Swali kwa Wanawake wa kileo: Nini kilichowatoa majumbani na kuanza kuingia mitaani na maofisini kutafuta hela?

Naendelea .....

Suala la haki sawa na majukumu ya viumne hivi viwili, ni suala lenye umri mkubwa sana, kwani kina Plato (Rejea kitabu chake kiitwacho "The Republica") na mwanafunzi wake Aristoto walilijadili pia, mwalimu akasema ya kuwa mwanaume na mwanamke wako sawa kwa sifa na majukumu, lakini mwanafunzi wake akampinga vikali juu ya nadharia yake hiyo mfu.

Naendelea kunukuu

Aristoto dhidi ya mwalimu wake Plato


"Mwanafunzi wa Plato, Aristole ni mwanafikra mwingine wa ulimwengu wa kale, ambaye maoni na mawazo yake tunayo. Ametoa maoni juu ya tofauti kati ya mwanamke na mwanaume na ameyapinga vikali maoni ya mwalimu wake. Anaamini kuwa mwanaume na mwanamke wanatofautiana sio kwa kiasi tu bali hata kwa sifa. Anasema kwamba jinsia hizi mbili zina vipaji vya aina tofauti na majukumu waliyopewa na sheria ya maumbile na haki walizopewa, vyote vinatofautiana sana. Kwa mujibu wa Aristole, kanuni zao za maadili pia zinatofautiana katika mambo mengi. Inawezekana kuwa sifa ya maadili ikawa bora kwa mwanaume lakini isiwe hivyo kwa mwanamke na kinyume chake. Katika ulimwengu wa kale maoni ya Plato yaliondolewa, yakachukuliwa ya Aristole. Wasomi waliofuatia walipendelea maoni ya Aristole kuliko ya Plato." (Mwisho wa kunukuu)
 
Haya sasa unasema wewe, nilikuuliza swali ambalo hukulijibu, nilikuuliza kusoma ni ibada au si ibada ? Nikaona ukaanza kuleta
Kusoma kupi una maanisha ?

Uchawi ?

Maneno ya Allah na Mtume ?

Au unakusudia kusoma nini ?
Sasa wewe unasemaje mufti.

Iko wapi dalili inayomkataza mwanamke kusomea udaktari ama urubani ?
Usiwe unarudia mambo ambayo yako wazi tayari, nani amesema uharamu utakuwa kwa mwingine kwa muda huo ?
Kwa hiyo unakubali kuwa kuharibika kwa baadhi ya wanawake wanaosomea udaktari hakufanyi kwa wengine iwe haramu kusomea kwa kuharibika kwa wachache hawa ?
 
Mwanachuoni wa usuli na Mufasiri, aitwae Muhammad al Amiinash Shanqiitwiy al Jakaniy (Allah amrahamu) ana maelezo mazuri sana katika kuelezea hiyo Kaida uliyo iweka hapa,
Hata huyu mwanawachuoni angekuwepo basi ningemhoji kama ambavyo nakuhoji wewe.

Sasa usikimbie maswali kwa kuweka kauli za ulamaa ambazo hazijajibu maswala yangu.
Madhara yanaanzia katika namna ya mazingira ya upatikanaji wa hizo Elimu
Kwa hiyo unataka kusema kuwa mazingira yakiwa mabaya ya kutafutia elimu mwanaume tu ndiye anayeruhusiwa kutafuta elimu hiyo ?

Hayo mazingira mabaya ni yapi ?
 
Kwa hiyo unataka kusema kuwa mazingira yakiwa mabaya ya kutafutia elimu mwanaume tu ndiye anayeruhusiwa kutafuta elimu hiyo ?

Hayo mazingira mabaya ni yapi ?
Naanzia hapa, unahoji kitoto sana. Nani amekwambia baya kwa mwanamke ni zuri kwa mwanaume ? Isipokuwa yale yaliyi bainishwa.

Unajua athari za mchanganyiko kati ya mwanamke na mwanaume ? Sasa kuweka wazi mambo yaliyo wazi ni matumizi mabaya ya akili.

