Taarifa za uongo kutoka BBC

Taarifa za uongo kutoka BBC

Jioni hii nilikuwa nasikiliza habari za dira ya dunia nimemsikia muandishi wa habari David Nkya, akisema yupo kambi la wakimbizi la Mtendeli iliyopo Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma

Kwanza hilo kambi halipo, tulilifunga miaka mitatu iliyopita. Akaongeza uongo wake kuwa Tanzania ina makambi matatu ya wakimbizi wakati ni mawili tu.

Wiki iliyopita mtangazaji huyu huyu alisema Kambi la Nyarugusu limepoke wakimbizi zaidi ya 12,000 kutoka DR- Congo! Wakati uhalisia ni kwamba, Hadi Leo tarehe 1, wakimbizi tuliowapokea hawafiki hata 9,000.

Najiuliza tu, Hizi contents za uongo za BBC zinamnufaisha nani?
TCRA wapo bize kupambana na channels za pilau huku nchi ikichafuliwa na propaganda chafu
 
Huenda hizo ndio Data alizopewa na kwenye vitabu vya misaada (wapigaji) kuna pesa inayoletwa ili kuhudumia hizo Kambi tatu na hao wakimbizi zaidi ya 4000 ambao hawapo (pesa zinahudumia matumbo ya watu)
Hii inaingia akilini
 
Mwambie Mwenyewe Yupo humu, ukitwambia sisi tufanyeje?🤷‍♂️
 
Kazi ya BBC ni kulisha watu uongo sana ndo agenda zao izo tokea miaka ya nyuma uko
 
Back
Top Bottom