Tabia ya wanaume kuvaa pens na kuzurura mitaani, ni ukosefu wa Maadili

Mambo yalianza kuharibika enzi za Mzee wa Ruksa.

Kimsingi ndio nguo zilianza kupatikana, inaonekana we mtoto sana, wakati wa Nyerere watoto tulikuwa na uniform za shule tu na wazazi wana suruali na shati moja la kushonesha na wamama wana khanga za Mwatex, Urafiki na Sunguratex, mzee Mwinyi ndio aliyeachia mipaka na nguo zikaanza kuingia, nashangaa watoto wa juzi wanaosema awamu ya kwanza wakati kipindi hicho mabinti wakubwa tu walikuwa wanatembea vifua wazi kabisa matiti nje na hii imeeisha miaka ya katikati ya 80's. Hapa wanajifanya wachungaji wa kukariri tu na kuweka standards za vichwani kwao kama wanajua sana na kuingilia uhuru wa watu!
 

Ujumbe kutoka madrasa,upuuzwe.
 
Basically fanya yanayokuhusu acha watu waishi maisha yao! Watu walikuwa uchi na hakukua na ubakaji, huu ulianza na kuongezeka baada ya usafi kuongezeka zaidi, miaka hiyo unatongoza msichana ananuka mikojo ana chupi moja tu hamna mwenye kutamani wala kubaka! Ulizeni muambiwe, hii nchi imetoka mbali sana na bado inasuasua kuendelea!
 
Ujumbe kutoka madrasa,upuuzwe.
Wanaume hawatopuuza.

Hivi utajisikiaje umevaa pens unayoita ya Heshima, Kisha unapishana na Mwanaume mwenzio kabana makalio na kipens, nyeti zote zimejichora kweupe halafu anasingizia joto?
 
Basi na suruali tuache maana nayo tumeiga. Turudi zetu kwenye vibwaya. Sijui utasemaje ukiona watu wameziba tupu tu kwingine kote kuko wazi?
 
Basi na suruali tuache maana nayo tumeiga. Turudi zetu kwenye vibwaya. Sijui utasemaje ukiona watu wameziba tupu tu kwingine kote kuko wazi?
Nadhani ujumbe uko clear,

Wanaume turudi kwenye nafasi yetu kuongoza Maadili ya familia na JAMII.

Tusijitoe ufahamu.
 
Hii tabia imeanza baada ya wale washinda vijiweni kuanza kwenda Jim kwaajili ya kutanua misuli ndio ujinga ulipoanzia wanajifanya wanaonyesha 6mbavu za mbwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…