Hata huyu mwanawachuoni angekuwepo basi ningemhoji kama ambavyo nakuhoji wewe.
Nacheka sana unapo jitutumua kwenye hakuna. Huna uwezo wa kuhoji mbele ya dalili na marejeo, tofautisha kati ya kuhoji na kuuliza maswali, Wanazuoni huulizwa maswali na hawahojiwi, na jifunze kuyaweka maneno mahala pake. Mtu huwezi kutumia hata tamko "kuhoji", utawezaje kuliweka hilo mahala pake.
Sasa usikimbie maswali kwa kuweka kauli za ulamaa ambazo hazijajibu maswala yangu.
Hakuna swali nililo kimbia kijana, unachotakiwa utulize akili na uongeze umakini.

Onyesha kauli gani niliyo iweka ya mwanachuoni, haijibu maswali yako.
 
Kusoma kupi una maanisha ?

Uchawi ?

Maneno ya Allah na Mtume ?

Au unakusudia kusoma nini ?
Ina maana hukujua unachokijibu huko awali ?

Uchawi uko wazi hali yake, sasa unapouliza kuhusu Uchawi nakushangaa, wakati hukmu ya uharamu wa kujifunza uchawi inajulikana.
Sasa wewe unasemaje mufti.
Una tatizo kubwa sana la kutotumia maneno mahala pake, na unatakiwa uwe makini katika hilo.

Nani muft hapa ?
Iko wapi dalili inayomkataza mwanamke kusomea udaktari ama urubani ?
Nilikuuliza unionyeshe haja ya mwanamke kusomea urubani, hukuonyesha hili. Je asiposoma urubani ndege hazitarushwa au asiposomea utabibu watu hawatatibiwa ?
Kwa hiyo unakubali kuwa kuharibika kwa baadhi ya wanawake wanaosomea udaktari hakufanyi kwa wengine iwe haramu kusomea kwa kuharibika kwa wachache hawa ?
Nionyeshe haja ya huyo mwanamke kusoma hiyo fani ya udaktari.

Imaam Ibn Baz (Allah amrahamu) aliwahi kuulizwa swali kunako binti kwenda kusoma katika maskuli, muulizaji alikuwa ni wa kutoka nchi ambazo haziendeshwi kiislamu (Kama sijakosea). Imaam akamjibu kwa kumwambia yafuatayo au kama alivyojibu.

Akasema : "Kama kuna shule ambayo hairuhusu michanganyiko baina ya watoto wa kiume na watoto wa kike, inaruhusu stara ya kisheria" mpeleke mwanao akasome.

Sasa nionyeshe katika nchi yetu hii ni wapi mazingira hayo yapo ?

Lakini, imaam Ibn al Qiyyim al Jawziyah, katika chake (Jina kidogo limenitoka, nikilikumbuka kwa ukamilifu wake nitaweka hapa) akasema Shaykh, miongoni mwa sababu zinazo leta mabalaa na wabaa ni kuruhusu michanganyiko ya jinsia mbili tofauti na hili halina shaka ndani yake, na mwenye kupinga hili atakuwa hajui au mpotoshaji mwenye kufata matamanio ya nafsi yake.

Sasa huwezi kubishana na Elimu na haki kijana.
 
hakuna namna ya kuzuia wanawake ila ukweli ni kwamba kwenye kazi za kutumia akili kubwa wengi hawawezi wanategemewa kubebwa
 
Nilikuuliza unionyeshe haja ya mwanamke kusomea urubani, hukuonyesha hili. Je asiposoma urubani ndege hazitarushwa au asiposomea utabibu watu hawatatibiwa ?
Kwa hiyo hii ndo hoja ya kuwa haifai mwanamke kusomea hizo fani kweli ?

Kwa hiyo kuendelea kwa jambo fulani bila uwepo wa mwanamke ni dalili kuwa jambo hilo mwanamke haifai kulifanya ni haramu ati kwa kuwa hata bila yeye linafanyika ?

