Amefuata utaratibu wa kupata hizo nyaraka? na je benki iliwasiliana na mteja na mwisho hizo photocopy ni certified copy of the original?
Ni hatari sana .
TOKA MAKTABA :
“
kizimba maalum cha shahidi” maana yake ni sehemu ya kusimama au kukaa wakati wa kutoa ushahidi iliyoandaliwa mahsusi ili kumwezesha shahidi anayelindwa kutoa ushahidi bila kuonekana isipokuwa kwa jaji au hakimu anaeyeendesha shauri husika
"
shahidi” maana yake ni mtu anayehitaji ulinzi kutokana na tishio au hatari iliyopo au inayoweza kutokea kutokana na kutoa taarifa katika chombo cha kusimamia sheria, kutoa au kukubali kutoa ushahidi kuhusiana na kosa au shauri la jinai au kwa sababu nyingine yoyote ambayo mahakama inaweza kuona kuwa inatosheleza, na anajumuisha mtu anayestahili ulinzi kwa sababu ya kuwa na uhusiano na mtu huyo;
“
uhariri” inamaanisha kuondoa taarifa za utambulisho kutoka kwenye hati au kitu;“ulinzi wa shahidi” maana yake ni hatua au mbinu za kumlinda shahidi ambaye maisha, usalama, au mali yake inaweza kuwa katika hatari au tishio kutokana na kukubali kutoa ushahidi mahakamani katika shauri husika
5. Mamlaka ya
(1)Mahakama inaweza kutoa amri ya ulinzi iwapo itaridhika kwamba mtu aliyebainishwa katika maombi ni shahidi kwa madhumuni ya Kanuni hizi na maisha yake, usalama wake, au mali yake inaweza kuwa katika hatari au tishio kutokana na yeye kuwa shahidi.
(2)Katika kutoa uamuzi chini ya kanuni hii, mahakama itazingatia mazingira ya shauri ikiwa ni pamoja na—
(a)uzito wa kosa ambalo linahusishwa na ushahidi au maelezo ya shahidi huyo;
(b)aina na umuhimu wa ushahidi au maelezo husika;
(c)aina ya hatari inayoweza kumkumba shahidi;
(d)uwepo wa njia mbadala zinazofaa kumlinda shahidi;
(e)kumbukumbu ya makosa ya jinai ya shahidi au mshitakiwa;
(f)uwezekano wa amri husika kuzuia ushahidi kudodoswa ipasavyo na mdaawa yeyote katika shauri au kutohatarisha maslahi ya haki; au
(g)hatari inayoweza kutokea kwa umma iwapo shahidi hatalindwa.
(3)Maombi ya amri ya ulinzi yatasikilizwa katika faragha.
6. Amri za ulinzi
(1)Mahakama inaweza kutoa amri ya ulinzi kwa kuelekeza hatua yoyote au mchanganyiko wa hatua zifuatazo kwa madhumuni ya
(a)kuzuia kuwekwa wazi kwa umma au vyombo vya habari utambulisho au mahali alipo shahidi, au watu wanaohusiana naye au kuhusishwa naye kwa njia mbalimbali, ikiwemo;
(i)kuondoa taarifa zinazomtambulisha kutoka kwenye taarifa za mahakama zinazowekwa wazi kwa umma;
(ii)kuhariri taarifa zinazomtambulisha katika nyaraka au vitu;
(iii)kutofichua jina la shahidi au mhanga au kumpa jina bandia kwenye hati ya mashtaka au taarifa;
(iv)kutofichua maelezo au nyaraka zinazoweza kupelekea utambuzi wa shahidi;
(v)kutoa ushahidi kwa kutumia vifaa vya kupotosha au kubadilisha picha au sauti, au akiwa haonekani;
(vi)kumpa shahidi jina bandia ambalo halitasababisha utambulisho wake kwa namna yoyote ile;
(vii)kukataza mhusika yeyote katika shauri kuweka wazi taarifa zozote za shahidi kwa mtu asiyehusika;
(viii)kumpa shahidi chumba maalum na kilichojitenga cha kusubiria; au
(ix)kuendesha mwenendo wa shauri katika faragha;
READ MORE :