Swali kwa Ayubu Rioba: Siku hizi sera ya Taifa inaruhusu taasisi za kidini kunufaika na fedha za walipa kodi kupitia TBC?

Swali kwa Ayubu Rioba: Siku hizi sera ya Taifa inaruhusu taasisi za kidini kunufaika na fedha za walipa kodi kupitia TBC?

Utakubali kuwepo na vipindi vya dini ya kihindu pia? Wahindi wanalipa kodi kubwa sana pia.
Wakiomba na wao,wanapewa,ni kwamba hawajaomba,Tulisoma shule na wanafunzi wa kisinga singa,wa kiume,wakivyaa vilemba kichwani,ni baada ya kuombewa na viongozi wa dini yao,kuwa hiyo ni imani yao,na ilikuwa shule ya serekali,hawakukatazwa kuvyaa.
 
Utajipa tabu sana,katika lugha ya kiswahili karibia 30%ni maneno ya kiarabu,hii lugha kuikwepa sio rahisi,hata namba 0123456789,tumefundishwa mashuleni ni namba za kiarabu.Itabidi hata kiswahili na namba tuache kutumia.
Sio kweli kwamba katika lugha ya kiswahili karibia 30%ni maneno ya kiarabu. Kamusi Kuu ya Kiswahili niliyo nayo hapa mezani imeonyesha kwenye mabano maneno yote yenye asili ya kiarabu. Hayazidi asilimia tano.

Pia, hata kama ni kweli kwamba tarakimu za 0,1,2,3,4,5,6,7,8,9 ni namba za kiarabu tayari zimebantuishwa. Ni kama ambavyo tunajenga nyumba, kuvaa nguo, na kuendesha magari yasiyo ya kibantu. Mambo haya hayana athari kwa Utaifa wetu.
 
Hapana. Habari ya "kuzima TV" haina nafasi katika hoja hii kwa kuwa TBC ni civi space.
Yaani TBC ni eneo ambalo linapaswa kuwa huru dhidi ya kanuni na mienendo ya kiparokia (particular phenomena), ambayo ni kinyume cha kanuni na mienendo mtambuka (universal phenomena).
Mkuu Kama una hoja peleka ofisini kwao moja kwa moja ingawa nina uhakika itagonga mwamba.

Hii ni nchi secular huwezi kumpangia mtu asikilize au asisikilize kitu kipi.

Mimi mkatoliki ikifika ijumaa asubuhi sisumbuki kufungulia TBC na pia sijisumbui kuangalia channel yoyote ya dini isiyokuwa yangu ingawa ninao marafiki wa dini zote.

Ndivyo tulivyolelewa kama taifa, kuvumiliana.
 
Nashauri yawepo, kama watakuwepo na wengine wataoona hawajatendewa haki kwao kutokuwa na sikukuu yao nao wanatakiwa ku-propose siku wanayotaka kuwa yao ya mapumziko wapeleke mapendekezo yao serikalini.
Kwahiyo kwa upande wako hauoni kuwa hilo linahusisha dini na serikali?
 
Tuache kupoteza muda na mambo ya kubalance. Taasisi, mifumo, idara na shughuli zote za serikali zisitumike kama jukwaa la dini YOYOTE.
Utakuja kukataza pia wanaokwenda miskitini na makanisani,mahekaluni,wasipite kwenye barabara zilizojengwa kwa kodi zao.
 
China wanaapa kwa Katiba tu na hakuna mambo yoyote ya kidini yanahusishwa katika viapo au kuendesha serikali.
Sisi sio wachina na msingi wa uwepo wa taifa letu haufanani na ule wa China.

Soma historia za mataifa mbalimbali itakusaidia kukuza upeo wa kidunia.
 