Huu msingi umeutoa katika dalili gani ?

Yaani leo iwe ni haramu kwa mwanamke kuendesha gari ati kwa kuwa hata asipoendesha gari bado litazidi kuendeshwa tu ?

Kana kwamba mwanamke kila kazi atakayofanya aangalie kwamba bila yeye kazi itafanyika na kama itafanyika bila yeye basi iwe haramu kufanya ?

Yaani unataka kuharamisha mwanamke kufanya kazi kwa ajili ya mahitaji yake mwenyewe sio ?


Aliyekuambia kwamba mwanamke haruhusiwi kufanya kazi kwa maslahi yake binafsi na kwamba lazima iwe ya ummah peke yake nani ?

Nionyeshe haja ya huyo mwanamke kusoma hiyo fani ya udaktari.
Haja ipo kwa sababu..

1.kunawake zetu na mama zetu ambao kisheria wanatakiwa watibiwe na wanawake wenzao huko mahospitalini,kusoma wanawake udaktari kunasaidia kuwepesisha jambo hilo.ila kwa dharula ya uhaba wa wanawake ndo wanatibu wanaume.

Au unatakataa kuwa kwa mujibu wa sheria ya uislamu ipo haja ya mwanamke kutibiwa na mwanamke mwenzake ?

Sasa wewe ambae unakataa mwanamke kusoma katika mashule ya mchanganyiko kwa kukwepa munkari wa mchanganyiko baadae unaukaribisha munkari wa mwanamke huyo kufanyiwa matibabu na kuonekanwa uchi wake na mwanaume wa kando,hili kwako sawa tu huoni tatizo yaani.

Una mawazo mgando sana bwana.

Yaani unadhani kutokuwepo kwa madaktari wa kike ni jambo limeibuka tu,ni jambo lina sababu nyingi za huko nyuma.

Unapowazuia wanawake mia moja wasiende muhas kusomea udaktari kwa kigezo cha kuwa pale wanachanganyika wanawake na wanaume na hilo ni kosa maanna yake tunapoteza madakatari 100 wa kike ambao wangeweza kupunguza wimbi la wanawake kutibiwa na wanaume.

Sasa matokeo yake madaktari wa kike wanapungua na madaktari wa kiume wanazidi.hili linapelekea kutokea kwa munkari mwingine mkubwa zaidi ambao una madhara kuliko ule wa mchanganyiko wa vyuoni.

Munkari huo ni ule wa mke wako,mke wangu,mama yako,mama yangu kufunuliwa nguo na kuonwa tupu zake na daktari wa kiume ambaye ndo alisomea udaktari kwa sababu wale wanawake mliwakataza.

Hii sio sawa.

Wewe niambie sasa hii sawa kuepuka munkari mdogo na baadae kuzua munkari mkubwa huko mbeleni ?


Kama kuna shule ambayo hairuhusu michanganyiko baina ya watoto wa kiume na watoto wa kike, inaruhu
Sasa unadhani ukiweka kauli ya ibn baazi Allah amrehemu ndo itakuwa mwisho wangu wa kuhoji ?

Naendelea kuhoji kuwa kwa mujibu wa sheria ya dini ni mwanamke peke yake ndo anayekatazwa kuwa katika mchanganyiko na wanaume ama hata mwanaume anakatazwa kuchanganyika na wanawake ?
Sasa nionyeshe katika nchi yetu hii ni wapi mazingira hayo yapo ?
Kwa hiyo wanaume wanaruhusiwa kuchanganyika na wanawake ila wanawake tu ndo hawaruhusiwi kuchanganyika na wanaume ?

Kwani hapo tatizo ni uharamu wa elimu au tatizo ni uharamu wa mchanganyiko ?

Kama uharamu ni elimu je kwa mwanaume ni halali ?

Na kama uharamu ni mchangayiko je mchanganyiko huo kwa mwanaume ni halali ?
Kwenye hiyo michanganyiko mabalaa yanayokusudiwa si ni zinaa n.k.

