuzaji wa meno ya tembo (pembe za ndovu)... "Soma gazeti hapa chini"

Ilimbukwe kuwa mwaka jana kituo cha utangazaji cha Aljazeera kilitoa data kuhusu tembo wa Tanzania kuuwawa na kuonyesha kwamba mwaka 2007 kulikuwa na jumla ya tembo 146,879 na mpaka mwaka jana 2014 tembo hao wameuwawa kwa asilimia 64% na kubaki tembo 56,000 tu...

Mytake: Hili suala la Kinana tulifikiri ni uzushi ila ukiona waziri mkuu aliyekaa madarakani kwa miaka 10 kaliweka wazi mbele ya wananchi ni wazi hakuna ubishi tena katika hilo....
kinana hagombei urais. angeligombea bila shaka angekatwa kama ni fisadi. labda sumae anafahamu kwa nini ccm imemkata yafaa atuambie.
 
Kamata hao weka ndani. Magufuli analalamika kila siku nchi ina mijizi. Si ndiyo hiyo aanze nayo ili atushawishi kama kweli anammanisha?
 
Dah alisema msigwa wakasema mzushi sasa ni waziri mkuu wakabushe tuone
 
Haya kwa mara nyingine Kinana anaguswa na kashfa ya kumaliza tembo wetu. Hivi TISS huwa wanafanya kazi kwa maslai ya Umma au kwa maslai ya Viongozi wa CCM?
 
kinana hagombei urais. angeligombea bila shaka angekatwa kama ni fisadi. labda sumae anafahamu kwa nini ccm imemkata yafaa atuambie.
Sumaye alikatwa kwa sababu Raisi Kikwete alitaka kuwaweka anayesemwa ni Mdogo wake wa damu Membe na wanayesema ni girl friend wake tangu wakiwa chuo Asha Rose Migiro
 
Ukawa wanatumia mbinu za kisayansi kuendesha kampeni.
sumaye analipua mabomu na kwa akili za kawaida mtu kama sumaye wananchi wa kawaida watamuamini anayosema maana alikuwa waziri mkuu anajua kila kitu tofauti na slaa kama angezungumza wengi wasingeamini maana hakuwahi kuongoza serikalini.
lowassa anashambulia kwa sera ya kuleta mabadiliko ya maendeleo.
sehemu yoyote kwenye mkusanyiko wa watu ukikusanya maoni utakuta lowasa anakubalika kwa wastani mkubwa kupita jpm.

Acha uzushi ndugu yangu sehemu yeyote wapi!? Sisi kijiweni kwetu sio wanywa viroba tusiojua kama hivyo vijiwe vinginevyo, ila tusubiri uone magufuli anavyoingia ikulu
 
Back
Top Bottom