Wakuu,
Kikundi cha wanamgambo wa Kiislamu kinachohusiana na Al Qaeda, JNIM, kimedai kuhusika na shambulio dhidi ya kambi ya kijeshi katika jimbo la Loroum kaskazini mwa Burkina Faso, ambapo wamesema waliua wanajeshi 60.
Shambulio kubwa lilitokea katika mji wa Sole, huku shambulio jingine mashariki mwa jimbo la Gnagna likiwaangamiza wanamgambo 10 wa serikali (VDP).
Pia, kiongozi wa JNIM nchini Burkina, Ousmane Dicko, alionekana kwenye video akiwataka wakazi wa Djibo kuhama kwa usalama wao. Djibo ilishambuliwa Jumapili, ikiwa ni pamoja na kambi ya jeshi, kituo cha polisi na soko.
Mashuhuda walisema mamia ya wapiganaji walishambulia na kuua wanajeshi na raia. Vifaru vya kijeshi vilichukuliwa na miili ya wanajeshi iliteketezwa na milipuko. Video kwenye mitandao zilionyesha wapiganaji wa JNIM wakizunguka mji wa Diapaga, wakifyatua risasi, kuchoma maeneo na kuondoa bendera za serikali na Urusi.
=================================================
Al Qaeda affiliate JNIM has claimed responsibility for an attack targeting a military post in Burkina Faso's northern Loroum province in which the group said 60 soldiers were killed, the SITE Intelligence Group said on Tuesday.
The U.S.-based non-governmental organization, which tracks online activity of Islamist militants, said JNIM had posted messages on Monday and Tuesday in which it took credit for four assaults in Burkina Faso and Mali.
The attacks highlight the difficulties the three Sahel nations of Burkina Faso, Mali and Niger, ruled by military leaders, are facing in containing the insurgents. Burkina authorities have not commented on the latest attacks.
The most notable attack occurred in the Burkina town of Sole, where JNIM fighters raided the army military post and killed soldiers, SITE Intelligence said, without specifying on which day it took place.
Another Burkina attack killed 10 members of a pro-government militia known as VDP in eastern Gnagna province, SITE added.
Source: Reuters