Sasa hiyo zinaa anazidi mwanamke mwenyewe ama anazidi na mwanaume ambaye naye yupo katika mchanganyiko huo ?

Sasa kama mwanaume naye yupo mbona akatazwe mwanamke tu wakati mabalaa yanapatikana kwa kuwepo na mwanaume,mbona wanaume hawakatazwi ?

Wakati sheria ya kiislamu ikimkataza jambo mwanamke na mwanaume inamkataza.

Ikimuadhibu mwanamke na mwanaume ina muadhibu.


Sheria yenu hiyo ya kuwakataza wanawake tupu imetokea wapi ?
 
Naanzia hapa, unahoji kitoto sana. Nani amekwambia baya kwa mwanamke ni zuri kwa mwanaume ? Isipokuwa yale yaliyi bainishwa.
Kwa hiyo unakubali kuwa kama haifai mwanamke kusoma kwa zama hizi kutokana na mazingira basi na mwanaume pia haifai kusoma kwa sababu kama ni baya basi baya kwa wote ?
Unajua athari za mchanganyiko kati ya mwanamke na mwanaume ? Sasa kuweka wazi mambo yaliyo wazi ni matumizi mabaya ya akili.
Hizo athari si zinafanywa na wanawake na wanaume.sasa mbona akatazwe mwanamke tu wakati hizo athari zinatokea kwa kutekeleza wote wawili mwanamke na mwanaume.

Mfano kuzini atazini mwanamke na mwanaume.

Sasa mbona akatazwe mwanamke tu wakati na mwanaume nae anakumbwa na athari hizo ?

Au unataka kusema kuwa mwanaume hana dhima akizini sio ?
Okey.
Hakuna swali nililo kimbia kijana, unachotakiwa utulize akili na uongeze umakini.

Onyesha kauli gani niliyo iweka ya mwanachuoni, haijibu maswali yako.
Jibu nukta baada ys nukta comment ziko wazi huko nimeendelea kukuuliza.
 
Unajitutumua sana aisee ila ndo hivyo tu,mambo mazito haya.

Inataka ufahamu kuacha ushabiki na ufulani kasema.
 

Imam Malik aliombwa na Khalifa Abu Jaafar Al Mansuur aandike kitabu na kisha Khalifa akamuahidi atakifanya kitumike kwa Waislam wote wafuate mwenendo wa Imam Malik. Lakini Imam Maalik alimwambiaje?

Kuna watu wa sehemu fulani na fulani nao wana dalili zao ambazo ni madhubuti vilevile kuna mambo tumetofautiana nao. Kwa hiyo kuwalazimisha wafuate mwenendo wangu mimi ni kuwakosea heshima kwa sababu dalili zao wanazitoa kwenye quran na sunnah vilevile. Ndicho alichojibu Imam Malik.

Ajabu iliyoje kwako wewe? Msimamo wa mwana wa zuoni unayemfuata wewe ndiye unaouona madhubuti na ndiyo uliyosahihi kabisa ya wengine ni ukanjanja. Haitoshi unaiharamisha vilevile.

Na ajabu iliyoje unayosema mwana wa zuoni haojiwi? Ama ufahamu kwamba kuna swali linalobeba hoja? Kinachotakiwa ni nidhamu ya kuuliza ama ya kuhoji. Kwa sababu swali lililobeba hoja linahoji kwa sababu anayehoji naye ana uthibitisho wa kauli uliyoitoa kama muafaka kuhusu suala fulani.

Ama umesahau yule mama aliyemuuliza swali Khalifa Umar Ibn Al Khatwaab inakuaje anawapangia wanawake kiasi cha mahari ya kuolewa wao. Akatoa na aya kwenye Quran kuonyesha kuwa Mungu anasema wanawake ndiyo wenyewe wanaopanga mahari. Hili si swali peke yake bali ni swali lililobeba hoja. Kwa maana ni swali lililobeba uthibitisho wa kile kilichotolewa muafaka. Khalifa Umar Ibn Al Khatwaab baada ya kumsikiliza yule mama kwa swali lililo na hoja alijibu huyo mama yupo sahihi na mimi Umar nimekosea.

