Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 31,009
- 60,629
Kuna namna tunafeli kama jamii...Mimi nimeshajiuliza sana ila nikawa nabaki bila majibu sahihi ila uhalisia uliopo mtaani ni majibu tosha. Watu wanasomesha mabinti zao na wanawazingatia sana huku mitaani na hata humu jf wapo.
Hatuwezi kuwasema wake wasomi kuwa wana tabia za hovyo kwenye ndoa na kuona ni kosa kubwa kuoa wasomi huku tukiendelea na kupenda kuwasomesha watoto wetu wakike, ni wazi ni jambo la ajabu. Tunawaandalia nini kama tunajua hili?
Kwa hoja hii ni dhahiri hichi tunachoshahuriana humu na kupiga makelele kila mara ni ubatili mtupu na ieleweke ya kuwa nafasi ya mwanamke/mwanaume kwenye jamii ni ile ile.
Kwanza kwakujumuisha mambo kwa namna ambayo hatutoi nafasi ya kutafuta mzizi haswa wa tatizo u-wapi. Pili, kwakukimbilia solution ambazo sio reasonable, practical wala realistic.
Kwa mwenendo huu + mentality iliyotawala kwa sasa , miaka ijayo itakua na wasomi wengi wanawake na single mothers tutakua tumeongezeka mpaka waoaji wachanganyikiwe.