Tafadhali Rais Samia, Kikeke apewe Ukurugenzi TBC pengine ataleta mabadiliko

Tafadhali Rais Samia, Kikeke apewe Ukurugenzi TBC pengine ataleta mabadiliko

Kwa maoni yangu, naona ni Upumbavu na Upuuzi kumchukua 'Mtangazaji' anayepikiwa kila kitu, yaani kwamba hahusiki na na lolote lile,Kuanzia ukusanyaji wa habari mpaka matayarisho ya kipindi(editing,production etc) halafu ndie aje kuwa Mkurugenzi wa Chombo kama TBC ati kwasababu alikuwa akionekana kwenye luninga na alikuwa akifanya kwenye kampuni ya uingereza ya BBC! Huo ndio Ushamba wenyewe! Ndi Ulimbukeni 2.0
Bolded ..

Kwa CCM kila kitu kinawezekana... Na sintashangaa kabisa.
 
Kifupi hawezi kuacha KAZI hivi hivi BBC lazima kuna kitu atafanya. Ila huyu Kikenke ni Muingereza kwa sasa. Labda aajiriwe kama expertriate na analipwa mshahara wa mfanyakazi asiye raia. Patamu hapo.
Ameshachukua uraia..??
 
Mtangazaji mahiri Salim Kikeke siku ya jana aliaga rasmi, akitoa taarifa ya kuondoka katikaShirika la Habari la Uingereza baada ya kufanya kazi kwa kipindi cha miongo miwili (Miaka 20)

Kikeke kupitia matangazo ya Dira ya Dunia yanayorushwa na StarTV kwa hapa Tanzania aliaga rasmi kwamba matangazo ya jana ndiyo ya mwisho katika shirika hilo ambalo amefanya nalo kazi kwa miaka 20.

Kwa "experience" na "exposure" aliyoipata Kikeke kwa kipindi cha miaka 20 akiwa katika moja kati ya mashirika makubwa ya habari ulimwenguni nadhani ni muda wa Kikeke kurejea nyumbani, ni muda wa Taifa kufaidi matunda ya kijana wake, ni muda sahihi Rais Samia Suluhu afanye maamuzi yakayoleta mapinduzi pale TBC, ni muda sahihi KIKEKE AENDE KUHUDUMU KAMA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA HABARI TANZANIA (TBC).

Tumeona Zhura Yunus akipeleka ujuzi wake Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ya Tanzania na Charles Hillary akifanya hivyo kwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Zanzibar, sasa tumtumia Kikeke pale TBC.

Haya ni maoni na mapendekezo yangu tu, wadau mnaonaje?
Yaani bwana Liyoba hatoshi umeona au?
 
Kwa maoni yangu, naona ni Upumbavu na Upuuzi kumchukua 'Mtangazaji' anayepikiwa kila kitu, yaani kwamba hahusiki na na lolote lile,Kuanzia ukusanyaji wa habari mpaka matayarisho ya kipindi(editing,production etc) halafu ndie aje kuwa Mkurugenzi wa Chombo kama TBC ati kwasababu alikuwa akionekana kwenye luninga na alikuwa akifanya kwenye kampuni ya uingereza ya BBC! Huo ndio Ushamba wenyewe! Ndi Ulimbukeni 2.0

Tunawatafutia watu sifa ambazo kiuhalisia hawana, ni sifa za Kishamba Kuna tofauti gani na Kusema ati kwa sababu anajua King-eleza na amekuwa amebatizwa na anavaa kaptula na anakaa chumba cha ndani cha mkoloni basi ndie aje kuwa Kiranja wa wengine! This is a Stupidiest mentality on earth.
Sitaki kuamini bado tuna watu wamepumbazwa na bado wanataka kuendeleza kama sio kuchochea Ukoloni mamboleo. its Absurd.
Unadhani kuibadili taasisi ya serikali ni jambo rahisi, mpaka awe na "mkono" wa mwenye nchi.

Kama una bajeti ndogo, utatoa Hela mfukoni?

Sheria inayounda mashirika hayo pia ni mwiba.

