Tabia ngumu ya mzazi, watoto mtaijua vizuri pale mzazi mmoja akifariki (wakiwa hivi pamoja hufichiana siri)

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Familia nyingi zina watu mizigo.

Ninaposema tabia mizigo ninamaanisha watu wenye tabia ngumu kumeza. Watu ambao wanavumilika tu kwasababu ni ndugu au wazazi lakini kiuhalisia hawafai hawafai! (Yaani kama ni chakula basi hawafai kwa kulamba, kutafna au kulumangia). Na hizi tabia ngumu za wazazi huwa hazioneshi ukali wakiwa pamoja! Kwasababu mmoja humfunika mwenzake na madhaifu yake.

Picha linaanza pale mzazi mmoja akifariki, hapo ndipo utajua nani alikuwa mvumilivu kwenye hiyo ndoa iliyo kuzaa wewe. Kuna watu hadi huwa wanajiuliza Hivi huyu ni mzazi wangu kweli? Kama hujawahi kuiona haina mana Haipo.

Kibaya zaidi Mijitu yenye tabia ngumu kwenye familia huwa ndiyo ya Mwisho kufa. Hii ina apply kwenye familia, hadi viongozi wa kitaifa.
 
Mkuu weka tabia zako ngumu wacha siasa!..😅
 
Hebu acha usanii mkuu.Kuwa mnyoofu na utupe Aa Bee Chee za kilichofuata ITV!Ingawa nimekuelewa.
 
kunywa maji kwanza.
 
Exactly wapo
 
Kwenye hii comment mkuu sema nilisahau kuquote
Hope wa pili hakusumbui
Pole ya nn! Hilo ni somo chukua
 
Umemaliza ni kweli kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…