KERO Taarifa Binafsi: Kampuni ya mkopo mtandaoni (online loan app) imenidhalilisha sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Relax

Soma vizuri nilichoandika kuna majibu ya kila ulichouliza mwanzo na sasa hivi
 
Anyway, mimi sina cha kuwaambia tena.

Nimeelezea kadri ninavyojua na inavyotakiwa kua.

Hayo mengine sasa ni utashi wako.

Natafuta uzi wa kijana aliyeenda kuripoti kazini (kazi ilikua benki) akaambiwa unaonekana una deni la online la muda mrefu (ilikua deni la mtandao wa simu) haujalipa. Wakamterminate hata kabla hajaanza kazi.

Nikiupata nashare. Nikiukosa basi.

Taarifa za mdaiwa sugu huwasilishwa Credit Bureau idea ni kublock access zako za kukopa. So kila mwanachama wa Credit Bureau hawezi kukupa mkopo mpaka ukalipe huko kwingine. Kenya ni lazima kampuni ya mikopo iwe online ama la kujiandikisha, Bongo ni option.

Huu uzi ni kielelezo jinsi gani waTz tuna vipato vigumu, lakini pia tunafeli kutumia resources zilizopo. Kuna member anasema hua anakopa ili abet, na hua anablock kampuni akishakopa.

Wengi sana hatuna uchumi mzuri lakini hatujui kutumia resources pia (na hii naamini inatugusa weeeeeengi mno)
 
Hizo kampuni hazipo kweny credit bureau sio Kenya Wala Nigeria, wapo Kwa lengo la upigaji kutumia ujinga wetu.
Nasisi tunaish nao tu Hela za Bure hizo hawana Kaz nazo.
Kama kweny circle yangu ataona nimedharirika basi sio aina ya circle yangu akatafute circle yake
 
Mkuu, mi sioni shida uwepo wake. Maana,taratibu za mkopo wa benki ni ndefu, na vigezo vyao wengi hawana. Af pia,wewe unaweza kwenda benki kukopa elfu 50? Umemuona bilionea anakuja kukopa mtandaoni? Wenye shida na milioni 100,wanaenda benk. Na benki huenda iliondoa mikopo midogo kuepuka usumbufu. Wale wenye shida na elfu 20,50,... wakakumbukwa.
Sehemu za kulekebisha tu(sijui kama viongozi wao wanajua):
-Hakikisheni mnawasiliana na anaeomba mkopo. Wengi wao wanajua ni kukopa tu. Maana, kwenye maelezo ya mkopo, ni kama ukiopa elfu 10, utarejesha 12. Lakini ukikopa, utaona unatakiwa 18 elfu.
-Wasilianeni na wadhamini,mjilidhishe,wakikubali,wawekeni. Wakikataa,achaneni nao.
- Tumieni namba za ofisi kwa mawasiliano.
-Punguzeni matusi na dhalau kwa wateja wenu. Tumieni kauli za kiofisi.

Mtu anakwambia,mi nataka pesa,sina undugu na wewe, na matusi ya nguoni. Huyo utaanzia wapi kulipa! Haya,hata hajitambulishi,anataka pesa tu.
Wawe na hekima,ni msaada mkubwa kwa wengi
 
kuna nyingine Pesa X wana maneno ya shombo hadi niliwasave wote namba zao 11 kwenye access nilifinya kuna app moja ilikuwa hacked ilikuwa inaruhusu kupata sms na namba lakin inawapa empt kwahyo hawakupata access yoyote sikuwalipa niliwazulumu
Unajiona bonge la mjanja kujiita mdhulumati

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Unajiona bonge la mjanja kujiita mdhulumati

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Hao wamiliki wa online loan apps ndo madhulmati wakubwa.

Wanakuchaji overdue fee lakini hapo hapo wanakupigia simu kukutisha, kukutukana na kero kede kede.

Unawauliza si kuna hii fee mmenitoza ya kuchelewesha deni?
Si nitailipa na fee? Sasa matusi matisho ya nn?
Poor customer service, mbona voda, tigo watu wanakopa huko, wakichelewesha wanapigwa fine na wanalipa.

Hawa online apps dawa yao ni kuwapiga tu hela afu hakuna kuwalipa
 
Haya maujuzi kwangu kidogo sikuwa nayo mkuu.

Ila nimedhalilika pakubwa sana, hadi kuna demu naona ni kama ananiacha hivi kwa sababu ya sms aliyotumiwa
Kuna muda jitoe tu akili ili ujifunze kitu, wajibu kuwa ujapokea pesa yoyote na kama wanataka waende mahakamani, mi nishawajibu majibu hayo wakaishia kutukana tuu, hizo riba zao kubwa mno hawana pa kupereka kesi kama hizi,
 
Mkuu pole kwa yalokusibu.
Nilitamani niandike kirefu ila leo acha niandike kwa ufupi.

Mkuu kuwa na namba zaid ya 200 alafu unakopa kwenye app hayo ni matumizi mabaya ya rasmali watu
 
Mkuu pole kwa yalokusibu.
Nilitamani niandike kirefu ila leo acha niandike kwa ufupi.

Mkuu kuwa na namba zaid ya 200 alafu unakopa kwenye app hayo ni matumizi mabaya ya rasmali watu
Kuzungukwa na na 200 kwenye Phonebook sio issue JE,Watu wa aina Gani ? Kuna watu wana namba za familia (ukoo) , Wateja tofauti tofauti achilia mbali washikaji na washika dau ukiongeza na mliowoma nao primary,sec,HADI chuo achilia mbali wale WENYE Mbili+ unajikuta unaa namba hata 1000+ Tena umeyasave google 🤣
 
Kwani hao jamaa wamewahi kumtangaza mtu kwenye mitandao ya kijamii kama ameshindwa kuwalipa pesa zao?
 
Ukisha lipa tu wanakublock.
 
Hii kadhia ya mikopo ya mtandaoni ipo wazi kabisa wanadhalilisha haswa wanajisahaulisha kua wamelipwa.

Niliwahi kukopa day 1 kiasi Cha 20000 na marejesho iwe 26, nikalipa ila still wanadai cjawalipa na wakaanzakutuma taarifa kwa wazamana wangu.
 
Hii kadhia ya mikopo ya mtandaoni ipo wazi kabisa wanadhalilisha haswa wanajisahaulisha kua wamelipwa.

Niliwahi kukopa day 1 kiasi Cha 20000 na marejesho iwe 26, nikalipa ila still wanadai cjawalipa na wakaanzakutuma taarifa kwa wazamana wangu.
Licha ya wao kudhalilishana kwa kutuma jumbe za vitisho kwa mkopaji na wanaodaiwa kuwa wadhamini, je hatua gani nyingine ambayo wanaweza kuchukua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…