Vyombo vya sheria havipaswi kuwa jukwaa la dini yoyote. Kuna kipi kigumu hapa huelewei hadi unatukana makabila mengine??
We na ukoo wako mtakua masikini wakutupwa huko Usukumani, yaani we leo ndio umeona TBC inatumika kidini baada ya kuona waislam? Vp jumapili zote huwa huoni ya mapambio? Kweli mmeshikwa make..nde na mmekosa la maana lakujadili, nyie makafiri mna shida sana, wakwenu akiongoza nchi hua mnakuaga vipofu, kwa Taarifa yako mjijue mna matatizo maana kila awamu yenu ndio Taifa huteseka maana neno Haki kwenu hamnaga kabisa
 
TV inayolipiwa kodi na watu wa dini zote, waganga na wasio na dini haitakiwi kutumika kama jukwaa la baadhi ya imani mbili au tatu tu. Na ili kuondoa huo mkanganyiko vipindi vya dini visirushwe katika TV au redio za taifa pamoja na magazeti.
Hizo dini zina vyombo vyake binafsi, ingeleta mantikia kama vingekuwa vipiandi vya dini zisizo na vyombo vya habari kabisa
Hao wa dini mbili tatu pengine wanalipa kodi kubwa kuliko hao wasio na dini.

Wahindu ni sehemu ya hao wa dini mbili tatu, umeshajiuliza Marehemu Subhash Patel alikuwa analipa kodi kubwa kiasi gani?.

Umeshajiuliza Azim Dewji ameshalipa kodi kubwa kiasi gani tangu aanze kufanya biashara zake?.

Huu utaratibu ndio unaoliweka taifa letu hivi lilivyo.
 
Sio kweli kwamba katika lugha ya kiswahili karibia 30%ni maneno ya kiarabu. Kamusi Kuu ya Kiswahili niliyo nayo hapa mezani imeonyesha kwenye mabano maneno yote yenye asili ya kiarabu. Hayazidi asilimia tano.

Pia, hata kama ni kweli kwamba tarakimu za 0,1,2,3,4,5,6,7,8,9 ni namba za kiarabu tayari zimebantuishwa. Ni kama ambavyo tunajenga nyumba, kuvaa nguo, na kuendesha magari yasiyo ya kibantu. Mambo haya hayana athari kwa Utaifa wetu.
Ndio hivyo hivyo ujuwe hao wenye hizo dini ni watanzania,walipa kodi wana haki kutumia vyombo na miundominu na taasisi za kitanzania.
 
Nazijua haki zangu na najua faida za hali kuwa kama ilivyo.

Mimi sio wa jana wala wa juzi naelewa namna gani Tanzania inavyofaidika na huu utangamano tulionao.
Kama ni hivyo, kwa nini unaunga mkono TBC kutumika kama chombo cha kuendeleza ukoloni wa kilugha na kidini?
 
Mapumziko ya dini ya Eid na Krismas yanagharamiwa na serikali?
Halafu wafanyakazi wa serikali ukiwaambia wakae nyumbani bila kufika kazini hata mwaka mzima huku unawalipa watafurahi sana na wataona ni fursa ya kufanya mambo yao binafsi, hawatalalimika. Tatizo ni kwa watu wanaokosa huduma muhimu siku fulani kwa sababu ya mambo watu waliyojitungia.
Kwahiyo hata haya mapumziko ya kazi kwa sikukuu za dini kama Eid na Krismas nazo pia zisiwepo?
 
Huwezi kutenganisha,dini ya mtu,na miundominu ya nchi,kuanzia barabara,madaraja,vivuko,viwanja vya ndege,viwanja vya michezo,mashule,uanze kuwaliza wanaopita barabarani au kwenye madaraja au vivuko,kuwa wewe,unakwenda kanisani au msikitini kwenye ibada,ili umzuie asitumie miundombinu ya walipa kodi,itakuwa ni maajabu ya kwanza ya dunia.
Katika hivyo vipindi vya Tv,kama ukiona hakikuhusu,unabadilisha channel,hata wasiopenda mziki,dansi,taarabu,rumba huwa hawalalamiki,wanasubiri kuwa na kipindi wanachopenda,watizame.Ndio maana ukaona kuna ratiba ya vipindi,ukifika mda wa unachokipenda,unaangalia.
 
Taifa hili linakwenda kusherehekea miaka 60 ya uhuru desemba mwaka huu.

Sababu kubwa ya kuweza kudumu mpaka hapa lilipo ni uwezo wetu wa kuvumilia na kuishi kama ndugu, uwezo wa kujishusha.

Tungeendekeza akili kama za Huyu mleta mada siku nyingi zilizopita tungeshavunja hii nchi.

Tulifundishwa kuvumilia tangu tukiwa chekechea, kukaa Dawati moja mkristo na muislamu. Ukifika muda wa mkristo kwenda mafundisho anakwenda na muislam kwenda kusoma dini yake anakwenda.

