True story imenitokea a few days ago:
Kuna jamaa Fulani alikuja kwangu nikamkopesha hela kiasi kaweka kitu cha bond ili siku ikifike alete pesa yangu nimpe kitu chake!
Jamaa kakaa muda umekwisha zaidi ya miezi miwili hajaleta pesa yangu!
Nampigia simu siku ya kwanza Mara tatu kwa nyakati tofauti saa 1, 4 na 12.. mara hajapokea zote! Siku inayofuata nikapiga tena Mara 3 nyakati tofauti bila majibu! Siku ya tatu nikapiga Mara 2 bila majibu , napiga simu ya tatu AKAPOKEA tukasalimiana
Namuuliza kwanini nmekupigia simu Mara nyingi hupokei?
Akajibu "usinipangie matumizi ya simu yangu, njua unanidai una dhamana yangu hela yako ntakupa nikipata ,usininyime raha Wala kuingilia Uhuru wangu kisa unanidai" kusema ukweli nilifokea afu mtu anabainisha kuwa sijui kazi yake pengine alikuwa bize muda wote huo !
Sasa swali linakuja kichwani mwangu kwamba huyu bwana hata kam anafanya kazi gani je, anawezaje kuwa bize muda wote huo? Ina maana siku zote hizo hajashika simu yake?
Ukienda ndani zaidi utagundua kuwa watu sio waungwana