Swali kwa Ayubu Rioba: Siku hizi sera ya Taifa inaruhusu taasisi za kidini kunufaika na fedha za walipa kodi kupitia TBC?

Swali kwa Ayubu Rioba: Siku hizi sera ya Taifa inaruhusu taasisi za kidini kunufaika na fedha za walipa kodi kupitia TBC?

Taarifa ya habari inayohusu tukio la kidini ni suala tofauti na tukio la kidini kuwe sehemu ya programu ya kituo cha luninga. Huko BBC, FRANCH 24 , na RT hawana kipindi cha kiongozi wa dini kuketi hapo na kuanza kuhubiri watu wasiojulikana ni kina nani na wako wapi. Hasa huu ndio ujinga unaopingwa hapa.
Kuna vipindi kibao ambavyo kila jumapili bbc inaonesha matokeo kanisani, edher rejea mazishi ya Prince Phillip mchana kutwa kanisani.

Ktk tukio la dini ambalo waziri mkuu anahudhuria sioni kosa kituo cha tv ku cover hilo tukio.
Kwanza ulinukuu katiba ukasema tbc waliendesha shughuli ya Dini.
Nikakuambia uendesha ni tafauti na kureport.

Jitahidiuwe open minded achana na chuki za kilokole Mama
 
Lugha ya Taifa ni mali ya Taifa.

Neno la Kiingereza au Kiarabu likikopwa na kutoholewa linaanguka katika lugha mpya.

Mfano neno shirt limekopwa na kutoholewa likawa shati.

Hili sio neno la Kiingereza tena.

Ni Kiswahili.

Ni vivyo hivyo kwa mavazi.
Tunazungumzia Asili ya hayo maneno kuwa yametoka kwenye lugha za mataifa mengine kabisa na mengine yamebaki na maaana ileile.
 
ila nyimbo zisizokuwa na maadil ni ruksa.kinachuupq faraja roho ni tenzi za rohoni.Dini ziwepo kutupa faraja
 
Maadili yapi?
Kama hazina maadili iambieni serikali izifungie
ila nyimbo zisizokuwa na maadil ni ruksa.kinachuupq faraja roho ni tenzi za rohoni.Dini ziwepo kutupa faraja
 
Usiwe kama ngumbaru kuhamishia mjadala kwenye imani fulani ili ionekane uzi ni kwa ajili ya kupinga dini fulani. Suala ni vyombo vya habari vya taifa visiwe jukwaa la mahubiri kwa dini YOYOTE.
Tatizo unaweza kuwa ni kijana mdogo usiyeielewa hii nchi vizuri. Ungeielewa ungejua kuwa hayo mawazo yako ni njozi zisizoweza kuja kutimizwa pengine wewe ukiwa hai.
 
Tuvumiliane: Kwa kutumia mwongozo gani?
Mwongozo uliopo sasa. Mawaidha ya kiislam kama yanakukwaza badilisha chanel mkuu. Hautapungikiwa chochote.

Mwongozo wa kuvumiliana na kuishi kama watanzania wenye dini, mila, malezi na mitazamo tofauti.
 
Sijwahi kusikia waislamu au Wakristo wakilalamika nyimbo za bongo fleva kupigwa TBC. Waislamu na Wakristo wote wanzipenda sana na huzitumia hata katika harusi zao, maulid, kipaimara, arobaini n.k
Wanajielewa sana ndio maana hawababaiki.
 
Taasisi za serikali kutumika kama majukwaa ya dini ni matumizi mabaya sana ya pesa za walipakodi. Wote tupinge huu utaratibu.
Kuna madaktari wanafanya kazi kwenye hospitali za mashirika ya dini je nao waondolewe?
 
Naona unachanganya mambo. Hebu nirekebishe hivi:

1. Chombo chao cha habaro: KIna nani? Katoliki wana Tumaini TV, KKKT wana Upendo TV, Waislamu wa Iman TV, Watanzania wote wana TBC. Kwa hiyo, masuala ya kisekta yanapaswa kuonyeshwa kwenye TV za kisekta, na masuala ya kitaifa kwenye TV ya kitaifa. Hiyo ndiyo maana ya civic space.