Muamala wa kusoma na mustakabali wa kuyaelekea mambo ya kielimu unayokwenda nao ni mwenendo wa baadhi ya waislamu watu wanaojiita Answar Sunnah na kwa jina jengine mnajiita Salafi. Mnasoma elimu ya mabadiliko ya ukawaida hamsomi elimu ya mabadiliko ya kiufahamu. Matokeo yake mnaitikadishwa kuwa msimamo wa mambo upo hivi tu na wengine wote mnawaharamisha. Hamuiendei elimu kwa kuielewa bali mnaiendea elimu kwa kukitetea kile mnachofundishwa.

Kuwa makini! Kuna hadithi Mtume swallallahu alayhi wa aalihi wasallam kaziweka wazi juu ya watu wenye mwenendo kama wa kwako, na Mtume kawazungumzia ni watu wenye muelekeo mbaya. Hizo dalili nakuona unazo. Kingine una kiburi, una majivuno. Nakusihi pamoja na kuisihi nafsi yangu tuwe makini.

Tumuombe Mungu atupatie elimu na atupatie ufahamu wa hiyo elimu. Nakutakia kheri.
 
Allah akubaarik ndugu.

Umeongea maneno mazima sana.

Umegusia mambo makubwa sana.

Na nilimuambia bwana zurri kuwa huo msimamo wake ndio ambao unawaponza masalafy wengi kukatana kila kukicha,magomvi hayaishi,kejeli wao kwa wao mpaka unashangaa hawa jamaa vipi hawa.

Leo hakuna salafy ambaye amesalimika na mwenzake,huyu atamsema tule,yule atamsema yule mwingine na mwingine atamsema mwingine basi tafrani tupu kwa hawa ndgu.

Wanaziendea hadithi pasi na ufahamu,kuharibu kwaao ni kukubwa sana kuliko kutengeneza.
 
Allah akubariki nawe pia ndugu yangu.

Akuzidishie elimu, akuzidishie hekima, akuzidishie kheri nyingi zaidi.

Ulichikiandika kipo sahihi akhy. Kwa mwenye kutafakari pengine kwake ungekuwa ni mwito wa kutafakari.

Sheikh wangu aliniambia mwenye elimu inabidi aishi kama elimu yenyewe kwa maana matunda ya elimu, ni kama samaki ndani ya maji. Uhai wake ndipo ulipo na mwenye elimu uhai wake ni elimu. Maana elimu ni kama Jua linaangaza na dunia nzima inanufaika kutokana na mwanga wake. Lakini jua halinufaiki na dunia. Katika suala la elimu Mtume swallallahu alayhi wasallam alikuwa ni mpole, mnyenyekevu na alikuwa na huruma sana.

Mtume hakuwa ni mwenye kumlaani mtu, hakuwa mwenye kujikweza kujionyesha kuwa ana elimu kuliko waliyomzunguka na alijadiliana na kuamiliana na watu wa aina tofauti kwa lugha ya mahaba! Hakuwa na chuki. Aliwaelimisha watu na si kuwakosoa. Alikuwa anafundisha.

Kuna siku aalim wa Sheikh wangua liniambia kila kitu kina miiko yake na kina taratibu zake za kuziendea. Elimu nayo inataratibu zake na miiko yake; mfano ni Imam Shafii R.A alivopeteza uwezo wake wa hifdhi akaenda kwa mwalimu wake Imam Maalik R.A na kumpa hizo habaria. Mwalimu wake akamwambia elimu ni nuru itokayo kwa Allah, macho nayo yana nuru itokayo kwa Allah. Ukitizama mambo ya ajabu ile nuru Mungu anaiondoa machoni. Matokeo yake nuru itokayo kwa Allah ambayo ni elimu utashindwa kuisoma.

