Taarifa kwamba wapo wakuu wa wilaya wameomba kuacha kazi kwa ajili ya majukumu mengine binafsi zina ukweli?

Pesa zimekata Ukata unawakata
Hata hivyo kwa mtu mwenye kazi yake nzuri/biashara zake hawezi kukubali kuwa DC, kwani hana fungu lolote, kila kitu ana mtegemea DED!!, hata mafuta ya kwenye gari lake ni mkurungenzi ndiye ana muwekea!!au uamue kutumia style ya kamanda sabaya!!!!
 
Hata hivyo kwa mtu mwenye kazi yake nzuri/biashara zake hawezi kukubali kuwa DC, kwani hana fungu lolote, kila kitu ana mtegemea DED!!, hata mafuta ya kwenye gari lake ni mkurungenzi ndiye ana muwekea!!au uamue kutumia style ya kamanda sabaya!!!!
Kuna michongo mingi nje ya mshahara
 
Kuna michongo mingi nje ya mshahara
Kama michongo ya ubabe, sawa lakini DED ndo anaweza kuwa na michongo mara 100 ya DC kwa sababu, anaweza kuwa na vikampuni uchwara vyako kibao halafu akawa ana-influence tender ziende huko!! Na hiyo michongo ya ubabe ndo wanaitumia sana, na huko wilayani, kuwatisha wawekezaji!!
 
Kujilimbikizia mali, ardhi, biashara
 
Mkuu, unakosea sana unapotoa mfano wa Mwalimu. Wakati ule wasomi hawakuwa wengi ndio maana ikawa hivyo. Jua kuwa miaka 40 sio mzee, mzee ni yule wa miaka 60 na ndio maana wanastaafuu. DC mzuri ni yule wa 40yrs na amekuwa promoted kutoka chini.
 
Majungu na upuuzi...

Tanzania hii mtu atake kuacha kazi kama ya u DC ashindwe?Wakati wanaosubiri kum replace ni wengi kupita maelezo?..
Tatizo ni kukosekana uhuru. Wanakosa uhuru kwa kuogopa kuiudhi mamlaka ya uteuzi. Vijana wenye maono wanaona uteuzi umewafunga. Wengi wanatamani kuipanga kesho yao kwa kusoma zaidi, wakielewa uteuzi si ajira ya kudumu, inategemea upepo wa kisiasa. Hapa ndio umuhimu wa kuteua watu wazoefu wenye malengo yaliotimilika.
 
Ulinzi na usalama kwani kazi ya polisi ni nini? Wakati mnasema nchi hii ni ya amani. Wasiwasi uko wapi?
 
Unaposhindwa kusikilizana na madiwan au wazee wa chama ukataka kuacha kazi basi umeshindwa kazi sio kutaka by the way madiwan wanaingilianaje kiutendaji na DC kiasi cha kutaka kuacha kazi labda DED ningeelewa
DC anataka ahusike na yote yanayofanywa na office ya DED na hapo ndo mikwaruzano inapo anza.
 
Sasa hivi wakuu wa Wilaya ni mabillionea toka magu kufa mkuu wa wilaya anakuwa bilionea ndani ya miezi miwili tu ukusikia temeke barabara ya km1 iliyokuwa igharimu milioni1500 imetumia milioni 5800 hapo milioni 4300 wamekula wakuu wa wilaya na mkoa
Kama ulio andika hujachapia, tumekwisha. Ujenzi wa barabara ya lami uliwekwa wastani wa 1bn kwa km. Kama leo imefika 5.8bn, kazi iendelee!
 
Kweli u-DED una changamoto zake lakini ndiyo wanao-manage matumizi ya fedha za halmashauri.

U-DC ni cheo cha kisiasa tuu, hawana reliable source of income, wengine wanaomba mpaka hela ya mufata kwa DED.

Kuliko unipe U-DC bora unipe -DED. Waliowahi kufanya kazi halimashauri wanajua nani ni mkubwa kifedha kwenye ngazi ya wilaya.

Kimsingi nafasi ya ukuu wa wilaya inatakiwa ifutwe. It is the most useless post in the world.

Heri mfagia ofisi makes the office to look clean lakini kijana kuwa DC ni kukosa uelekeo na maarifa.
 
CCM inaangalia nani mwenye pesa, haiangalii nani kasoma, katika kugombea udiwani na kisha -mayor. Wenyeviti wa madiwani wasio na shule ni kawaida. Hata Tabora, awamu ya tatu nyuma alikuwa wa std 7, akaja msomi, awamu hii yupo aliishia la 5 lakini ana pesa ya kumwaga.
 
Yaweza kuwa nikutofurahia aina ya siasa yetu,kwenye mambo yote.
Mkuu nakubaliana nawe. Ma-DC wa sasa hawajui wapo chini ya nani (siku hizi delegation of power naona haipo). Na kwa kiasi kikubwa wanafanya kazi za siasa jambo ambalo kijana msomi anaona kama inampotezea vision yake.
 
Kuna michongo mingi nje ya mshahara
Sasa mkuu DC, michongo yake lazima awe ya mambo yanayohusiana na rushwa!!tofauti na hapo hana, labda visafari!!michongo ya rushwa haina garantii muda wowote kinawaka!!
 
Tatizo ni kuwa walioteuliwa hawajawahi hata kufanya kazi serikalini,unategemea mtu ambaye maisha yake amekuwa mulimbwende, anaendesha saluni au mgahawa au ni mwanamuziki au msherehaji gafla unampa kazi ya kusimamia kanuni na miongozo ambayo hana uzoefu nayo ataweza hilo ndio kosa hawa hawana ujuzi wowote, zamani wengi walioteuliwa walikuwa tayari wanakuwa na uzoefu katika utumishi wa serikali, siku hizi ni vimemo na kushikwa mkono na mamlaka za uteuzi na wapambe wao, sidhani kama mtumishi wa serikali ambaye yupo kazini na ana uzoefu na utumishi pamoja na uendeshaji wa serikali akiteuliwa kuwa mkuu wa wilaya au mkurugenzi wa maendeleo wa wilaya atalalamika, hao walioletwa hata kutengeneza bajeti hawajui, hao wachekeshaji wameshazoea maisha ya mijini leo hii uwapeleke Litopwasi unategemea matokeo yao yaweje kama si kulalamika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…