KERO Taarifa Binafsi: Kampuni ya mkopo mtandaoni (online loan app) imenidhalilisha sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Unaonekana unafaham mengi sana, emb nijuze kuhusu ku root simu
 
Tuwe wakweli sisi watanzania hatuna hulka ya kulipa mikopo kwa wakati, mfano wewe hiyo 42,000 umeomba mkopo na kupewa siku hiyo hiyo, ukaondoa shida yako. Sasa ni kwa nini usilipe hiyo pesa ndani ya muda au hata Kabla ya siku 7 kwisha?? Mwisho kila ikifika mwisho wa mwaka jitahidi ku edit phone book [emoji428] yako ili ufute Namba ambazo hazina umuhimu kwako, afadhali ubaki na majina 50 ya muhimu kuliko 200 hewa.
 
Haya mtoa mada kakuelewa.

Vipi kwa upande wa Kampuni iyo kutuma izo SMS ni sawa?
 
Kwa 97% ukienda na huu ushahidi mahakamani unapotea.

Mkopo Fasta na Pesa M loan siyo kampuni ni products za kampuni. Ambazo wewe unazipata kama applications playstore.

Kampuni ina jina lake. Kama hiyo doc ya BOT ungekua nayo ningeisoma nikutajie kama hii kampuni ipo au haipo.

Waziaa JamiiForums wawe na app ya kukopesha iitwe JamiiPesa. So hautakuta jina la JamiiPesa BOT bali Jamiiforums. Pia wewe umekopeshwa online, mkataba ni zile yes ulizobonyeza muda unakopa.

Pia, kampuni mpya inaweza operate wakati inasubiri vibali. Kikubwa maombi yawe yalishafanywa.

So jiangalie
 
Zachini chini, wanapiga pesa ndefu kwenye kuwatisha watu kuwa watavujisha picha na video zao za uchi au ngono,..hivyo kuna watu wanalipa kila mwezi hata baada ya mkopo kuisha....
Toa evidence juu ya hii ishu.

Hebu fikiria kwa akili ya kawaida.

Mtu anayekopa 42,000 ana influence gani kwa jamii kiasi tukiona picha yake tushangae?

Unajua kama blackmailing ni kosa kisheria?
 
Wapeleke Mahakamani kama hakuna kipengele hicho
 
Kama changamoto ya Elfu 42 unashindwa itatua au walokuzunguka kukusaidia kuitatua basi achana na kuwaza mwanasheria
Amua moja kulipa au kuwarusha
 
Nilitumiwa na Sunloan kuwa rafiki yangu mmoja wa kike ni mdaiwa[emoji1787] nilipomuuliza akajibi simple tu kuwa matapeli hao
 
Kubonyeza YES ndiyo mkataba wa maandishi ambao BOT imeelekeza ?

Nini maana ya BOT kusema "mkopeshaji akupe nakala ya mkataba wa maandishi ubaki nayo"
 
Silipi jomba na hamna kitu watanifanya.

Kwanini wanitangaze wakati dead line ilikuwa bado haijafika
doctor unakalia mbususu unashindwa kusave chochote matokeo yake umegeika tapeli. Lipa pesa ya watu mzee ama waombe chawa wenzio humu kina lucas wakusaidie kufukia mashimo... Ila wambie kabisa umebadili jina umerudia lile jina la zaman ili wakutambue wakulipie
 
Kubonyeza YES ndiyo mkataba wa maandishi ambao BOT imeelekeza ?

Nini maana ya BOT kusema "mkopeshaji akupe nakala ya mkataba wa maandishi ubaki nayo"
Trust me Bro.

Kama ushahidi wako ni ule. Unaenda kupotea.

Notice BOT kaelekeza hivyo kwaajili ya Microfinance.

Digital Lending Platforms zina sera na sheria zake ambazo ni tofauti na microfinance.

Anyway, nishachangia sana huu uzi wako kwa ninachokijua.
Kama utanielewa au hautanielewa katika nilichosema hapo ni juu yako.
 
