Tafadhali Rais Samia, Kikeke apewe Ukurugenzi TBC pengine ataleta mabadiliko

Aende ikulu akambadili greison,
ambaye amelewa madaraka
 
My friend!!! Lea chako. Usidanganywe na misemo ya zamani ya eti mpe mchawi akulelee mwanzo hatamdhuru.

Hiyo, haifanyi kazi siku hizi. Wachina wakipeleka watu wao kujifunza ng'ambo wanawawekea mapolisi wao huko huko wa kuwalinda na huku familia walizoziacha nyuma wanawekwa leani!!! Gadafi(R.I.P) naye alikuwa ameanza mtindo huo.
Huo mfumo unalipa!

Najua sauti ipo chini na msinitafute maneno eti niongeze sauti!
 
TBC ni Shirika la kumsifia Mwenyekiti wa CCM na serikali,kumbuka Tido alivyotaka kubadilisha Shirika Baba Kipara alivyokuja juu mpaka jamaa akaondoka.Nakumbuka wakati wa Tido tulikuwa tunaangalia ligi kuu ya England kama unakumbuka.
 
Kuacha kazi ya uhakika kwenye nchi zilizoendelea Ili uje kufanya kazi bongo inahitaji moyo sana
Ata Mimi huwa nashangaa,mtu unapiga mzigo ughaibuni na unavuta mshahara mrefu plus bonuses and insurance alafu unakuja Bongo kufanya kazi na vilaza.Kama yule Mfugale aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii, alikuwa Consultant kwenye kampuni kubwa kule Canada.
 
Aachane na TBC maana ilishapoteza uelekeo, ilishabaki kusifia uongozi na si kukosoa (balance story). Kikeke usiende TBC sifa yako itapungua.
 
Eti Fundi Maiko![emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Tatizo kubwa la TBC siyo Mkurugenzi na watangazaji.

Hata aende pale LISSU au Mbowe itabidi atangaze mambo ya CCM wanayotaka.

Ni aidha ukubaliane na maudhi yao au uache kazi.

  • Tunatekeleza
  • Kishindo Cha awamu ya 6
  • Safari ya Dodoma
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Na ndo anakokwenda
 
Mawazo ya kijinga kabisa Ila Kwa vile ni muislamu mwenzake na mtoa mada fuvu lake Lina shida basi atapewa
Udini unakusumbua.Charles Hillary amepewa kazi Zanzibar ni muislamu?Hizo fikra muflis za kidini hazitakufikisha popote.Kikeke akiwa na sifa za kuajiriwa ana haki sawa na mtanzania yeyote yule.Ukiacha kutumia makamasi kufikiri utaelewa hivyo.
 
Kwani Mkurugenzi Mkuu wa TBC ametoka..kwanini unazungumzia sehem ambayo tayar Ina mtu na yeye ameshafanikiwa kulipaisha shirika Hilo sana....sijui unajua TBC imetoka wapi na Sasa ipo wapi..unaijua..?? Pia usidhan kukaa nje ndio assurance ya utendaji mzuri....hapana..it's subjective...uzoefu yes lakini pia na elimu kichwani
 
Hii inamaanisha Kila anaepitia BBC basi anafaa kuwa mkurugenzi!?....

Uongozi hasa wa ngazi ya juu ...unahitaji vipawa fulani specific si umaarufu....

Si kila mchezaji bora..ama mashuhuri...Anaweza kuwa kocha bora
Sure..!!! Nakubaliana nawe jomba
 
Hii inamaanisha Kila anaepitia BBC basi anafaa kuwa mkurugenzi!?....

Uongozi hasa wa ngazi ya juu ...unahitaji vipawa fulani specific si umaarufu....
Umemaliza.
Na ni aibu kama taifa.. yani tusubiri watu watoke BBC ndio wapate nyadhifa hizo .
Utaratibu wa hovyoo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…