Akaniambia elimu haipo kwenye vitabu bali imo vifuani mwa watu. Ukikosa radhi ya mwalimu wako unakosa baraka. Utapata elimu ambayo haina baraka na mwisho wa siku utaharibu mambo. Akanisihi tena kuwa makini na kuwasema sema wana wa zuoni kwa ubaya kwamba yule ana nini!? Yule hana elimu ama kumsema mtu wa namna yoyote kwa sababu kuna wengine ni vipenzi vya Mungu.

Na Mungu anatangaza yeyote atakayemghasi kipenzi chake basi ametangaza vita na Mungu. Akaniambia hata kama ulikuwa na elimu na ni mfanya ibada ibada yako inaweza ikawa haina twaaa. Usidharau watu hii dini ni ya Mungu basi kuwa na heshima na viumbe vyake.

Kuna Sheikh mmoja anaitwa Shaji (jina la pili limenitoka). Sheikh akaniambia alikuwa anamzungumzia vibaya Imam Ghazali mfano wa umma wa leo tunavyozungumziana kwa ubaya, kutiana ukaafir na mambo mengine kisa haendani na madhehebu yako. Sheik akaniambia Shaji alivyolala akamuota Mtume swallallahu alayhi wa aalihi wa sallam akiwa amesimama na sahaba yake Umar lakini pembeni yupo Imam Ghazali.

Imam Ghazali akamshtakia Mtume kuwa Sheikh Shaji anamtukana na yeye hajui amefanya nini?! Mtume akamuamrisha Umar amtie bakora. Shaji kushtuka usingizini maumivu ya bakora anayo na alama pia. Shaji akatoa na kitabu akituambia tusitukanane, tusizungumziane kwa ubaya haujui unayemzungumzia kwa ubaya ana daraja gani kwa Mungu.

Sisemi niliusiwa ni ya sahihi zaidi ila katika haya niliyousiwa ndugu zetu Salafi sinalengo baya kwa hili nitakaloliandika na wala sina maana mimi ni bora na Mungu aniepishe na hiyo royo ya kujiona bora ila ninachokiona kwa Salafi hayo niliyousiwa ndiyo nisiyafanye wao wanayafanya na niliyousiwa niyafanye wao hawayafanyi. Wanakosa adabu ya elimu. Ndiyo maana kwao ni rahisi kuntamkia mtu kwa ubaya mwisho wa siku wanavuruga watu na wana vurugana wenyewe kwa wenyewe.
 
Wasaudia si dini ya haki inawaruhusu au?[emoji846][emoji1787][emoji847]
 
Umeandika maneno mazima sana ambayo kila mtu akiyasoma atapata faida na kuzidiwa na ubainifu.

Hata kama mtu unaitakidi sio muislamu basi haifai kumtukana wala kumlaani.

Tukirejjea kile kisa cha bwana mtume wa Allah alipokuwa na bibi aisha wakapita mayahudi kama sikosei wakamsalimia kwa ubaya, mtume akajibu kwa maneno mafupi tu "na kwenu pia "

mama aishha akapandisha jazba akawajibu "na nyie pia laana za allah ziwe juu yenu"

Mtume akamkataza mama aisha,mama aisha akamshangaa mtume mbona wanikataza wakati wao wamekuombea mabaya ?

Mtume akamuambia kwani huoni na mimi nilivyowajibu ?

Mtume lau angekuwa mtu wa kulaani laani ovyo basi angempongeza mama aisha,lakini mtume akamkataza asiwalaani wale watu badala yake angemaliza tu kwa kujibu kama alivyojibu mtume wa Allah.

Ijapokuwa kumkataza mtume mama aisha asiwalaani haina maana kuwa Mtume anakubali kuwa wale wapo katika uongofu ambao mtume kaja.

Nabii mussa aliambiwa na Allah akamlinganie firauni kwa kauli za kistaarabu pengine atawaidhika.

Leo hii asiyekuwa firauni anakejeliwa na kubezwa kana kwamba kamzidi firauni kwa mijidhambi yake kumbe tatizo huyo mtu anasherehekea maulidi au anafuata madhehebu fulani ambayo sio ya mbezaji au anakataa rai za kina albaniy na akina ashinqitwiy..

