Uongo wa taarifa unaonekana hapa! Kama ungesema ma-DED angalau inge-make sense kwa sababu kazi zenye changamoto huko mawilayani ni kazi za ma-DED na kundi lake la watalaamu manake hawa ndio wanafanyakazi moja kwa moja na madiwani! Huko mawilayani, hususani wilaya ambazo kata zake ni vijiji unaweza kukuta Diwani wa Form IV ndo diwani msomi; halafu wewe unaenda pale na usomi wako, lazima upate shida! Nilishawahi kuishi wilaya moja, unaambiwa Mwenyekiti wa Halmashauri ni Standard VII, halafu mzee ni Much Know balaa, huku akiwa amejaaliwa kipaji cha kuongea. Unaambiwa Halmashauri mzima (DED na Watalaamu wake) ilikuwa inamgwaya! Ujinga wa Halmashauri (DED na timu yake) ni kama unavyoona Bungeni Dodoma! Unakuta Waziri una PhD yako, umefanya kazi hadi ma Umoja wa Mataifa huko lakini bado wanatokea akina Msukuma na Lusinde wanakuambia "Uprofesa wako ni bure kabisa"!