Mungu anayekula kiti moto na Mungu asiyekula kiti moto vitu viwili tofauti
Mwandishi,
Mimi ni Christian, Kwenye mada husika, ni vitu vingi umeandika, hasa ni maswali ambayo kiuhalisia ni mazuri, yanafikirisha
Lakini, ukajisahau kutambua, jamii iliyopo inayounda utaifa, ni hiyo hiyo ya watu wenye dini ya Uislamu, Ukristo na upagani, na ndio hao Wapo bungeni, ndio hao wanapiga mziki wa rumba, ndio hao utawakuta Wapo msikitini na kanisani
Sasa unachozungumza kulalamikia Kodi zinatumika isivyo, eti tu inahudumia jamii ya wenye dini wakati TBC ilipaswa ihudumie mambo ya kitaifa Kwa kuwa Kodi inayotumika sijui walipaji ni kina nani, maana hujawataja walipa Kodi na wanaostahili kuitumia TBC
Ikiwa ni hivyo, ungeonyesha kukerwa pia, vipindi vya mziki wa kina daimond zikipigwa na kuonyeshwa TBC, Kwa kuwa na wao Wana dini Yao ya kipagani, Kwa nini miziki Yao ipigwe na kuwa na vipindi vyao TBC wakati walipa Kodi ni pamoja na waislamu na wakristo??
Ukiwaondoa hao wote, utuonyeshe sasa mlipa kodi ambaye unadai ndio anapaswa aitumie Tbc
Jambo la mwisho,
Chaneli za Dini na za kipagani, zimepatikana huku waliofanikisha uwepo wake, walikuwa wakiendelea kulipa Kodi ili zikatumike Kuendesha vipindi TBC na bado wanaendelea kulipa kodi, na chaneli zao wanalipia, na Kodi hizo zinaenda kuiwezesha TBC, Je ni Nani mwenye haki ya kuitumia TBC? Maana najua hata wewe mwenyewe ukitoka hapo utaingia kanisani ama msikitini, tuonyeshe ni Nani anastahili kuwekewa vipindi vyake hapo TBC Ukiondoa waamini wa dini na wapagani?
Haya ndiyo mambo ya kuandika sifuri ukafuta ziro
Kwa mawazo yangu, Mimi naona umekurupuka mzee