Tafakuri ya FaizaFoxy 7: Shule za kusomea ujinga. Tanzania na propaganda za Udini Shuleni

View attachment 2212053

Kwanini Zanzibar wana makumbusho hayo, nani muhusika wa kwenda kuwabeba hao watu kutoka bara hadi Zanzibar.

Hakuna jina la mwarabu hapo wa kutoka Oman bali mwafrika TippuTip.
Ungeitazama na kuisikiliza video ungepata jibu.

Hao walishikwa na wajanja wenzao wakawauza. Na usijidanganye kuwa biashara ya utumwa imekwisha imebadilika jina tu, Samatta yuko wapi? Hashim Thabiti yuko wapi. Hauna nduguzo "wabeba maboksi" huko je?

Unafikiri kama si utumwa huo ni nini? Huo ndio utumwa mamboleo kama ulikuwa huelewi.

Hapa hapa Tanzania leo hii, mchimba madini wewe, madini yako kwenye ardhi yako wewe, lakini pengine hata Tanzanite huijuwi na kama unaijuwa huna hata kipini chenye Tanzanite, kama si mtumwa tu wa kuwachimbiwa wengine ni nini?
 
Reactions: Ame
Hapa umerudi yule ninayekufaham, lakini yule aliyekuwa ana mnanga marehemu siyo FaizaFox niliyemzoea, mama anayejua kujenga hoja mwenye msimamo thabiti.

Nakusalimia tu!
 
What a pathetic old lady hivi unaweza fananisha dunia ya leo ambayo ni moral conscious na zama za utumwa.

Sammata na mwafrika yoyote hata mbeba maboksi awapo ulaya against their will na kama yupo ambae anatumikishwa bila ya ridhaa zao serikari husika ikijua mziki wake sio mdogo.

Hivi unadhani utumwa ni swala la watu kujitakia, we bibi kama hujui unyama halisi wa huyo TippuTip usichefue watu humu.

Keep your nonsense to your self.
 
🤣🤣🤣mwambie mwambie
 
Ni heri ya utumwa wa kulazimishwa kuliko utumwa wa hiyari.

Nimekupa mfano wa utumwa wako ukiwa ulaya na nimekupa mfano wa utumwa ukiwa hapahapa kwenu. Hujaelewa nilichokusudia.


Huyo huyo mzungu aliyemchukua utumwa babu yako kwa kuuzwa na babu zako waliokuwa wajanja zaidi leo unakufanya mtumwa huku unachekelea.
 
Ni afadhali mzungu anayekiri kufanya utumwa na anaomba msamaha.

Kuliko hawa wafuasi wa mbakaji na muuaji, wanatapatapa kutafuta vijisababu kufuta uovu wao.

Waarabu walihusika na biashara ya utumwa, huwezi kulifuta hili kisa hao maprofesa uchwara.
 
Huyo ni mwandishi wa Tanzania na propaganda za kidini..
Bahati mbaya hii video ina udini...kwa namna moja ama ingine kuna uteteaji mkubwa wa mwarabu kwenye biashara ya utumwa....jumba bovu lote anadondoshewa mzungu na mbantu.

Kwa kweli wacha tu shule niwe nimeenda kusomea "ujinga" ila hio mada ya huyo professor imegoma kabisa kuingia kichwani..

Najaribu kutathimini haya maisha ya mwarabu wa sasa yanasadifu kwa asilimia nyingi sana na mwarabu wa enzi za utumwa niliyo someshwa darasani.

Kwangu itabaki hivyohivyo....
 
Watu wameona kileja itakuwa kibibi.

Katazame michongo kwenye video niliyoiweka namba moja juu huko. Au wewe hupati mtandao wa kutosha mpaka shemeji arudi kazini?
Shemeji tena...
Si bure uzee umekufika vibaya.
 
Ni afadhali mzungu anayekiri kufanya utumwa na anaomba msamaha.

Kuliko hawa wafuasi wa mbakaji na muuaji, wanatapatapa kutafuta vijisababu kufuta uovu wao.

Waarabu walihusika na biashara ya utumwa, huwezi kulifuta hili kisa hao maprofesa uchwara.
Wapi alikuomba msamaha?

Hayoi mengine ulitoweka ni ujinga uliojazwa nao tu.

Yaleyale huna mapya, ni shule tu uliyosomea ujinga ndiyo iliyokuharibu. Pole sana. Mpo wengi tu, sikushangai.
 
Kwahiyo Faiza huamini kuwa waarabu walifanya biashara katili ya utumwa kwa mababu zako huku wakikuhubiria uislam au udini na ujinga ndo vimekujaa?
 
Mada umiona na kuisikiliza kwenye video niliyoiweka? Maana upo nje kabisa ya mada. Wewe unafikiri mada inanijadili mimi au Mohamed Said?


Shule za kusomea ujinga mnajulikana, hamjifichi.
 
Kwa hiyo umetumwa na waarabu kuja kuwasafisha umafia wao baada ya ile clip ya uarabuni kwenda viral?

Hao mnawashobokea sana mpaka kuiga utamaduni wao lakini they still treat you like animal na bado hamjifunzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…