Sura ya Mungu kupitia Wajapani

Sura ya Mungu kupitia Wajapani

Define common sense.

Dhana ya contradiction katika hoja ya uwepo wa Mungu sijaitoa katika dini, ni dhana ya kifalsafa.

Kwa nini unafikiri nimeitoa katika dini?

Na hata kama ningeitoa katika dini, ninapoitoa dhana si kitu muhimu kama usahihi wa dhana.

Kwa sababu hata kichaa anaweza kusema neno la maana siku moja.
Common Sense ni Akili ya Kawaida..

Umesema ni dhana ya Kifalsafa.. Kwahiyo contradictions zake ni kwenye Falsafa..
Ambazo Falsafa ni theories tupu.. Assumptions za kutosha.. Logics..

Leo ukiwa kipofu.. Ukaweza kuleta hoja hakuna mwanga sababu wewe huoni.. Hoja ukaweza kuitetea ni falsafa hiyo..!

Ukitumia common sense hata kama ni kipofu utajua kuna mwanga..!
Kifalsafa kipofu hawezi kusema kuna mwanga..
 
Kupitia jaribio la solar na motor tayari mtu kipofu atajua mwanga upo au haupo kwa kuhisi uwepo wake kupitia utendaji wa kazi.

Lakini si kila penye joto kuna mwanga, au kwenye kila mwanga kuna joto, kupitia hilo somo tayari atajua kuna nguvu ya mwanga japo haoni, kwani hata sie wazima hatuoni electromagnetic waves, lakini tunaona utendaji wake.

Thanks.
Kipofu atajuaje sasa ni mchana au ni usiku afanye jaribio..!!?
 
Mtu mwenye akili na anayeona vizuri, atayaangalia mazingira yanayomzuka, kwa wazi kabisa atahisi kuwepo kwa nguvu kuu ambayo inamzunguka yeye na dunia yote, ataona ujuzi, nguvu na utashi wa kuishi. Hivyo vyote humlazimisha mwanadamu kukubali kuwepo kwa uwezo wa akili ya fani zote ikiwa ipo nje ya dunia ya kimaumbile.

Mtu yoyote anaye tathmini nafasi yake hapa duniani anaweza kutambua kwamba kuna nguvu inayomuumba yeye, ikamleta yeye hapa, inayomtia usongefu ndani mwake, na halafu tena humwondoa, bila ya ruhusa au msaada wake kutakiwa kwa ajili ya lolote katika hayo.

Ukitaka mpaka kusubiri uthibitisho wa kuweko kwa Mungu kutoka kwa mtu/kitu ambacho nachenyewe kinategemea Mungu kwa kuwepo kwake basi utasubiri sana Kwani hakuna siku Mungu alifichika kuhitaji uthibitisho.

Mara nyingi kuangalia mazingira tu kunapotosha.

Mathalani.

Mtu anaweza kukaa kibarazani kwake, akaangalia ardhi, akajua dunia ni bapa.

Kumbe dunia ni tufe.

Mtu anaweza kuangalia angani, jua linachomoza , linazama, akafikiri jua linaizunguka dunia.

Kumbe dunia ndiyo inalizunguka jua.

Kama vitu vilivyo complex vinahitaji akili kubwa zaidi kuviumba viwepo, hoja hii inathibitisha haiwezekani awepo Mungu muumba vyote. Kwa sababu na yeye atakuwa complex na atahitaji muumba wake, na muumba wake atahitaji muumba wake, ad infinitum, ad nauseam.

Kwa hivyo, hoja yako ya kwanza nimekuonesha hatari ya kutafuta majibu ya maswali makubwa kwa njia nyepesi nyepesi tu. Unaweza kupotoka kirahisi. Inatubidi tujifunze sana, ukweli mara nyingine uko counterintuitive. Unaona dunia bapa, wakati ni tufe. Unaona jua linazunguka dunia, kumbe dunia ndiyo inqzunguka jua.

Scale yetu kwenye universe haitupi uwezo wa kuona na kujua mengi, inabidi tuchunguze kwa kina kabla ya kujiridhisha.

Hoja yako ya pili, also in a counterintuitive way, inatuthibitishia Mungu muumba vyote hawezi kuwapo.
 
Common Sense ni Akili ya Kawaida..

Umesema ni dhana ya Kifalsafa.. Kwahiyo contradictions zake ni kwenye Falsafa..
Ambazo Falsafa ni theories tupu.. Assumptions za kutosha.. Logics..

Leo ukiwa kipofu.. Ukaweza kuleta hoja hakuna mwanga sababu wewe huoni.. Hoja ukaweza kuitetea ni falsafa hiyo..!

Ukitumia common sense hata kama ni kipofu utajua kuna mwanga..!
Kifalsafa kipofu hawezi kusema kuna mwanga..
Wewe unasema falsafa na logic ni dhana tu.

Unaelewa kwamba hiyo computer/ simu inayokufanya uwasiliane nami hapa inatumia logic?

Unaelewa haya maandishi tunayotumia kuwasiliana yanatumia logic?

Unaelewa kwamba hata kuhoji falsafa na logic kutaka kuziponda, ushatumia logic?

Unaelewa kwamba hata huo mfano wako wa kipofu anayesema hakuna mwanga, unaiponda falsafa na logic, hapo hata wewe umetumia logic bado?
 
Wakati wa Vita ya pili ya dunia, majeshi ya Japan yalifanya unyama mkubwa sana huko China na Korea.

Huenda waliamua kujenga upya jamii yao.
 
Wewe unasema falsafa na logic ni dhana tu.

Unaelewa kwamba hiyo computer/ simu inayokufanya uwasiliane nami hapa inatumia logic?

Unaelewa haya maandishi tunayotumia kuwasiliana yanatumia logic?

Unaelewa kwamba hata kuhoji falsafa na logic kutaka kuziponda, ushatumia logic?

Unaelewa kwamba hata huo mfano wako wa kipofu anayesema hakuna mwanga, unaiponda falsafa na logic, hapo hata wewe umetumia logic bado?
Logic ninazoongelea sio za computer na simu.. Computer na Simu hizi technology..!

Sijahoji Falsafa.. Nimeelezea..

Yes.. Na hiyo ndio point.. Ukitumia logic unaweza kuprove vitu vingi..hata kama sio vya kweli..
Mimi Kipofu huwezi kuniambia kuna mwanga na sijawahi kuuona.. Mchana na usiku hakuna kitu hicho.. Kwangu kote giza.. Sasa ikija uwepo wa MUNGU logic haina kazi..!
Inatakiwa Common Sense..!
 
Unaelewa kwamba processor ya computer na simu inatumia logic gates?

Common sense ndiyo inaruhusu contradiction?

1_Id1PR-WSapj7nC0xg9kiNA.jpeg
 
Akat bongo mtu cm ikiita anaacha km dakk 5 msikie wimbo vizur [emoji1]
 
Back
Top Bottom