Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele ‘Maslahi ya Taifa’?

Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele ‘Maslahi ya Taifa’?

Ukweli ni function ya mambo kadhaa: mazingira/wakati unamotakwa kusemwa huo ukweli,hadhira na matokeo tarajiwa.Hivi hivi sio ukweli tu hata kinyume cha ukweli (uongo mtakatifu/uongo chanya) nao huzingatia mambo hayo.

Yesu Kristu,alipata mara kadhaa kufundisha kwa vitendo juu ya jambo hilo.Aliponya watu wengi sana lakini wengine aliwakataza wasiseme nani kawaponya.Kubwa zaidi,aliwazuia akina Petro na wenzie Yohana na Endrea(watoto Wa Zebedayo) wasiende kueleza jinsi walivyofika Mbinguni na kujionea kulivyo kuzuri ajabu.

Ukweli lazima usemwe kutegemea au kuangalia kwanza mpokeaji Wa huo ukweli husika.Kwa mfano mwanao Wa darasa la Pili akikuuliza hivi: ..." baba hivi wewe baba na mama mlinitoa wapi? Au...hivi baba: ..."mama alinizaa vipi"? Sasa ukweli unaujua jinsi Huyo mtoto alivyopatikana au jinsi mkeo alivyomzaa Huyo mwanenu.Je,utaueleza huo ukweli? Utaeleza process nzima jinsi mtoto wenu alivyopatikana?

Pili: sio lazima ukweli usemwe tu na wewe uliyeulizwa juu ya ukweli wenyewe? Kwa mfano,binti yako akikuuliza hivi: "baba mwalimu leo kanitukana eti... "angalia sura kama k.o.n.d.o.m.u.Hivi baba k.o.ndo.m.u ndio kitu gani na inafafanaje au huyo mtu k.o.n.d.o.m.u anaishi wapi?" Hivi utaweza kueleza ukweli juu ya hicho ulichoulizwa? Au hutamjibu kuwa ..." mwanangu hebu msubirie mamako au Dadako mkubwa ndio niliwasikia wanamuongelea Siku moja Huyo "MTU" ?Yumkini,mama au dada mkubwa watamueleza huyo mwanao kuwa "MTU" tusi la "mtu" uliyetukanwa ni hivi na hivi...tena kwa kuambatanisha na tahadhari kadhaa.

Ukweli lazima uzingatie matokeo: hivi unaweza akikuijia mtu amebeba AK 47 na amevaa Mask mwili mzima halafu akamuulizia Nyani Ngabu na ambaye unajua kwa hakika yuko wapi; hivi utasema ukweli aliko Nyani Ngabu?

Ukweli lazima uzingatie mazingira na uwezo Wa mtu wa kuuwasilisha huo ukweli: mfano munauguza mgonjwa yu taabani.Na mumeambiwa na Daktari kuwa sio rahisi mgonjwa wenu kupona.Je,wewe ukimpelekea mgonjwa chakula utafika tu na kumropekea kwamba ..."hutapona" ? Au Utamtafuta Padri au utasubiria Daktari mwenyewe tena mwenye taaluma ya counselling ili amueleze ukweli huo mgonjwa wako?

Kwa hiyo,ukweli una pillars zake na sio kwamba ni kitu cha kuropokwa tu.
 
Mkuu ni bora ukae kimya kama hutaki kuusema ukweli kuliko kutetea uongo hata kama ni kwa maslahi ya raisi, hakuna maslahi ya taifa katika kusema uongo hebu nipe mfano mmoja tu wenye maslahi kwa taifa kwa kusema uongo

Uongo na ukweli vyote vipo kuponya na kuzuia.Kinachoamua kipi kisemwe wapi,wakati gani na kwa sababu gani ni matokeo unayoyakusudia,hadhira itakayopokea Huo ukweli,Fanani wa kutoa huo ukweli au Uongo. Tujifunze mambo haya vizuri.
 
Pascal mkubwa mwenyewe ameonyesha udhaifu wake kwamba ukiwa jeuri mdhulumaji mwenye kiherehere ndio anawateua kuongoza wanyonge matokeo yake kila mtu anataka kuteuliwa so haki haitendeki tu kwa sababu ya kumfurahisha mtu yule., Awe msikivu ataepuka mengi hao anaowaamini ndio adui namba moja asikilize upinzani upo kumsaidia kwa sababu ya manufaa ya Taifa. Historia itamhukumu vibaya sana
 
Paskali.

Inawezekana kweli Magufuli anapenda challenge, naambiwa hata hiyo Ph.D aliyonayo aliichukua kwa sababu alikuwa challenged na mfanyakazi mwenzake serikalini kwamba yeye Magufuli hana Ph.D, akasoma na kuipata (whether this is a juvenile reason or not is another matter entirely).

Ikiwa Magufuli anavituma vyombo vya dola kufanya kamata kamata za kizushi,hilo ni jambo baya sana. Anaitia nchi sumu ya chuki.Anakuwa mjinga ambaye anaweka sumu katika kisimaanachochota maji yeye mwenyewe.

Kwa jinsi ninavyomuona Mgufuli siwezi kushangaa nikiambiwa huu ndio ukweli.

Lakini pia, inawezekana Magufuli haagizi waziwazi kwamba mkamateni fulani, ila kauli zake mbovu anazotoa rejareja, kama kumwambia Spika "washughulikie hukosisi tutawashughulikia huku" zinachangia. Teuzi za kuwateua watu vimbelembele nazo zitaonyesha walio vimbelembele "kuzawadiwa" kwa teuzi. Rais Tanzania ni mtumwenye nguvu sana, akisema kitu hata kwa mzaha tu, watu wanakichukulia serious, hivyokama hiindiyo sababu, yuko responsible kwa kauli zake.