Mawazo ya aina hii ndio yanayovunja nchi kama yakiachwa yaendelezwe pasipo kukemewa.
 
Mungu anayekula kiti moto na Mungu asiyekula kiti moto vitu viwili tofauti
Mwandishi,

Mimi ni Christian, Kwenye mada husika, ni vitu vingi umeandika, hasa ni maswali ambayo kiuhalisia ni mazuri, yanafikirisha

Lakini, ukajisahau kutambua, jamii iliyopo inayounda utaifa, ni hiyo hiyo ya watu wenye dini ya Uislamu, Ukristo na upagani, na ndio hao Wapo bungeni, ndio hao wanapiga mziki wa rumba, ndio hao utawakuta Wapo msikitini na kanisani

Sasa unachozungumza kulalamikia Kodi zinatumika isivyo, eti tu inahudumia jamii ya wenye dini wakati TBC ilipaswa ihudumie mambo ya kitaifa Kwa kuwa Kodi inayotumika sijui walipaji ni kina nani, maana hujawataja walipa Kodi na wanaostahili kuitumia TBC

Ikiwa ni hivyo, ungeonyesha kukerwa pia, vipindi vya mziki wa kina daimond zikipigwa na kuonyeshwa TBC, Kwa kuwa na wao Wana dini Yao ya kipagani, Kwa nini miziki Yao ipigwe na kuwa na vipindi vyao TBC wakati walipa Kodi ni pamoja na waislamu na wakristo??

Ukiwaondoa hao wote, utuonyeshe sasa mlipa kodi ambaye unadai ndio anapaswa aitumie Tbc

Jambo la mwisho,

Chaneli za Dini na za kipagani, zimepatikana huku waliofanikisha uwepo wake, walikuwa wakiendelea kulipa Kodi ili zikatumike Kuendesha vipindi TBC na bado wanaendelea kulipa kodi, na chaneli zao wanalipia, na Kodi hizo zinaenda kuiwezesha TBC, Je ni Nani mwenye haki ya kuitumia TBC? Maana najua hata wewe mwenyewe ukitoka hapo utaingia kanisani ama msikitini, tuonyeshe ni Nani anastahili kuwekewa vipindi vyake hapo TBC Ukiondoa waamini wa dini na wapagani?

Haya ndiyo mambo ya kuandika sifuri ukafuta ziro

Kwa mawazo yangu, Mimi naona umekurupuka mzee
 
Mapumziko ya dini ya Eid na Krismas yanagharamiwa na serikali?
Halafu wafanyakazi wa serikali ukiwaambia wakae nyumbani bila kufika kazini hata mwaka mzima huku unawalipa watafurahi sana na wataona ni fursa ya kufanya mambo yao binafsi, hawatalalimika. Tatizo ni kwa watu wanaokosa huduma muhimu siku fulani kwa sababu ya mambo watu waliyojitungia.
Serikali imehusika na masuala ya dini hapo kazi zimeacha kufanyika kwa sababu ya masuala ya dini walipa kodi wanakosa huduma siku hiyo kwa sababu kuna sikukuu ya dini.
 
Kama ni hivyo, kwa nini unaunga mkono TBC kutumika kama chombo cha kuendeleza ukoloni wa kilugha na kidini?
Sio ukoloni bwana mdogo ndio uhuru wenyewe wa kuabudu na siku zote unazo gharama zake.

Badili chaneli mkuu waachie wenye dini yao wamuabudu Mungu wao kama na wao jumapili wanavyokuachia.

Achana na hizi roho za chuki na ubaguzi.
 
Msingi ya uwepo wa Taifa letu ni Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884 hadi 1885 ambapo wakoloni mabeberu wa Ulaya walijigawia vipande vya maeno Africa na kuwa makoloni yao. Baada ya kuondoka Tulibaki na mataifa huru na dini pia ikiwemo ile iliyoletwa na waarabu waliokuwa wanafanya biashara ya utumwa.
Sisi sio wachina na msingi wa uwepo wa taifa letu haufanani na ule wa China.

Soma historia za mataifa mbalimbali itakusaidia kukuza upeo wa kidunia.
 
Back
Top Bottom