Anachojali Mwenyezi Mungu ni kilicho rohoni mwa mtu na wakati mwingine kitu sahihi mbele ya Mwenyezi Mungu ni kile kinachoonekana siyo sahihi machoni petu na wakati mwingine kilichosahihi machoni petu siyo sahihi machoni pa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu hajali pia tofauti tulizonazo wanadamu maana pachoni pake tunazoziona kama tofauti yeye haoni tofauti na wakati mwingine tunachoona siyo tofauti yeye anaona ni tofauti. Hivyo, tunapoomba tunamwachia Mwenyezi Mungu kuamua kwa namna anayoona inafaa na siyo lazima kwa namna tunayoona inafaa kwetu. Tuendelee kumwomba Mwenyezi Mungu kila siku au kila tunapoweza ili mapenzi yake (siyo yetu) yatimie.