Tabia ya kutafuta ugomvi bila sababu za msingi inasababishwa na nini?

Tabia ya kutafuta ugomvi bila sababu za msingi inasababishwa na nini?



Guys,

Naomba tuweke utani wa siku zote pembeni, mnishauri kitu na tuwe serious kidogo tafadhali.

Mimi nina tabia moja hivi, napenda kumchokoza hasa mtu ninayempenda sana, yaani naanzisha kama kaugomvi mpaka nahakikisha mtu kapanic ile aanze kutype meseji ndefu kama mvua.

Kisha nakaa pembeni, naanza kucheka yaani nacheka mpaka nalia lakini unakuta mtu kakasirika kweli na anakuwa anaamini tunagombana lakini deep down Mimi nipo zangu sawa, na nikimjibu namchokoza zaidi naye anaendelea kufunguka akiwa very serious, ila Mimi ndiyo raha yangu nimuone tu hivyo nafuraaahi.

Hii kitu siyo mara moja wala mara mbili, wala mara tatu, mpaka sasa naona hii siyo hali ya kawaida..!! Nikikaa zangu huko naanza zangu tu kuchokoza mtu, na nina enjoy ajabu.

Nimejaribu kuacha nashindwa maana nitajikuta tu tayari nishaanza kutafuta ugomvi ambao hata haupo.!! Yaani tukae muda kidogo hakuna purukushani.? Sijiskii kabisa nitatafuta tu chanzo na lazima nitakipata, nakaa pembeni na popcorn zangu naanza kuenjoy sasa.

Hivi hili litakuwa tatizo gani?
Narcissistic behavior. Kisaikolojia ni ugonjwa huu.
 
ya kwake ni vise versa, huwa upande mmoja unachukia while mwingine unafurahia

sijapenda mimi namuombea Mungu ambadilishe
Hahaha..
Ahsante dear, na uwe serious na maombi kweli tafadhali..!!
 
wanawake wa sasa wagomvi sana, sio wa kwenye ndoa tu hata michepuko, zamani michepuko ilikuwa tulizo la moyo ila kwa sasa maisha yamebadilika
Hahaha..
mpaka kina Mwita mnavurugwa sikuhizi.? Kwisha habari yenu..!
 
Hali hii ya kupenda mtu akasirike inawezekana imetokana na malezi yako mtoa mada.
Kama tangu ukiwa mdogo uliishi na ndugu au mzazi mkali sana, mkorofi kwa aina kama za wale wa mama wakambo wasioishi vizuri na watoto wa nje wa mume. Unajikuta ukali wao unakuwa unauzoea na kuwa ni sehemu ya maisha yako.

Hivyo ukija kuolewa na mume mpole unajikuta kama kuna kitu kinapwaya kwenye nafsi yako, maana ulishazoea maisha ya misuguano. Hata huyo mwanaume ulie nae akikuacha, bado utajikuta unaangukia kumpenda tena mwanaume mwingine ambae nae atakuwa na tabia za kupenda ugomvi.
Msichokielewa ni kuwa napenda tu kumuona kamind kisha anakuwa mkweli na anapambana kutetea penzi, basi me moyo burudani.. Nimeishi na wazazi wa kawaida kabisa.!
 
Kweli Mimi nahisi ninazo hizo sense zenu Aisee sitaki maujingajinga.....Kuna mmoja Hadi Leo anaulizaga hivi nilikukosea nini?Sina hata muda wa kujibu Upuuzi wake😂😂😂😂maana hachelewi kuanza drama.....Hivi unajua Kuna wanaume wenzenu wanaletaga drama za kulia?
Naomba nikutane na mmoja atalia mpaka kamasi..!
 
Zinaanzaga ludodoludodo hivyo. Kikawaida mwezio akiwa anaumia unatakiwa uimpathaizi sio kucheka. Aka kana tendency hiyo, believe me.
He's doing that kwa her significant other ONLY ila ingekuwa anafanya kwa kila mtu basi angekuwa kwa category ya wale wa grandiose

Ila asipoangalia anaweza akawa
 
Back
Top Bottom