Castr
JF-Expert Member
- Apr 5, 2014
- 35,012
- 70,201
RelaxKama kipi mkuu!! Kwani umetembea na mke wa mtu? Hicho kitakushushia hadhi.
Kwani,umemdhulumu yatima au mjane? Hicho, nafsi itakusuta.
Kutowalipa si kwamba hutaki kulipa. Kwani shida zimeisha? Zipo. Ila sasa. Umekopa kwa sababu umekwama. Na huenda kwenye kulipa,umekwama.
1. Kwa nini wasiweke utaratibu hata wa kulipa kidogo kidogo?
2. Kwa nini watukane mteja kama kweli wapo kibiashara?
3. Kwa nini wakudhalilishe? Wakikupigia simu,wakajitambulisha, utashindwa kuongea nao?
4. Kwa nini ukute namba zaidi ya 50, zinakupigia, zinakutumia sms, zote zinakudai. Kampuni ni ipi kati ya hizo?! Wengine wanaenda mbali, wanakwambia utume hiyo pesa kwenye number furani. Kwa nini wasisisitize utumie njia ulotumia kukopa!
Wakiacha matusi yao na sms za kihuni, mbona watapata! Utaratibu mbovu, ndo chanzo cha yote hayo
Soma vizuri nilichoandika kuna majibu ya kila ulichouliza mwanzo na sasa hivi