Yote kwa yote ni bajeti. Lazima watu wa tv wawe na special package ya maana ya mavazi, wawe na saloonist wa maana

Mila na desturi za shirika. Ngumu kuzibadili.

Ayoub Rioba na Tido walau wamesogeza
 
Tbc ilikufa toka walivyomuondoa Tido mhando ,Labda akiletwa kekeke maiti inaweza fufuka ,Ila sidhani hilo lkitawezekana maana pale hatakiwi mtu mwenye mawazo chanya
Tatizo hilo
 
Hii inamaanisha Kila anaepitia BBC basi anafaa kuwa mkurugenzi!?....

Uongozi hasa wa ngazi ya juu ...unahitaji vipawa fulani specific si umaarufu....

Si kila mchezaji bora..ama mashuhuri...Anaweza kuwa kocha bora
Ni mawazo yako tunayaheshimu, lakini waliopita na kupewa nafasi wanaweza kukuprove wrong
 
Naomba niwakumbushe ndugu zangu Yanga imeingia nusu fainali

Haya mjadala uendelee
 
Kifupi hawezi kuacha KAZI hivi hivi BBC lazima kuna kitu atafanya. Ila huyu Kikenke ni Muingereza kwa sasa. Labda aajiriwe kama expertriate na analipwa mshahara wa mfanyakazi asiye raia. Patamu hapo.
Kwa hiyo unatuambiaje kuhusu Zuhra Yunus?
 
Kwa maoni yangu, naona ni Upumbavu na Upuuzi kumchukua 'Mtangazaji' anayepikiwa kila kitu, yaani kwamba hahusiki na na lolote lile,Kuanzia ukusanyaji wa habari mpaka matayarisho ya kipindi(editing,production etc) halafu ndie aje kuwa Mkurugenzi wa Chombo kama TBC ati kwasababu alikuwa akionekana kwenye luninga na alikuwa akifanya kwenye kampuni ya uingereza ya BBC! Huo ndio Ushamba wenyewe! Ndi Ulimbukeni 2.0

Tunawatafutia watu sifa ambazo kiuhalisia hawana, ni sifa za Kishamba Kuna tofauti gani na Kusema ati kwa sababu anajua King-eleza na amekuwa amebatizwa na anavaa kaptula na anakaa chumba cha ndani cha mkoloni basi ndie aje kuwa Kiranja wa wengine! This is a Stupidiest mentality on earth.
Sitaki kuamini bado tuna watu wamepumbazwa na bado wanataka kuendeleza kama sio kuchochea Ukoloni mamboleo. its Absurd.
UMEKARIRI
Kikeke amekuwa mtafuta habari, mtangazaji na Mhariri kabla ya vyote alafu kama unadhani ni rahisi nenda na wewe kakusanyiwe habari usome hata Kanisani au msikitini kwenu tu, Kalaghabaooo
 
Akienda TBC inabidi akili aziache London, pale atazitumia za kutokea Lumumba.
Hawezi toboa, watamfanyia figisu tu ndio wabongo tulivyo. Kuna aina flani ya maisha ambayo wanayo ofisi za serikali ambapo ukija na mfumo mpya lazma utachukiwa tu. Watu wanataka wapige hela sio kazi.
 
Yaani Kikeke kabisa umvalishe Kaunda Suit na atulie kwenye V8 kusubiria maelekezo toka Lumumba? Hizo kazi za kina Musiba labda

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]kwa kweli boss atakuwa machepelechele hawezi maana mizaha mingi sana yule
 
UMEKARIRI
Hutaki? Yakhee
Kikeke amekuwa mtafuta habari, mtangazaji na Mhariri kabla ya vyote
Sawa Whats your point?
alafu kama unadhani ni rahisi nenda na wewe kakusanyiwe habari usome hata Kanisani au msikitini kwenu tu,
Wapi niliposema kuna urahisi? Narudia Usidhani kila mtu anayeonekana Kwenye Luninga za Ulaya kuwa ndio mwenye Exposure au Experience kupita ya yule aliyoko Tanzania. Kwa Taarifa yako bwana Ryoba ana Exposure na Experience.. zaidi ya! amekuwa Kiongozi toka akiwa shuleni, haijalishi na haina maana kuwa ndio kila kitu, ila mentality yako ndio imekaa kushoto kudhani Salim Kikeke experience na exposure yake BBC ndio kila kitu. Nawafahamu wote....na sio kwa kutizama luninga tu. Salim anaweza kuchangia TBC kwa kisomo chake ila sio kwa mantiki uliyotumia kuwa kwasababu amekaa na Wazungu basi ndie anafaa. Ondoa hiyo fikra potofu.

