Tabia ya kutafuta ugomvi bila sababu za msingi inasababishwa na nini?

Mwanaume anakaa mahali anapopata PEACE OF MIND yani hata uwe na shape nzuri vipi na unajua kupika vipi pia Chumbani unaikatikia kama feni lakini dada mwanaume Humpi amani yani wew ni kumvuruga tu bhasi jua ipo SIKU ATAKUACHA bila taarifa.
Huu ndio ukweli mchungu...hata wanawake we need peace kwakweli
 
Hata wanawake tupo Kama mlivyo wanaume, Sipendi kabisa Kero!!yaani nikiwa na mtu ananifokeafokea kila saa namshangaa Sana atachoona hapo Ni vumbiiii tu
Yaah yani mahusiano ya Kuleteana fujo bila sababu ya msingi sio kabisa japo kweli kuna ile Kuvurugana sometimes kwa sababu za maana.
 
Hali hii ya kupenda mtu akasirike inawezekana imetokana na malezi yako mtoa mada.
Kama tangu ukiwa mdogo uliishi na ndugu au mzazi mkali sana, mkorofi kwa aina kama za wale wa mama wakambo wasioishi vizuri na watoto wa nje wa mume. Unajikuta ukali wao unakuwa unauzoea na kuwa ni sehemu ya maisha yako.

Hivyo ukija kuolewa na mume mpole unajikuta kama kuna kitu kinapwaya kwenye nafsi yako, maana ulishazoea maisha ya misuguano. Hata huyo mwanaume ulie nae akikuacha, bado utajikuta unaangukia kumpenda tena mwanaume mwingine ambae nae atakuwa na tabia za kupenda ugomvi.
 
Hata wanawake tupo Kama mlivyo wanaume, Sipendi kabisa Kero!!yaani nikiwa na mtu ananifokeafokea kila saa namshangaa Sana atachoona hapo Ni vumbiiii tu
Hahahahah nilichojifunza kwenye maisha kuna wanawake wana sense kama za kiume ila wachache mno!

Halafu kuna wale ambao wana bitchiness to the max! Yani mwanamke anakuwa msumbufu tu automatically anapenda drama za kijinga na kupigizana kelele on a daily!
 
Kweli Mimi nahisi ninazo hizo sense zenu Aisee sitaki maujingajinga.....Kuna mmoja Hadi Leo anaulizaga hivi nilikukosea nini?Sina hata muda wa kujibu Upuuzi wake😂😂😂😂maana hachelewi kuanza drama.....Hivi unajua Kuna wanaume wenzenu wanaletaga drama za kulia?
 
Sipo kundi hilo my dear, ahsante kwa kushiriki pia..!
 
Mwanaume anakaa mahali anapopata PEACE OF MIND yani hata uwe na shape nzuri vipi na unajua kupika vipi pia Chumbani unaikatikia kama feni lakini dada mwanaume Humpi amani yani wew ni kumvuruga tu bhasi jua ipo SIKU ATAKUACHA bila taarifa.
Hahaha..
Sawa mzee wa kimasikhara..!
 
Sijui labda Wanaume tupo tofauti ila Mimi huwaga ni mwepesi sana wa Kumpotezea mtu yani Naweza kukupenda kufa lakini Ukileta drama za kifala na kunikosesha amani unaweza hisi sijawahi kukupenda kabisa[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Hujapenda we phaller..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…