Tafadhali Rais Samia, Kikeke apewe Ukurugenzi TBC pengine ataleta mabadiliko

Hatujui terms zake za ajira kama ameajiriwaje? Ila taratibu za kumuajiri ambaye alishakana uraia maana yake ni mgeni.
Sahihi mimi sizijui!
Wewe unazijua?
Alafu hoja yako ni kukana uraia au Mi6? Usichnganye mambo wewe,
 
Tbc ilikufa toka walivyomuondoa Tido mhando ,Labda akiletwa kekeke maiti inaweza fufuka ,Ila sidhani hilo lkitawezekana maana pale hatakiwi mtu mwenye mawazo chanya

Tbc wanataka mtu anae endana na mawazo ya serikali, ukiwa creative tu kidogo tayari unaondolewa. Yalimkuta tido muhando, why kikeke aende pale?
 
Sahihi mimi sizijui!
Wewe unazijua?
Alafu hoja yako ni kukana uraia au Mi6? Usichnganye mambo wewe,
Kwa sheria za Tanzania mpaka sasa Mtanzania wa kuzaliwa ukiwa Raia wa nchi nyingine automatically umeukana uraia na si Raia wa nchi hii. Na ndiyo maana Diaspora ambao ndiyo wameshajiondoa Utanzania walipigania Sana Uraia pacha ili watambulike na kuwa na haki nchi zote 2 I e Tz na nchi aliyo Raia. Mambo ya M16 yanaingiaje hapa?
 

Suali la udadisi, kwani bi Zuhura pale kurugenzi ameajiriwa kama mgeni au mTZ?
 
Yaani wabongo ndio maana mnashikishwa ukuta... Mtu akiishi ulaya kidogo akirudi mnaamini atakuwa ana maarifa au pesa kuliko nyie... Kikeke ni fala tu kama mafala wengine kukaa bbc miaka 20 haimanishi ana utashi kuliko bibi yako kule kijijini...
Yaani ndo maana hata sishangai CCM/TANU kutawala miaka 62 .Maana watanzania wengi hawajielewi.
 
Ana kadi namba ngapi ya ccm?
Ataweza kuandaa na kurusha vipindi vya kipropaganda?
Kama hana hivyo vitu ajiendee tu AZAM
 
Litakuwa si vema kumpa Salim Kikeke ukurugenzi wa TBC ni chombo kikubwa sana kwake.

Mzee Tido Mhando aliweza kukiongoza chombo hicho ingawa si kama ilivyotakiwa na akaundiwa zengwe.

Hata huyo Ayubu Rioba nae ameanza kujifunza kuongoza maana hakuwa na zoefu wa uDG.

Ukurugenzi mkuu wa chombo kama TBC wabeba sifa nyinig za ziad ikiwemo sifa kuu kwamba mkurugrenzi mkuu pia ni mhariri mkuu wa chombo hicho yaani Editor-in-Chief.
 
Hayachanganyikani mafuta na maji, tbc inaongozwa kisiasa zaidi na ndipo anguko lake lilipo anzia
 
Suali la udadisi, kwani bi Zuhura pale kurugenzi ameajiriwa kama mgeni au mTZ?
Yeye Zuhura sijui ila Kikenke ni Raia Uingereza. Wenye kujua Zuhura waseme. Na kama Zuhura ni Raia Uingereza basi na Kikenke ataajiriwa kwa taratibu zilezile zilizotumika kumuajiri Zuhura. Tanzania kila kitu kinawezekana🤣🤣🤣🤣
 
Watu weusi tuna akili za kiBWEGE sana sana!....kwanini APEWE badala yakushindana halafu hata akipewa kama akili yako inavyokutuma unadhani atabadili nini....
TIDO sialikuwepo pale au ulikuwa hujazaliwa
 
Mkuu, ni kweli zilezile taratibu ndizo hizohizo zitatumika "provided" umo kwenye system.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…