Taarifa za Heche za Benki ya CRDB zaonyeshwa hadharani Mahakamani na Wakili wa Serikali bila idhini ya mwenye Akaunti

Na Martin Maranja Masese

Taarifa za kibenki za mteja zina ulinzi mkali wa siri za wateja, kuzingatia kanuni ya Usiri wa Kibenki (Bank Secrecy and Confidentiality Principle). Nguzo kuu inayojenga uaminifu kati ya benki na wateja.

Kisheria, taarifa za kibenki za mteja zina ulinzi mkali wa siri za wateja unaotokana na mkataba kati ya mteja na benki, Sheria ya Taasisi za Benki na Fedha, na Sheria ya Ulinzi wa Taarifa za Binafsi.

Benki inatakiwa kulinda taarifa za mteja isipokuwa katika mazingira manne pekee: (i) Compulsion of Law), (ii) Duty to the Public, (iii) Interests of the Bank, (iv) Consent of the Customer.

Wakati John Heche anatoa ushahidi wake katika kesi ya uhaini ya Jamhuri Vs. Tundu Lissu, Wakili Mkuu wa Serikali, Katuga ametoa nyaraka zake za ‘photocopy’ kuonyesha akaunti ya benki ya John Heche.

Nyaraka hizo za ‘photocopy’ zimetolewa na Wakili Mkuu wa Serikali ili kuonyesha taarifa za miamala ya John Heche mbele ya Mahakama kutoka katika akaunti yake ya Benki Na. 01522005XXX.

Nyaraka za kibenki kama zikihitajika na Mahakama, zinatakiwa kuwasilishwa Mahakamani zikiwa unauthenticated au uthibitisho wa kisheria (Bankers’ Books Evidence Act/Certified Copies).

Soma Pia: Leo tarehe 14 September, Shahidi John Heche ameshafika tayari mahakamani

Anyways, kama kuna kuvunja mkataba wa usiri wa mteja (Breach of Duty of Confidentiality), John Heche akimaliza kutoa ushahidi wake Mahakamani, ataona nini anatakiwa kufanya katika jambo hilo.
Sasa ulivyo huna haya tuseme ùnajua sheria kuliko wale majaji? We ni zumbukuku tu sema umeumia huyo lofa wenu kuumbuliwa. Kielelezo ambacho hakijafuata taratibu za kisheria isingekubaliwa na kumbuka mshtakiwa ni mwanasheria asingekubali. Acheni ujuaji wa kipuuzi wakati kihalisia hamjui chochote
 
Barking at the wrong tree.
 
images (9) (5).jpeg
 
Acheni kumtoa shahidi kwenye mstari, kama yeye mwenyewe hajalalamika kwanini nyie mlete taharuki.
Iko hivi kesi ni ushahidi, na shahidi anabidi atoe ushahidi wa utetezi au kushtaki pasina kuacha shaka. Hili hilo litokee lazima shahidi awe muadilifu na atoe taarifa ambazo anaweza kuzithibitisha. Kinachowatesa mashahidi wa mshitakiwa wanatoa taarifa nyingi ambazo hawana uhakika nazo, halafu wanajionesha mbele ya mahakama kwamba wao ni waadilifu na hawana makandokando.

Hali kama hiyo ndo inafanya upande wa mashtaka kutumia nguvu kubwa kujaribu kuonesha mashahidi wa utetezi hawana uadilifu wanaousema na vilevile taarifa zao nyingi hawana uhakika nao. Kwa hiyo tutulie tuendelee kujifunza
Ni sawa,katuga katoa wapi nyaraka binafsi za mtu.sheria inasemaje ? USITETEE uharifu
 
Acheni kumtoa shahidi kwenye mstari, kama yeye mwenyewe hajalalamika kwanini nyie mlete taharuki.
Iko hivi kesi ni ushahidi, na shahidi anabidi atoe ushahidi wa utetezi au kushtaki pasina kuacha shaka. Hili hilo litokee lazima shahidi awe muadilifu na atoe taarifa ambazo anaweza kuzithibitisha. Kinachowatesa mashahidi wa mshitakiwa wanatoa taarifa nyingi ambazo hawana uhakika nazo, halafu wanajionesha mbele ya mahakama kwamba wao ni waadilifu na hawana makandokando.

Hali kama hiyo ndo inafanya upande wa mashtaka kutumia nguvu kubwa kujaribu kuonesha mashahidi wa utetezi hawana uadilifu wanaousema na vilevile taarifa zao nyingi hawana uhakika nao. Kwa hiyo tutulie tuendelee kujifunza
Je kutumia taarifa za kibenki ni sahihi kisheria, au serekali inaweza kutumia njia yoyote? Maana iweje muweke mashahidi wa Jamuhuri wa Siri, lakini muweke taarifa za mtu za Siri wazi huko huko mahakamani?! Ama hilo nalo unataka kujifunza?
 