View attachment 2911035
benki kubwa wanaonya watu kila siku
Hiyo ni wazi,mahakamani hawawezi kukupeleka kwa sababu watajiharibia wenyewe.
1. Ni kweli,unapokopa wanasaidia. Na si kwamba watu hawawezi kurudisha. Ila kama mnataka biashara iende vizuri(wakopeshaji)

-jaribuni kupunguza liba.
-kuweni wastaarabu. Ikibidi,onaneni na mkopaji,kukwama si ajabu,anaweza lipa hata nusu nusu na akamaliza. Sasa,unatuma meseji,imejaa lugha za kihuni na vitisho,unategemea nini? Kuna watu hawaogopi kudhalilika.
-acheni ujinga na uhuni. Mkidai watu,utakuda tena si namba ya kampuni husika inayokudai, unaanza kutumiwa sms na namba nyingi sana. Kiofisi,hiyo itawashushia hadhi na kuwafanya muonekani hamjielewi.

2. Kuruhusiwa kuaccess contacts na sms, hakuwapi mamlaka ya kuwatafuta waliomo kwenye simu. Kisheria,hizi taasisi haziruhusiwi kudukuwa mawasiliano ya mtu,ukizingatia hazitambuliki. Ukikutana na mteja mjanja, kesi ni hot keki na inalipa sana.

3. Mkiona mtu harudishi hiyo hela, kuna mawili. Huenda kakosa kabisa. Kaeni nae,mpendi hata option ya kulipa kwa awamu.
Vinginevyo, huenda haogopi kudhalilika. Je,dunia ya leo,ataulizwa ulikopa? Atajibu ndio. Atauliza walokukopesha unawajua? Atajibu siwajui.
Kama siyo benki,si taasisi inayojulikana, utamdhalilisha kwa nani?

4. Kama mnahitaji kuwa msaada kwa watu,elimisheni basi hata matumizi ya pesa. Watu wawe hata kikundi, kiwe na biashara inayoeleweka, kisheria,wakopesheni. Ila sasa,mti mmoja mmoja,liba kubwa.
Kwa anaewajua,anajua nyie ni wezi. Uzuri hamjifichi. Mnadaigi hela za wachina walikuja kuwekeza.
Mchina ana huruma gani na mbongo? Japo pia wana akili. Kwenye 100,000 yeye kupata 5,000 hana hasara. Kwa njaa zenu, kwenye hiyo laki,mnataka liba ya 47,000. Wapi na wapi!

Uzi huu wameanzisha wao,na kujibizana wao.
Wekeni utaratibu wa kistaarabu. Kama mkopaji anachukua 20,000 anarusisha 35,000 wakiwa wengi mmekomboa hasara ya asiye lipa. Fanyeni arudishe hata 25,000 muone kama watu hawatawalipa.

Pili,hela za kugawa kama njugu mtandaoni,mnazitoaga wapi?! Basi ongeeni na Voda,Tigo na mitandao mingine wawe wanakata wateja na kuwalipa!

Af cha ajabu,namba zote zinazodai,zikiwa whatsapp, ni picha za micharuko tuuuu. Haina shida, badhi yetu wanajipatia huduma kimasihara. Ajirimi watu wanaojielewa,wastaarabu. Mtu katukana mteja. Mnatarajia nini!! Sasa kama umemdhalilisha,unamdai wa nini wakati umeshajilipiza ujinga?

Wekeni mchanganuo wa malipo tuone na ushuru wa TRA.
Af,ongeeni na BOT.

Meseji inayowatumia watu,inawakost nyie,hamjui tu. Ina maanisha hamruhusiwi kukopa.
Na mahakama itamuamuru mtuhumiwa kulipa,lakini haimuwekei kiwango. Neva.
 
Wanipeleke mahamani wakanifunge kama wanaweza.

Silipi hata kumi hata kama uwezo wa kulipa nnao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…