2. Utoaji wa huduma za jamii kama vile afya na elimu kupitia ushirika wa serikali na mashirika ya dini: Dini zinasajiliwa MOHA, shule zinasajiliwa Wizara ya Elimu, AZAKI zinasajiliwa Wizara ya Ustawi wa Jamii. Kwa hiyo, huduma za jamii kama vile afya na elimu sio kazi ya msingi ya taasisi za dini. Zinaweza kufutiwa leseni za shule na hospitali na kubakiza leseni ya MOHA.
Bado sijaona ubaya wa TV ya serikali kurusha vipindi vya dini tena kwa dakika chache za siku za ibada zao, kuna maeneo hizo TV za kisekta hazifiki, lakini vilevile kuna wakati hizo TV za kisekta zinarusha vipindi vya serikali kama hotuba za viongozi je nalo ni baya?
 
Nimekuwa nikipinga kuchanganya shughuli za kidini kwenye shughuli, mifumo na taasisi za serikali bila kujali mfalme ni nani.
Mkuu, kule Bungeni huwa wanafanya sala kila waanzapo session, na hata kwenye matukio makubwa ya kitaifa kama sherehe za maadhimisho mbalimbali huwa wanaalikwa viongozi wa dini zote kufanya sala, je ina maana kumtaja Mungu katika sehemu kama hizo ni matumizi mabaya ya nafasi/muda wa umma?
 
1. Usiwachukie Wakristo, wasaidie waondokane na huo unafiki unaouona kwa Wakristo.
2. Ila siamini kuwa wanafiki ni Wakristo tu, bali kwamba mnafiki anaweza kuwa muumini wa dini yoyote.
3. Sidhani kama wanaonuna kwa sasa ni Wakristo (ingawa inawezekana kwa baadhi ya wanaonuna kuwa Wakristo) na ndio 'wanaolazimisha tusiyaone mema anayotutendea mama'.
4. Siku nyingine ukichangia hoja jaribu kupima hoja yako na uwasilishaji wake.
Thanks
 
Sala ya bungeni huwa ni ya dini gani?
Mkuu, kule Bungeni huwa wanafanya sala kila waanzapo session, na hata kwenye matukio makubwa ya kitaifa kama sherehe za maadhimisho mbalimbali huwa wanaalikwa viongozi wa dini zote kufanya sala, je ina maana kumtaja Mungu katika sehemu kama hizo ni matumizi mabaya ya nafasi/muda wa umma?
 
Nimeyaona haya leo
Samahani... we mwenzetu ni mgeni nchi hii? Au unataka kutuambia umeanza kutazama tiibiisii wakati huu wa SSH? wakati wa Mwendazake, JK, BM havikuwepo hivyo vipindi au enzi za AHM na JKN hukuwahi kusikiliza RTD vitu kama "inueni mioyo... Quran tukufu?"
JE WADHANI KWANINI RAIS SSH KAJA NA SALAAM MPYA YA KITAIFA? JE WADHANI KWANINI HIYO SALAAM YAKE BAADHI WANAIPINGA? Je kwanini wapo viongozi bado wanatoa salaam za kidini kwenye mikutano au vikao vya serikali ilhali serikali haina dini?
 
View attachment 1792731
Dk. Ayub Chacha Rioba, Mkrugenzi Mtendaji wa TBC

Kwa kuzingatia matakwa ya katiba ya Tanzania, swali hapo juu linatokana na bonde la ufa lililopo kati ya yale ninayoyaona, na yale ninayoyatarajia kuhusiana na uendeshaji wa TBC.

Niliyoyaona TBC1

Tangu 15 Novemba 2020
nilipoikosoa TBC katika namna inavyotekeleza dhima yake ya kuelimisha umma juu ya COVID19 kwa kuzingatia misingi ya ukweli, ukweli wote na ukweli pekee, leo tena, tarehe 21 Mei 2021, nimeona matukio mawili yasiyo ya kawaida.
  1. Asubuhi kabla ya kipindi cha Bunge cha mswali na majibu TBC1 walirusha kipindi cha "Madrasa" kilichokuwa na ujumbe unaotembea kwa upande wa chini ukisomeka "Mashindano ya Kuhifadhi Kurani Tukufu kwa Waislamu Wanawake Yameandaliwa na Taasisi ya Kiislam ya African Relief Foundation." Kurani zilizokuwa zinasomwa zimeandikwa kwa Kiarabu.
  2. Mchana, mara tu baada ya matangazo ya Maadhimisho ya miaka 40 ya kuanzishwa kwa SADC, ambako Ayub Rioba alikuwa mwongozaji, kilifuata kipindi ncha swala ya Kiislamu. Swala ilianza kwa maelezo ya Kiarabu kwa dakika zipatazo tano.
Nafahamu pia kwamba, TBC1 imekuwa na kawaida ifuatayo:
  1. Kila alfajiri madhehebu ya dini tofauti hupewa muda wa kusoma sala ya asububi.
  2. Kila usiku wa kati, kabla ya saa sita, madhehebu ya dini tofauti hupewa muda wa kusoma sala ya kufunga siku.
  3. Kila Jumapili pia, madhehebu ya dini tofauti hupewa muda wa kusoma ibada za Jumapili.
Matarajio kwa mujibu wa Katiba

