Hapo kwenye Uislamu wanaume wameamrishwa kuoa zaidi ya mke mmoja, sio kweli na kama umefundishwa hivyo umedanganywa
Katika Uislamu kuna mambo yameamrishwa mfano kufuata nguzo tano za Uislamu (kushuhudia kuwa Mungu ni mmoja tu, kusali sala tano, kufunga mwezi Ramadhani, kutoa zaka, na kwenda kuhiji Makka kama mtu ana uwezo huo), pia tumeamrishwa kupenda na kuwatunza wazazi wetu wote wawili, pia tumeamrishwa kukemea mabaya yani katika Uislamu mtu hatakiwi kukaa kimya aonapo jambo lililokuwa sio sahihi kulingana na dini.
Sasa hilo suala la kuoa mke zaidi ya mmoja sio maamrisho, ni sunna (kwa maana mtume mwenyewe alilifanya) na ni muongozo toka kwenye Quran (kwa maana ni namna ya kufanya wanawake waolewe katika vipindi ambavyo wanaume wamekufa vitani ama pia kuzuia uzinzi, kuhakikisha kila mwanamke ana ndoa yake na ana mtu wa kumlinda na kumtunza)
Kwahiyo kuoa mke zaidi ya mmoja sio amri, ni jambo tu ambalo Qurani haioni ubaya wake, kama watu watalifanya kiadilifu.