..Wakili, awe wa serikali, au binafsi, ana kinga ya kuvunja sheria mbele ya Jaji?

..Nilidhani kunatakiwa walau kuwe na karipio, au kupelekwa ktk kamati ya maadili.
Kwani Wakili wa Mshtakiwa aliweka pingamizi? Na unaweza kuta kuna sheria inampa DPP kupata hizo taarifa bila kibali cha mwenye akaunti.

Mambo kama haya ndio yananifanya niamini kuwa Lissu hakupaswa kujitetea mwenyewe. Hiyo kazi angewaachia wakina Kibatala. Wao wangeweza kumtayarisha vizuri shahidi dhidi ya maswali kama haya.

Amandla...
 
Hana ushahidi 😁,bora ungekaa kimya kuliko kuonyesha usivyoelewa sheria
Heche kwanza angepaswa kabla ya kukubali kuwa ni Account yake angepaswa kuuliza hizo Risiti zimifikaje mikononi mwa wakili.pia fedha zake Ktk acc yake binafsi zinauhusiano gani na kesi hii.kitendo Cha kukubali kuhojiwa kwa kutumia copy badala ya Document ambazo zimethibitishwa kisheria hiyo inamuweka Ktk Hali ngumu ya kumshtaki muhusika na Bank.
 
Kwani Wakili wa Mshtakiwa aliweka ping amini? Na unaweza kuta kuna sheria inampa DPP kupata hizo taarifa bila kibali cha mwenye akaunti.

Mambo kama haya ndio yananifanya niamini kuwa Lissu hakupaswa kujitetea mwenyewe. Hiyo kazi angewaachia wakina Kibatala. Wao wangeweza kumtayarisha vizuri shahidi dhidi ya maswali kama haya.

Amandla...

..mimi ninavyoelewa muendesha mashtaka hatakiwi kutumia ushahidi uliopatikana bila kufuata sheria.

..kwa hiyo kama Katuga hakufuata sheria ktk huo ushahidi wake basi atakuwa ameikosea mahakama, na ame-impeach credibility yake.
 
Kabisa. Lakini inawezekana kabisa kuwa sheria za Tanzania zinamruhusu kufanya alivyo fanya. Kama ni hivyo basi hakuvunja sheria.

Amandla...
 
Na Martin Maranja Masese

Taarifa za kibenki za mteja zina ulinzi mkali wa siri za wateja, kuzingatia kanuni ya Usiri wa Kibenki (Bank Secrecy and Confidentiality Principle). Nguzo kuu inayojenga uaminifu kati ya benki na wateja.

Kisheria, taarifa za kibenki za mteja zina ulinzi mkali wa siri za wateja unaotokana na mkataba kati ya mteja na benki, Sheria ya Taasisi za Benki na Fedha, na Sheria ya Ulinzi wa Taarifa za Binafsi.

Benki inatakiwa kulinda taarifa za mteja isipokuwa katika mazingira manne pekee: (i) Compulsion of Law), (ii) Duty to the Public, (iii) Interests of the Bank, (iv) Consent of the Customer.

Wakati John Heche anatoa ushahidi wake katika kesi ya uhaini ya Jamhuri Vs. Tundu Lissu, Wakili Mkuu wa Serikali, Katuga ametoa nyaraka zake za ‘photocopy’ kuonyesha akaunti ya benki ya John Heche.

Nyaraka hizo za ‘photocopy’ zimetolewa na Wakili Mkuu wa Serikali ili kuonyesha taarifa za miamala ya John Heche mbele ya Mahakama kutoka katika akaunti yake ya Benki Na. 01522005XXX.

Nyaraka za kibenki kama zikihitajika na Mahakama, zinatakiwa kuwasilishwa Mahakamani zikiwa unauthenticated au uthibitisho wa kisheria (Bankers’ Books Evidence Act/Certified Copies).

Soma Pia: Leo tarehe 14 September, Shahidi John Heche ameshafika tayari mahakamani

Anyways, kama kuna kuvunja mkataba wa usiri wa mteja (Breach of Duty of Confidentiality), John Heche akimaliza kutoa ushahidi wake Mahakamani, ataona nini anatakiwa kufanya katika jambo hilo.
Basi kama hivyo na mahakama zetu zinaongozwa na maku na ni za kipumbavuuuu! Kwa nini hawakukataa hapo hapo!
 
Back
Top Bottom