View attachment 2911035
benki kubwa wanaonya watu kila siku
Hiyo ni wazi,mahakamani hawawezi kukupeleka kwa sababu watajiharibia wenyewe.
1. Ni kweli,unapokopa wanasaidia. Na si kwamba watu hawawezi kurudisha. Ila kama mnataka biashara iende vizuri(wakopeshaji)
-jaribuni kupunguza liba.
-kuweni wastaarabu. Ikibidi,onaneni na mkopaji,kukwama si ajabu,anaweza lipa hata nusu nusu na akamaliza. Sasa,unatuma meseji,imejaa lugha za kihuni na vitisho,unategemea nini? Kuna watu hawaogopi kudhalilika.
-acheni ujinga na uhuni. Mkidai watu,utakuda tena si namba ya kampuni husika inayokudai, unaanza kutumiwa sms na namba nyingi sana. Kiofisi,hiyo itawashushia hadhi na kuwafanya muonekani hamjielewi.
2. Kuruhusiwa kuaccess contacts na sms, hakuwapi mamlaka ya kuwatafuta waliomo kwenye simu. Kisheria,hizi taasisi haziruhusiwi kudukuwa mawasiliano ya mtu,ukizingatia hazitambuliki. Ukikutana na mteja mjanja, kesi ni hot keki na inalipa sana.
3. Mkiona mtu harudishi hiyo hela, kuna mawili. Huenda kakosa kabisa. Kaeni nae,mpendi hata option ya kulipa kwa awamu.
Vinginevyo, huenda haogopi kudhalilika. Je,dunia ya leo,ataulizwa ulikopa? Atajibu ndio. Atauliza walokukopesha unawajua? Atajibu siwajui.
Kama siyo benki,si taasisi inayojulikana, utamdhalilisha kwa nani?
4. Kama mnahitaji kuwa msaada kwa watu,elimisheni basi hata matumizi ya pesa. Watu wawe hata kikundi, kiwe na biashara inayoeleweka, kisheria,wakopesheni. Ila sasa,mti mmoja mmoja,liba kubwa.
Kwa anaewajua,anajua nyie ni wezi. Uzuri hamjifichi. Mnadaigi hela za wachina walikuja kuwekeza.
Mchina ana huruma gani na mbongo? Japo pia wana akili. Kwenye 100,000 yeye kupata 5,000 hana hasara. Kwa njaa zenu, kwenye hiyo laki,mnataka liba ya 47,000. Wapi na wapi!
Uzi huu wameanzisha wao,na kujibizana wao.
Wekeni utaratibu wa kistaarabu. Kama mkopaji anachukua 20,000 anarusisha 35,000 wakiwa wengi mmekomboa hasara ya asiye lipa. Fanyeni arudishe hata 25,000 muone kama watu hawatawalipa.
Pili,hela za kugawa kama njugu mtandaoni,mnazitoaga wapi?! Basi ongeeni na Voda,Tigo na mitandao mingine wawe wanakata wateja na kuwalipa!
Af cha ajabu,namba zote zinazodai,zikiwa whatsapp, ni picha za micharuko tuuuu. Haina shida, badhi yetu wanajipatia huduma kimasihara. Ajirimi watu wanaojielewa,wastaarabu. Mtu katukana mteja. Mnatarajia nini!! Sasa kama umemdhalilisha,unamdai wa nini wakati umeshajilipiza ujinga?
Wekeni mchanganuo wa malipo tuone na ushuru wa TRA.
Af,ongeeni na BOT.
Meseji inayowatumia watu,inawakost nyie,hamjui tu. Ina maanisha hamruhusiwi kukopa.
Na mahakama itamuamuru mtuhumiwa kulipa,lakini haimuwekei kiwango. Neva.