Tabia ya kupiga simu zaidi ya mara mbili inakera sana

Yeah sure.....Ila mi binafsi labda nisiwe na simu mkononi....Ila huwa naheshimu Sana mtu anayenipigia
 
Nasapoti mawazo ya mtaoa mada ( ), mtu at least upige mara 2 kama hauna jambo la dharura ukiona simu haijapokelewa basi jiongeze labda mwenye simu yuko bize au mazingira ambayo si rafiki kuongea na simu , hapo kaa piga muda mwingine baadae.

Inakera unakuta missed call 4 , 6 au 10 halafu mtu hana jambo la dharura au muhimu ambalo linahitaji kufanyia ndani ya muda huo aliopiga simu.
 
Ndo maana wengi wenu bado maskini sana. Ukipigiwa simu usiache kupokea. Kama mtu anaongea upuuzi mchane na kumwambia awe anapiga kuongea vya maana. KUTOPOKEA SIMU NI TABIA YA KIMASKINI. Kuna wale kama namba ni mpya hawapokei kabisa.. huu ni ujinga uliokubuhu. Kwenye huu ulimwengu wa digital mawasiliano ya aina zote usipuuze. Kuna wale ukituma message anasema sijaona.. upuuzi mtupu. Binti wa dukani kwangu alikuwa ana tabia ya kutoona message nikamwambia achague kuona message au kuacha kazi siku hiyohiyo ndo ghafla akabadili tabia.
 
Huwa situmii SMS watu wazima mfano awe ndugu yake mzee au mama mzazi, sasa kuna ambao huwa nawapigia siku zote hawapokei hivyo napiga mara moja leo napiga mara nyingine after 2 weeks. Napiga kwa interval hiyohiyo mwaka unakata, miaka miwili inakata na hawapokei. Ila ukituma SMS anajibu hata siku nne baadae.

Nikaacha kwa sasa tunakutana misibani.
 
Ni kweli muasibu/mhasibu/muhasibu😂😂
 
Mm naongoza hasa nikiwa kwenye relationship iliyonishika😂😂😂😂 yaani Huwa Sina kias ni kukugongea calls muda wowote niwe mkweli😂😂

ila Kwa pipo zingine hapana Huwa sipig sana naweza hata nisifungue missed call hata siku 2 Tena namba ngeni ndio sizipendi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…