Tabia ya kupiga simu zaidi ya mara mbili inakera sana

Tabia ya kupiga simu zaidi ya mara mbili inakera sana

Kataa kubali ila itoshe kusema anatoka kanda ya ziwa ,sitaki kutaja kabila maana ni wajomba zangu 😀
Jamaa ni Mbondei aliyekulia Kusini ni Mwanangu sana na jana baada ya kumaliza kuandika hii post dk 6 baadae akanibip 🤣🤣🤣
 
Dah huyo mchukulie tu ndivyo alivyo japo siku moja muelekeze
Kuna mambo yanamchanganya Jamaa yuko 38 mbele yangu kama miaka miwili na miezi kadhaa.
Kinachomchanganya shule alikuwa hataki na umri umeshaenda na kila anachofanya kinavurugika akiangalia wadogo zake watatu wana maisha yao.
Mdogo wake kaolewa na Mshikaji ambaye yupo Central Bank, anayefuata ni Telecommunications Engineer na Mwingine ni IT officer kwenye taasisi ya umma na mwingine yupo Law School. Yeye ndio anazurura tu lazima dishi liyumbe 🤣🤣🤣
 
Kuna mambo yanamchanganya Jamaa yuko 38 mbele yangu kama miaka miwili na miezi kadhaa.
Kinachomchanganya shule alikuwa hataki na umri umeshaenda na kila anachofanya kinavurugika akiangalia wadogo zake watatu wana maisha yao.
Mdogo wake kaolewa na Mshikaji ambaye yupo Central Bank, anayefuata ni Telecommunications Engineer na Mwingine ni IT officer kwenye taasisi ya umma na mwingine yupo Law School. Yeye ndio anazurura tu lazima dishi liyumbe 🤣🤣🤣
Hapo lazima dish liyumbe kama namuona anavyokuomba ushauri muda mwingine kuwa hivi siwezi kurudi shule alafu nije kuajiriwa 😀😀

Ijapokuwa naamini hata hao ndugu zake Wana maisha ya kawaida kulingana na hizi ajira za nchi yetu hivyo muoneshe hii komenti ,mwambie kusoma sio kutoboa Wala kupata ajira sio kuwa tajiri ,kikubwa acheze na hao nduguze ,wampe walau mtaji mueleze anaweza kuanza moja na bado ni mdogo Sana .
 
Mie napiga moja tu.. tena haiiti mpaka mwisho, usipo pokea sikutafuti tena mpaka ww ndio unitafute.

Siangalii cheo wala nini mwendo ni ule ule.

Kuna mmoja nilimpigia simu akanikatia.. nikamuacha kama wiki hivi ajanitafuta, siku yupo na shida zake akaanza kupiga simu na mie kama kawaida nikaweka silent nikaendelea na mambo yangu, baadae nikamtext tu kumuuliza alikuwa na shida gani.

Dharau sipendi, ukimkatia mtu simu ambatanisha na sms hata ya kumpooza sio unakata as if nilikuwa napiga simu kukuomba hela ya kula.
 
Ukiona Sijapokea simu tuma message. Sijui kwanini watu huwa wanashindwa kuelewa jambo hili
Wana scroll chini afu wanaona ulichoandika. Wanaamua kutofungua sms yako kumbe washaona ulichokisema. Yaani bado ujasema!
 
Upo kwenye shughuli yeyote inayokunyima uhuru wa kupokea simu

Upo kazini busy na kazi kiasi cha kuepuka kupokea simu binafsi kwa sababu ni muda wa kumtumikia mwajiri ukihudumia wateja wake

Umeamua kuchukua muda wa kupumzika, umechagua kutokusikiliza yeyote ili uache akili yako ipate utulivu.

Kiufupi ni mazingira yeyote ambayo yanakufanya usipokee simu, kwa sababu una uhuru wa kutumia simu yako.

Lakini unakutana na mbongo ambaye hana kiasi. Yeye akili yake inamtuma akupigie simu mpaka upokee, anapiga simu hata mara 10. Ajabu ni kwamba hana hata jambo la dharura na kwamba angekupigia mara moja kisha baadae ukiwa free umpigie. Hata common sense tu ya kwamba ngoja niache sms imsaidie kujua kiasi kuhusu shida yangu.

Inakera sana kuona mtu anapiga simu nyingi mfululizo bila sababu ya msingi. Kama simu yako haipokelewi tulia, missed call moja au mbili zinatosha
Anataka figooo huyoo mpwaa msaidiee
 
lakn sometimes inategemea umuhimu wa simu hyo. Mimi leo kuna mtu nahitaji anipe taarifa fulan hv ya biashara, nimempigia mara 17 na bado nampigia kwa sababh jamaa ni mlevi kwa hyo navizia kupiga kila mda labda pombe ztakua zimemuisha atapokea.
 
Back
Top Bottom