Lakini pia, inawezekana kabisa vyombo vya dola vinajipendekeza tu na tuseme Magufuli hajaagiza chochote implicitly au explicitly.

Hata kama ni hivyo, Magufuli akiona vyombo vya dola vinavuka mpaka kwa kutaka kujipendekeza kwake, ana wajibu wa kuvikemea viache mtindohuo ama kwa kusemapublicly, amakwa kuwaambia ndani kwa ndani serikalinihuko.

Kuna hotuba moja alikuwa anatoa Mzee Jomo Kenyatta Kenya.Alikuwa ameenda kufungua hospitali pande za Magharibi.Muda huo Kenyatta ana mgogoro mkubwa na Oginga Odinga, baba yake Raila. Kenyatta alitukana matusi mabaya sana siku ile kwa sababu wafuasi wa Odinga walimvunjia heshima, akasema anaweza kumfunga Odinga, lakini anajua Odinga ni rafiki yake hivyo anamuheshimu, ila awakanye wafuasiwake.Kuna mtu mmoja kimbelembele aka shout kama kumchombeza Kenyatta kwamba "mfanyizie tu huyo".Kenyatta badala ya kumuendekeza yule kimbelembele, akamkaripia sana pale pale jukwaani akimwambia kwamba, Mimi Jomo Kenyatta najua nini cha kufanya, usione kwamba nimempaka Odinga Oginga hapa, ukajifanya unanijua sana na unaweza ku anticipate moves zangu. Na huyu Oginga ingawa nina mgogoro naye, lakini mgogoro wangu naye ni wa wazee na wewe kimbelembele tu kaa chini usikilize maneno ya wazee usitake kutoa hukumu. Mimi najua nitakachofanya.

Kwakweli hotuba ile ya Kenyatta ilikuwa na matusi mabaya sana. Lakini pia Kenyatta alikuwa anaonyesha bonafide "gangstar" yake kwamba hapangiwi na wafuasi wake ajenda, na hata kama ana mgogoro wa ngazi ya juu na viongoziwenzake wa kitaifa, watu vimbelembele tu hawawezi kumpangia cha kufanya.

Sikupenda matusi ya Kenyatta.Lakini nilipenda alivyomkaripiayule kimbelembele.

Magufuli kama ana vimbelembele wanaotaka kumpangia ajenda ambayo yeye mwenyewe hana, ana wajibu wa kuwakaripia hao vimbelembele.

Akishindwa kuwakaripia, tukisema kawatuma, hata kama hajawatuma, kuwaachia tu wafanye wanavyofanya itakuwa complicity ambayo kwa rais ni kama kawatuma tu ila anatafuta kitu kinachoitwa "plausible deniability".
 
tatizo la tanzania hakuna mazingira ya "national interest", mazingira ya national interest yanaandaliwa na serikali iliyo madarakani kwa kushirikisha upinzani kwenye maamuzi ya nchi na kutoa haki zote stahiki na kuelewa kuwa nchi ni ya wote wanaongoza na wapinzani.

kutumia nguvu na kutengua maagizo ya katiba kuminya haki ya upinzani haiwezi kujenga national interest, kunaweka mpasuko wa vuta nikuvute, na hapa ndipo tulipofika, ni kuvuna ulichokipanda
serikali ulojaa kiburi na ego wanaamini kuwa nguvu ndio zitajenga na wanaamini kuwadhibiti kutisha na kutesa upinzani ndio utatia adabu ili wanyamaze kwa kutii amri,katika mazingira haya hamna kujenga nchi ni kuimarisha mvutano na mpasuko tu
 
Mbona hii nchi inakuwa na watu wapumbavu hivi? Yaani wewe unatembea na mke wa mtu sirini huku unatamba mtaani kwamba hufanyi jambo hilo Leo katokea anaeijua hiyo siri na kuivujisha badala ya kujitathimi na kujirekebisha unaanzisha vitimbi vya kumtafuta alievujisha inamaana tabia yako chafu na huna mpango wa kuacha hivyo unasubir moto wa duniani na mbinguni
 
Sijasoma article yako, ila nimesoma kichwa cha habari na bila kupepesa macho ni kwamba raia wana haki ya kujulishwa kila kitu hasa lihusulo matumizi ya kodi zao.

Uzalendo sio kukubali kila kitu ambacho kinakuja kwa jina la development hata kama kinaleta maafa kwa nchi.
 
walishasema kazi yao kuuu ni kupingapinga tu basi lakini nafikiri kuna haja ya kujitafakari sio kila kitu kuropokaropoka kuna issues nyingine ni too classified sio lazima Uzi disclose for political gain hii issue ni national matter against our enemy na wanatushangaa baadhi yetu kuwa upande wao
Kwa mfano hii ya bombardier kushikiliwa kwa sababu ya deni. Hii pia ni classified information in your opinion? Ni kweli kwamba ukitafuta hukumu hiyo huwezi kuipata? Are you sure hukumu hii ni confidential??? This is really crazy..
 
Hebu tufafanulieni nyie ambao Lissu amewakera sana kusema tunadaiwa na ndege imezuiliwa. Hivi maslahi ya taifa katika suala hilo ni yapi??? Yaani Lissu angekaa kimya ili kulinda maslahi yapi ya taifa letu?
 
Ukweli ni nini?

Tuanzie hapo kwanza.

Mtu wa Australia anaponyoosha kidole juu kwake na kusema huku ni juu na mtu wa London anaponyoosha kidole juu kwake kusema huku ni juu, wananyoosha kidole juu kumoja? Wapi ni juu kweli, kwa mkazi wa Australia au wa London?

Sent from my Kimulimuli
 
Back
Top Bottom