Kimsingi kila mtu ana hofu ya Maisha akikosa mipango ya kuishi. Lakini pia,hakuna mtu anataka kutulia na mtu ambae hana uhakika na maisha yake.
Nadhani mabinti wa umri huo wana options nyingi za wanaume sababu ndio prime moment kwao kuchaguliwa na wanaume. Sasa kiakili lazima watakuwa more vulnerable kushinda dada zao ambao wameshaanza kushuka kisoko na wanapungikiwa na options.
Wao kutaka pesa na mali ni tabia ya nje na wamejifunza kwasababu ya mfumo wa maisha ya sasa ya mitandao (tabia mbaya ya kukemewa kabisa) lakini sio tabia ya asili. Ukiwa na profile yako kama mwanaume ni rahisi sana kumshusha standards binti wa miaka 16 hadi 23 sababu hakuna analojua kuhusu maisha anafuata mikumbo ya waliomtangulia sokoni. Anachohitaji ni uhakika na akiupata kwako itakuwa ngumu kwake kuishawishi akili kuwa kuna sehemu bora ya kuwepo na mwanaume zaidi ya hapo mlipo.
Mwanamke wa miaka 29 tayari ameshaharibu mchezo wake na karata zimemuishia hana ya kucheza au ana michezo michache ya kucheza. Akileta uzembe tu ni kumpa mwanaume nafasi ya mchezo wa "Kwangu,kwangu,kwangu,stop,stop, naomba kadi special , kula mbili, kula joker,kadi mbili,nimemaliza"
Huyu lazima standards, ziwe juu. Sababu anacheza kwenye limits hana ujanja ameshakuwa looser. Sasa ukimuendea wa 29 unakwenda kukutana na standards without rewards. 29 atanipa nini muhimu alichonacho katika ulimwengu wa mwanamke.