Katiba ya Tanzania, ibara ya 19(2) inasema kuwa, "shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi."

Na ibara ya 4(1) inasema kuwa shughuli zote za Mamlaka ya Nchi katika Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo vyenye mamlaka ya utendaji, mamlaka ya kutekeleza utoaji haki, na mamlaka ya kutunga sheria. Yaani, Serikali, Bunge, na Mahakama.

Hivyo, matarajio yangu ni kwamba, kwa kuwa TBC ni mali inayoendeshwa kwa kodi ya umma chini ya usimamizi wa serikali isiyofungamana na dini yoyote, basi yafuatayo yanapaswa kuonekana:

  1. Programu zenye sura ya kitaifa katika ngazi ya maudhui
  2. Programu zenye sura ya kitaifa katika ngazi ya lugha
Hii maana yake ni kwamba, yafuatayo hayapaswi kuonekana:
  1. Programu zenye sura ya kisekta katika ngazi ya maudhui
  2. Programu zenye sura ya kisekta katika ngazi ya lugha

Pia, nafahamu kuwa, dini nyingi tayari zinavyo vyombo vyake vya habari kwa ajili ya kuendesha shughuli zake. Kanisa Katoliki wana Tumaini TV, KKKT wana Upendo TV, Waislam wana Iman TV, Wapagani wa "Ramli TV," nk

Nakumbuka kuwa, kwa sehemu kubwa, sala nyingi za madhehebu ya KiIslamu zinatumia lugha ya Kiarabu, jambo ambalo linakiuka sera ya kujenga umoja wa kitaifa kwa kutumia lugha ya Taifa la Tanzania.

Hata ibada kadhaa na litania nyingi za Kikristo zinasomwa kwa lugha ya Kilatini ambayo sio lugha ya Taifa la Tanzania.

Nakumbuka kuna wakati Kardinali pengo alikuwa anaitwa na wazee wetu wa kule Mwenge Parokiani, Dar es Salaam, ili akawaendeshee ibada kwa lugha ya Kilatini, kama walivyokuwa wamezoea zamani, kabla Kanisa Katoliki halijatunga sera ya kuendesha ibada kwa Kiswahili na kimila.

Kwa hiyo, katika mazingira ya sasa, yafuatayo ni matarajio yangu:

  1. Kanisa Katoliki waendeshe programu zao za kisekta kupitia Tumaini TV,
  2. KKKT waendeshe programu zao za kisekta kupitia Upendo TV,
  3. Waislam waendeshe programu zao za kisekta kupitia Iman TV,
  4. Wapagani waendesha programu zao za kisekta kupitia "Ramli TV," nk
Uhalisia wa mambo

Pamoja na matarajio haya, uhalisia wa mambo ni kwamba, matakwa ya Katiba ya Tanzania kuhusu umuhimu na ulazima wa kutenganisha dini na dola hayajatimia kama ifyatavyo:

  1. Kanisa Katoliki wanaendesha programu zao za kisekta kupitia TBC1,
  2. KKKT wanaendesha programu zao za kisekta kupitia TBC1,
  3. Waislam wanaendesha programu zao za kisekta kupitia TBC1,
  4. Shughuli za Bunge zinaanza kwa kusoma dua kwa "Mola",
  5. Viapo vya watumishi wa umma vinamaliziwa kwa maneno "Ewe Mwenyezi Mungu Nisaidie," wakati Katiba ya nchi haitambui neno "Mungu."
Kama Katiba ya nchi inayakataza mambo haya, kwa nini tunayatenda, kama ambavyo mfano wa TBC1 leo umeonyesha?

Ni muhimu swali hili lijibiwe ili tujichunguze kama vyombo vya dola vinakweza maslahi ya vikundi na kutweza maslahi ya pamoja kitaifa, au vinginevyo.