Allah atufe salama kwa kweli.
 
Masalafi wengi sana wanaamini kuwa chao ndo sahihi na kufuata kisichokuwa chao basi ni dhwalaala.

Kuna mwalimu wetu mmoja yeye hakubaliani na mambo ya maulidi na dua za msikitini,lakini anavyoyazungumzia kwa utaratibu na ustaarabu mpaka wengine wanamsema kuwa anatetea watu wa bidaa,lakini maalim yeye harudi nyuma anasema kuwa wale ni watu wana maoni yao ijapokuwa kwa upande wangu naona sio sahihi.

Hawa ndio watu wa kusoma kwao ni watu wenye busara na hekima na uvumilivu.
 
Kwa hiyo hii ndo hoja ya kuwa haifai mwanamke kusomea hizo fani kweli ?

Kwa hiyo kuendelea kwa jambo fulani bila uwepo wa mwanamke ni dalili kuwa jambo hilo mwanamke haifai kulifanya ni haramu ati kwa kuwa hata bila yeye linafanyika ?
Sasa niambie ulazima wa jambo ambalo linakiuka asili ya mwanamke ni upi ?

Aya inasema wanawake walazimiane na majumba yao. Ikitokea wakatoka basi watoke kwa haja, hii haja inakuwa katika mlango wa dharura, na dharura hukadiriwa kwa makadiriyo yake. Kwahiyo unapo uliza swali la hovyo kama hili ulitakiwa utoe ushahidi wa kuruhusu jambo hili, toka katika hadithi au Qur'aan. Sasa Uislamu wetu umeruhusu watu kuhoji ila umekataza kuhoji ujinga, na tukapigiwa mfano kwa Wana wa Israeli walivyo potea kwa kuhoji hoji kwao ujinga.

Kadhalika aya ikawazindua kwa kuwaambia tabia ya kutoka toka kwa kujifaragua ni tabia ya Wanawake wa Jahiliya.

Sasa nasubiri unipe haja ya Mwanamke kutoka kwenda kusoma Udaktari na unithibitishie ya kuwa hawa waliopo hawatoshelezi wengine ?
Huu msingi umeutoa katika dalili gani ?
Msingi ni aya ya 33 katika sura ya 33.
Yaani leo iwe ni haramu kwa mwanamke kuendesha gari ati kwa kuwa hata asipoendesha gari bado litazidi kuendeshwa tu ?
Maana ya dharura ni hii mzee. Au wewe una mafhumu gani juu ya dharura ?
 
Kijana ngoja hili nilihitimishe kwa mtindo huu, maana huna hoja. Kuna nukta zifuatazo :

1. Mwanamke anaruhusiwa kufanya kazi penye haja, na ikitokea hiyo haja huwa ina kadiriwa kwa makadirio yake. Yaani stara,na pasiwe na mchanganyiko.

2. Maslahi na ufisadi,ufisadi ukiwa mwingi jambo kuliko maslahi, jambo hilo halifai kufanyika.

3. Ulamaa wengine wakafika mbali wakasema hivi, kwa mtu amabaye ni dharura kufanya jambo fulani, ukatokea mbadala wa kuondoa hiyo dharura, basi hapo hapo anatakiwa jambo hilo aliache. Mathalani, ikatokea kuna binti, nyumbani kwao hakuna wa kuleta rizki ila yeye, ataruhusiwa kuafuta rizki kwa kuzingatia masharti yale, ikaja kutokea mletaji rizki akapatikana hapo kwao, basi yeye hiyo dharura huondoka, na atatakiea kuacha hiyo kazi na kurudi nyumbani.

4. Athari ya mchanganyiko kila mwenye akili timamu anaijua isipokuwa yule mwenye kujitia upofu. Haja ya mwanamke kusoma hizo fani hakuna. Sababu waliopo wanatosheleza wasio kuwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…