Kalaghabaooo
Utajijiju
 
Mtangazaji mahiri Salim Kikeke siku ya jana aliaga rasmi, akitoa taarifa ya kuondoka katikaShirika la Habari la Uingereza baada ya kufanya kazi kwa kipindi cha miongo miwili (Miaka 20)

Kikeke kupitia matangazo ya Dira ya Dunia yanayorushwa na StarTV kwa hapa Tanzania aliaga rasmi kwamba matangazo ya jana ndiyo ya mwisho katika shirika hilo ambalo amefanya nalo kazi kwa miaka 20.

Kwa "experience" na "exposure" aliyoipata Kikeke kwa kipindi cha miaka 20 akiwa katika moja kati ya mashirika makubwa ya habari ulimwenguni nadhani ni muda wa Kikeke kurejea nyumbani, ni muda wa Taifa kufaidi matunda ya kijana wake, ni muda sahihi Rais Samia Suluhu afanye maamuzi yakayoleta mapinduzi pale TBC, ni muda sahihi KIKEKE AENDE KUHUDUMU KAMA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA HABARI TANZANIA (TBC).

Tumeona Zhura Yunus akipeleka ujuzi wake Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ya Tanzania na Charles Hillary akifanya hivyo kwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Zanzibar, sasa tumtumia Kikeke pale TBC.

Haya ni maoni na mapendekezo yangu tu, wadau mnaonaje?
Itasaidia kuleta mapinduzi? Media ambayo inatoa hbr kwa kufuata maelekezo ya wanasiasa? Ni ngumu sana hiyo!! Ili media ifike mbali na iwe na weledi ni lazima iwe independent, lkn sio hao wanaopewa maelekezo leo wafanye nn wakatishe kipind flan warushe futuhi flan la kisiasa.
 
Camera za TBC wakati wa ARDHIO kama vile wanatmia CAMERA ZA SIMU ZA TECNO. Watangazaji wanavyovaaa sasa hasa watangazaji wa kiume jamani kama wametoka kuazima makoti. Viatu vina vumbi. Masofa sijui wanachonga kwa fundi maiko. Huwa naangalia RWANDA TV jamani tukubali tupo usingizini TBC
Mavazi yana uhusiana na kazi mkuu?
 
NAKATAA KATA KATA ASIPEWE HIYO NAFASI.

Kumbukeni alichofanyiwa Tido Mhando, yaani inside the door hujui yanayofanyika mngejua mngekaa kimya.

Ataharibu VC yake kwa hiyo nafasi.
 
Mavazi yana uhusiana na kazi mkuu?
Kwani hujui. Emu angalia wanavyovaa RWANDAN TV UBC KBC NTV lingamisha na TBC. Angalia aljazeera BBC CNN DW FOX SKY NEWZ BTSPORTS na vituo vingine. Presenters wa TBC hasa wa kiume anatoka nyumbani na nguo alizovaaa anaenda moja kwa moja kwenye camera tena studio aseee kile ni kioo cha Taifa emu tufiche aibu yetu basi hata kama hatuna kiwanda cha nguo ndo tuvae mitumba kwenye luninga ya Taifa. Kumbuka TBC inaendeshwa kwa kodi za wanainchi na watu binafsi wanapeleka matangazo palee mishahara ya watumishi TBC inatoka HAZINA lakini kuvaa wanazidiwa hata na watangazaji wa blog tv jameni. Camera mbovu sana za mnato kama vile unaangalia SLIDE SHOW.

Kuandika majina ya watu hawawezi tena viongozi wakubwa tuuu. Graphics na content analyst very poor emu viwango vyao vya elimu viangaliwe upya ile ni STATE CONTROLED MEDIA inaonekana dunia nzima.
 
Back
Top Bottom