Napendekeza kwamba ni kosa la kikatiba kutumia kodi ya raia asiye na dini kuhudumia taasisi za kidini. Ni kama ambavyo ni kosa kutumia kodi ya mtu asiye na chama cha siasa kutoa ruzuku kwa chama cha siasa. Kuna tatizo hapo.

Mapendekezo kuhusu mtazamo wa kisera

Nakumbusha kwamba, kote duniani, sera za kutenganisha dini na dola hugawanyika katika sehemu mbili:

  1. Sera zinazofuata mtindo wa Kimarekani.
  2. Sera zinazofuata mtindo wa KIjerumani.
Sera zinazofuata mtindo wa Kimarekani. Hapa, serikali huyapiga kisogo masuala yote ya dini, kiasi kwamba hakuna senti ya mlipa kodi inatumika kufadhili taasisi za kidini. Habari ya sijuo airtime kwa programu za kidini, sijui kufungua bunge kwa dua, hakuna.

Sera zinazofuata mtindo wa KIjerumani. Hapa, serikali haiyapigi kisogo masuala yote ya dini, kwani kuna senti fulani ya mlipa kodi inatumika kufadhili taasisi za kidini. Kwa mfano, huko Ujerumani, mfumo wa "TRA" yao unatumika kukusanya sadaka kutoka kwa waumini ambao ni waajiriwa, halafu sadaka hiyo inakabidhiwa kwa makanisa yaliyosajili waumini wao. Lakini, mfumo huu unabagua baadhi ya madhehebu ya kidini.

Hivyo basi, kwa kuwa Sera zinazotenganisha dini na dola kwa kufuata mtindo wa Kijerumani zina ubaguzi; na kwa kuwa sera zinazotenganisha dini na dola kwa kufuata mtindo wa Kimarekani hazina ubaguzi, napendekeza yafuatayo:

  1. Kwamba, programu zote za kidini, ambazo kwa sababu hiyo ni programu za kisekta ziondolewe katika TBC;
  2. Kwamba, programu zote za kidini, ambazo kwa sababu hiyo ni programu za kisekta ziendeshwe kupitia vituo binafsi vya madhehebu ya kidini;
  3. Kwamba, TBC ijielekeze katika programu zenye kujenga umoja wa kitaifa kwa kueneza lugha ya Taifa, na sio lugha nyinginezo;
  4. Kwamba, utaratibu wa kusoma dua mwanzoni mwa shughuli za Bunge ufutwe.
  5. Kwamba, Bunge litunge sheria inayotoa mwongozo rasmi kuhusu sera ya kutenganisha dini na dola hapa nchini Tanzania. Yaweza kuitwa "The Separation of Religion and State Act of 2021."
Pingamizi tarajiwa na majibu yake

Kuna pingamizi moja naona laweza kuibuka dhidi ya hoja yangu hapo juu. Linahusu tafsiri potofu ya tunu ya uvumilivu. Kwa hiyo nalijibu mapema kabla halijaibuka.

Fikiria kwamba, kuna mtu A anayemaini kuwa kitendo X ni haramu kidini, na hivyo kuamini kuwa kitendo hiki kinapaswa kupingwa.

Lakini, kwa mujibu wa tunu ya uvumilivu, mtu A anatakiwa kuamini kwamba ni sahihi kujizuia kupinga kitendo X, endapo kitafanywa na mtu baki B, kwa sababu kitendi hicho ni miongoni mwa matendo yanayopaswa kuvumiliwa na wanajamii.

Kwa hiyo, uamuzi wa mtu A kuvumilia kitendo cha mtu B unaonekana kumaanisha kwamba, mtu A anakubali imani kwamba “X ni kitendo kinachopaswa kupingwa” na anakubali imani kwamba “X ni kitendo kisichopaswa kupingwa,” ambazo ni imani mbili zinazopingana kimantiki.

Hata hivyo, kama tunu ya uvumilivu ikitafsiriwa vizuri haitaonekana kuwa na mkanganyiko huu wa kimantiki. Kwa mujibu wa tafsiri sahihi ya tunu ya uvumilivu, kukubalika na kukataliwa kwa kitendo X kunategemea mazingira ya kitendo hicho.

Yaani, uvumilivu wa mtu A kuhusu imani X, katika mazingira M, haumaanishi kwamba mtu A anapaswa kuonyesha uvumilivu kuhusu imani X, katika kila mazingira mbali na mazingira M.

