OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Upo kwenye shughuli yeyote inayokunyima uhuru wa kupokea simu
Upo kazini busy na kazi kiasi cha kuepuka kupokea simu binafsi kwa sababu ni muda wa kumtumikia mwajiri ukihudumia wateja wake
Umeamua kuchukua muda wa kupumzika, umechagua kutokusikiliza yeyote ili uache akili yako ipate utulivu.
Kiufupi ni mazingira yeyote ambayo yanakufanya usipokee simu, kwa sababu una uhuru wa kutumia simu yako.
Lakini unakutana na mbongo ambaye hana kiasi. Yeye akili yake inamtuma akupigie simu mpaka upokee, anapiga simu hata mara 10. Ajabu ni kwamba hana hata jambo la dharura na kwamba angekupigia mara moja kisha baadae ukiwa free umpigie. Hata common sense tu ya kwamba ngoja niache sms imsaidie kujua kiasi kuhusu shida yangu.
Inakera sana kuona mtu anapiga simu nyingi mfululizo bila sababu ya msingi. Kama simu yako haipokelewi tulia, missed call moja au mbili zinatosha