Taarifa Kwa Umma: Fact Finding Mission-Jimbo la Kigamboni

Jitambulishe tukujue we ni nani na uchunguzi wako utasaidia vipi wamanchi au mamalaka za juu.
Shida yako ni hiyo tu au kuna kingine?Nispojitambulisha na kama utafiti wangu ni kwa ajili ya kjifunza tu basi niache kujifunza?
 

Baada ya kibano cha wajumbe kuna kiunzi kingine cha umangi-meza wa serikali ya CCM kubana kazi kama yako ya kitafiti / maoni. Sheria zingine mnazotunga CCM hamkujua zitakuja kuwa pia kikwazo kwenu.

Kibali unaocho au ufahamu kuwa chini ya utawala wenu wa CCM Mpya zoezi kama hili ni batili na haramu.

Tafiti, social science survey na maoni yanahitaji ruhusa ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS kwa mujibu wa sheria iliyopitishwa kwa wingi na wabunge wa CCM.
Sheria ya takwimu kuwabana watafiti? Mtakwimu mkuu wa Serikali atoa ufafanuzi
Source : azam tv

Maoni kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Takwimu :: Matangazo ...
28 Sep 2018 · Msimamo wa Asasi za Kiraia kuhusu Mapendekezo ya ... waitaka serikali kutekeleza Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa ...
Maoni kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Takwimu :: Matangazo :: Vyombo vya habari :: Twaweza.org
 
(1) Hebu malizia kwanza hiyo M na J kwenye jina lako na uweke mawasiliano yako.

(2) Kampeni zimesharuhusiwa kuanza?
 
Angalau wewe umeanza kuelewa...Wengine naona wana sentiments.Kama wewe ni kazi wa Kigamboni unaweza leta maoni yako pia

Mkuu naona unalazimisha kumalizia nyumba yako kwa pesa za Bashite. Unakuja na Id fake unajifanya kukusanya maoni ww ni nani? Kwani hakuna mikutano ya mitaa mpaka uweke email yako ukusanye maoni? Acheni utapeli wa kijinga.
 
Mbona watu wana hofu za namna hii,Mimi nafahamu ninachokifanya sijui kama wewe unaelewa ulichokisema

Unafahamu unachokifanya? Huo ndio utaratibu wa kukusanya maoni ya wananchi? Nyie ndio wale matapeli wa hiyo pesa tuma kwenye namba hii.
 
Mmedhamiria kukusanya maswali ili kummaliza aliopo kuwa hajui changamoto za kg.
Mipango ya kuleta maji ya 1.Dawasco tuondokane na maji chumvi.
2.Soko la samaki.mapato ya samaki yanaenda ilala peke ake ingawa sehemu kubw ya uvuvi Dsm inayovuliwa ni bahari ya kigamboni.
3.Ahadi ya rais wakati wa uzinduzi wa daraja.alisema ole njia imeanzia buyuni inaenda mpaka pugu.Basi barabara ya kibada buyuni ikamilike na kisha buyunivpajengwe soko kubwa la mnada wa samaki.
 
Pili pale tulipompora manji gezaulole pajengwe michezo complex yaani viwanja vya michezo yote kuanzia uogeleaji,riadha zote,netball,kikap,football.badala ya kuja na hoja ya kizamani za kugawa kwa wananchi.natumai panatosha pamoja na kuwa ofisi za serikali zimeshakaa lakini patatosha tu.
 
(1) Hebu malizia kwanza hiyo M na J kwenye jina lako na uweke mawasiliano yako.

(2) Kampeni zimesharuhusiwa kuanza?
Mkuu,natamani nifanye hivyo ila wakati muafaka ukifika nitaweka ila kwa sasa wana Kigamboni wanweza kutoa maoni yao ili tuandae mipango nakuhakikisha wagombea wote wanatambua matarajio yetu ili kama wakijipima wakiona hawatoshi wajue kwamba kazi ni nzito.
 
Weka kibali cha ruhusa ambacho kimetolewa na tume ya uchaguzi, vinginevyo ni zoezi haramu.
 
Asante sana ndugu yangu wewe ni mwanakigamboni kweli.Tuendelee kutoa maoni ili tupate viongozi bora wanaojua kile tunachotaka kwa maendeleo ya kigamboni.Tunataka wananchi nao wawe na sauti sio wagombea kuja na ahadi hewa na rushwa na kupotea baada y uchaguzi kwenda kukusanya faida.Mabadiliko yataanzia Kigamboni.
 
Matatizo na mahitaji yote muhimu ya watanzania yanajulikana na yanafanana,acha kupoteza muda.
Ikifika wakati wa kampeni itakuwa kampeni ila kwa sasa ni fact finding tu.
 
Weka kibali cha ruhusa ambacho kimetolewa na tume ya uchaguzi, vinginevyo ni zoezi haramu.
Uharamu wa hili zoezi ni upi,Kibali cha tume kitalipa zoezi uhalali?Usiwe na uchungu moyoni na kushindwa kufikiri kama mzalendo.Kama vyama vvyote vingetumia mfumo huu wa maoni kwa hakika wananchi wengi wangshiriki na tungepata maoni ambayo yanaakisi mahitaji ya wananchi
 
Matatizo na mahitaji yote muhimu ya watanzania yanajulikana na yanafanana,acha kupoteza muda.
Mkuu,hakuna kitu kama hicho,ila kama umechagua kuamini sishangai kwa nini miaka 50+ baada ya uhuru bado tuna watu wenye fikra kama zako.Ni uthibitisho kwamba kuna tatizo katika mfumo wetu wa elimu na uongozi
 
Umeshindwa hata kudesign email yenye mvuto, yaani email ilivyokaa tu inaonyesha kitu unachofanya siyo formal na obviously haupo serious nacho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…