Ndio kusema kwamba, kitendo X sio haramu kila wakati, kila mahali na kwa kila mtendaji. Yaani, wema wa kitendo X, au ubaya wake, unategenea mazingira ambako kitendi hicho kitafanyika.

Kwa hiyo, tafsiri sahihi ya tunu ya uvumilivu iko hivi: fikiria kwamba kuna mtu A anayemaini kuwa kitendo X ni haramu kidini, na hivyo kuamini kuwa kitendo hiki kinapaswa kupingwa katika mazingira M.

Lakini, kwa mujibu wa tunu ya uvumilivu, mtu A anatakiwa kuamini kwamba ni sahihi kujizuia kupinga kitendo X, endapo kitafanywa na mtu baki B, kwa sababu kitendi hicho ni miongoni mwa matendo yanayopaswa kuvumiliwa katika mazingira N.

Kwa hiyo, uamuzi wa mtu A kuvumilia kitendo cha mtu B unamaanisha kwamba, mtu A anakubali imani kwamba “X ni kitendo kinachopaswa kupingwa” katika mazingira M na anakubali imani kwamba “X ni kitendo kisichopaswa kupingwa,” katika mazingira N.

Ukitumia somo hili katika mjadala wa sasa, maana yake ni hii: “X ni kitendo kinachopaswa kupingwa” katika mazingira M na anakubali imani kwamba “X ni kitendo kisichopaswa kupingwa,” katika mazingira N, ambapo:

  • X ni kitendo cha kuendesha programu za kisekta katika TV
  • M ni mazingira yanayohusisha TV ya Taifa TBC
  • N ni mazingira yanayohusisha TV ya taasisi ya kidini kama vile Tumaini TV, Iman TV, Upendo TV, nk.
  • Ambapo, mazingira M na mazingira N yote yanapatikana ndani ya nchi moja ya Tanzania.
Huu ndio uvumilivu tuliofundishwa tangu shule ya chekechea mpaka chuo kikuu, na sio vinginevyo.

Katika Taifa moja, lenye mseto wa kidini, lazima kuwepo na sehemu za umma mpana ambako programu za kisekta hazikanyagi. Maeneo hayo ni pamoja na:

  • Vyombo vya habari vya Taifa (Hapa, lugha ya Taifa ni alama na nyenzio ya kujenga Utaifa)
  • Shule za Taifa (Hapa sare ni alama na nyenzio ya kujenga Utaifa)
  • Vyuo vya Taifa (Hapa mtaala mmoja ni alama na nyenzio ya kujenga Utaifa)
  • Vituo vya usafiri wa umma (Hapa vituo vya mabasi ni mfano wa uwepo wa maslahi ya pamoja Kitaifa)
  • Maktaba za Taifa Hapa vitabu mmoja ni mfano wa uwepo wa maslahi ya pamoja Kitaifa)
  • Barabara za Taifa (Hapa barabara ni mfano wa uwepo wa maslahi ya pamoja Kitaifa)
  • Na kadhalika
Katika maeneo haya ni marufu kuendesha mihadhara ya kidini kama ambavyo tumekuwa tunashuhudia tangu DG wa TISS aliyepita na aliyekuwa na mrengo wa kilokole, alipopewa mamlaka ya kuongoza TISS. Tujisahihishe kuanzia leo.
maelezo meengi kisa inakuuma kwa maudhui ya kiislam kutumia siku ya ijumaa.mbona hupingi wakristo kutumia siku ya jumaa pili? acha chuki za hovyo hizo.
vile vile mbona huja hoji kwani ccm wanatumia TBC katika mambo yao? chukulia mfano kipindi cha kampeni kila sehemu mwenda zake alipokuwa ccm walirusha live, na hata sehemu akihutubia njiani nao walikuwa wanarusha live hizo ni kampeni za chama kimoja mbona hukuhoji hilo?
Hata jana tu katibu wa ccm na sekretariet yake walivyopokelewa hapo Lumumba TBC walirusha live.mbona husemi kwamba ccm inabidi watumie tv yao ya channel ten.Acha chuki ndugu kazi iendelee
 
MPUMBAF MJINGA MDINI
Kawaida yenu tunaijua mkisha ona Nchi inaongozwa na WAISLAM mtaanza kuhoji kila aina ya ujinga Madhebu za Kikristo kila siku zitatoa MATAMKO mkitawa na Wagalatia wenzenu hata wakivuruga Nchi namna gani mnaufyata kimyaaa
Tumesha wazioe Waatoliki mnataka Nchi iwe ktk mikono yenu tu pumbaf zenu!
mwendazake mkatoliki mwenzao kila akienda kanisani TBC ilirusha live mbona hawakusema?
 
