SANCTUS ANACLETUS
JF-Expert Member
- Mar 5, 2016
- 3,338
- 4,676
Ukweli ni function ya mambo kadhaa: mazingira/wakati unamotakwa kusemwa huo ukweli,hadhira na matokeo tarajiwa.Hivi hivi sio ukweli tu hata kinyume cha ukweli (uongo mtakatifu/uongo chanya) nao huzingatia mambo hayo.
Yesu Kristu,alipata mara kadhaa kufundisha kwa vitendo juu ya jambo hilo.Aliponya watu wengi sana lakini wengine aliwakataza wasiseme nani kawaponya.Kubwa zaidi,aliwazuia akina Petro na wenzie Yohana na Endrea(watoto Wa Zebedayo) wasiende kueleza jinsi walivyofika Mbinguni na kujionea kulivyo kuzuri ajabu.
Ukweli lazima usemwe kutegemea au kuangalia kwanza mpokeaji Wa huo ukweli husika.Kwa mfano mwanao Wa darasa la Pili akikuuliza hivi: ..." baba hivi wewe baba na mama mlinitoa wapi? Au...hivi baba: ..."mama alinizaa vipi"? Sasa ukweli unaujua jinsi Huyo mtoto alivyopatikana au jinsi mkeo alivyomzaa Huyo mwanenu.Je,utaueleza huo ukweli? Utaeleza process nzima jinsi mtoto wenu alivyopatikana?
Pili: sio lazima ukweli usemwe tu na wewe uliyeulizwa juu ya ukweli wenyewe? Kwa mfano,binti yako akikuuliza hivi: "baba mwalimu leo kanitukana eti... "angalia sura kama k.o.n.d.o.m.u.Hivi baba k.o.ndo.m.u ndio kitu gani na inafafanaje au huyo mtu k.o.n.d.o.m.u anaishi wapi?" Hivi utaweza kueleza ukweli juu ya hicho ulichoulizwa? Au hutamjibu kuwa ..." mwanangu hebu msubirie mamako au Dadako mkubwa ndio niliwasikia wanamuongelea Siku moja Huyo "MTU" ?Yumkini,mama au dada mkubwa watamueleza huyo mwanao kuwa "MTU" tusi la "mtu" uliyetukanwa ni hivi na hivi...tena kwa kuambatanisha na tahadhari kadhaa.
Ukweli lazima uzingatie matokeo: hivi unaweza akikuijia mtu amebeba AK 47 na amevaa Mask mwili mzima halafu akamuulizia Nyani Ngabu na ambaye unajua kwa hakika yuko wapi; hivi utasema ukweli aliko Nyani Ngabu?
Ukweli lazima uzingatie mazingira na uwezo Wa mtu wa kuuwasilisha huo ukweli: mfano munauguza mgonjwa yu taabani.Na mumeambiwa na Daktari kuwa sio rahisi mgonjwa wenu kupona.Je,wewe ukimpelekea mgonjwa chakula utafika tu na kumropekea kwamba ..."hutapona" ? Au Utamtafuta Padri au utasubiria Daktari mwenyewe tena mwenye taaluma ya counselling ili amueleze ukweli huo mgonjwa wako?
Kwa hiyo,ukweli una pillars zake na sio kwamba ni kitu cha kuropokwa tu.