1. Nilichokisema mimi ni kwamba dini/imani ni sehemu ya utamaduni wa watu/walipakodi.
2. Kama kipindi kinachorushwa kinahusu dini/imani (sehemu ya utamaduni wa watu), kama kinavyoweza kuhusu uchumi, siasa na jamii, kwa kuzingatia taaluma ya uhandishi wa habari kwa namna ambayo haivunji maadili au sheria za nchi,
3. Na kwa vile baadhi ya walipakodi ni waumini pia katika hiyo dini/imani,
4(i) Basi, hakiwezi kukiuka utaratibu wa kawaida wa kurusha vipindi vya TV au radio na
(ii) hivyo (kwa maoni yangu) hakuna utata wowote katika hili.
5. Labada wewe mwenyewe uonyeshe urushaji wa hivyo vipindi vinavyosemwa ulikuwa na utata gani au ulikiuka utaratibu gani wa urushaji wa vipindi.
6. Kama urushaji wa hivyo vipindi una tatizo, basi tujadili hilo tatizo kuliko kujadili jambo la jumla hivyo.
Naona hujaelewa wazo langu. Basi twende kwa mtindo wa point counter point namna hii:

1. Nilichokisema mimi ni kwamba dini/imani ni sehemu ya utamaduni wa watu/walipakodi.

Jibu: neno dini lina maana nyingi: Kuna dini ambayo ni sehemu ya utamadni wa Kitaifa, dini ambayo ni sehemu ya utamadni wa kikabila, dini ambayo ni sehemu ya utamadni wa Wakristo, dini ambayo ni sehemu ya utamadni wa Waislamu, dini ambayo ni sehemu ya utamadni waWahindu, dini ambayo ni sehemu ya utamadni wa Wabuda, nk. Unaongelea dini gani na utamaduni gani?

2. Kama kipindi kinachorushwa kinahusu dini/imani (sehemu ya utamaduni wa watu), kama kinavyoweza (kurushwa kikiwa na maudhui) kuhusu uchumi, siasa na jamii, kwa kuzingatia taaluma ya uhandishi wa habari kwa namna ambayo haivunji maadili au sheria za nchi,

Jibu: Dokezo kuu la hoja inayojadiliwa hapa linaanzia kwenye ibara ya 4(1) na 19(2) za Katiba ya Tanzania (1977). Ibara hizi haziongelei uchumi, siasa wala jamii. Zinaongelea kutenganisha shughuliza serikali na shuguli za dini. Hiyo ndiyo fokasi ya hoja.

3. Na kwa vile baadhi ya walipakodi ni waumini pia katika hiyo dini/imani,

JIbu: TBC inatumia kodi ya walipa kodi wote, wakiwemo watu wasio na dini. Haitumii kodi ya baadhi ya walipa kodi.

4(i) Basi, hakiwezi kukiuka utaratibu wa kawaida wa kurusha vipindi vya TV au radio na

Jibu: Hitimisho hilo halitokani na madokezo sahihi, kama nilivyoonyesha hapo juu, na kwa hiyo halina uhalali.

4(ii) hivyo (kwa maoni yangu) hakuna utata wowote katika hili.

Jibu: Hitimisho hilo halitokani na madokezo sahihi, kama nilivyoonyesha hapo juu, na kwa hiyo halina uhalali. Utata upo kama nilivyoonyesha hapo juu.

5. Labada wewe mwenyewe uonyeshe urushaji wa hivyo vipindi vinavyosemwa ulikuwa na utata gani au ulikiuka utaratibu gani wa urushaji wa vipindi.

Jibu: Bandiko langu limeonyesha vema utata. Linao muundo ufuatao: matarajio, uhalisia, ufa kati ya matarajio na uhalisia, mapendekezo ya kuziba ufa, na majibu ya pingamizi tarajiwa. Soma kwa kutulia

6. Kama urushaji wa hivyo vipindi una tatizo, basi tujadili hilo tatizo kuliko kujadili jambo la jumla hivyo.

Jibu: Tatizo ni urushaji wa vipindi vya kidini kupitia TBC kuvunja kanuni ya 4(1) na 19(2) ya Katiba ya Tanzania (1977), na bandiko langu limeonyesha vizuri tatizo hili.
 
Back
Top Bottom