Wengi tu wanaajiriwa. Ni jubudi zako tu. Kama ulijichanganya ukaajiriwa Kaliua DC shauri yako
....Uko TRA Mkuu ???....[emoji846]Wivu tu unakusumbua.
Ukiona ghorofa imesimama hadi hapo jua ana kibali tayari vinginevyo ungeshakuta Alama nyekundu.
Kaliua District Council.Kaliua DC pakoje mkuu?.
Hebu tutajie hivyo Vyuo vya uchochoroni tuvijue,Kilaza utakatiza wapi kwenye medicine, labda hivyo vyuo mlivyoanzisha huko vichochoroni
Otherwise, Life Audit kwa Wafanyakazi wa TRA na Polisi iwe ni jambo la lazima.Afisa wa TRA ana mshahara shingapi?
Mali za watoza ushuru hadharaniHuu ugomvi wa wafanya biashara na TRA naona ndio kwanza bado mpyaa........☺
Basi comments ziwe fupifupi ili kuokoa muda..😊
Swala siyo kulipwa swala una akili ya kusoma medicine?kuna madaktari kibao hawategemei hata mshahara na hiyo 3.5m ni takataka kwao.Hebu tutajie hivyo Vyuo vya uchochoroni tuvijue,
Soma Medicine ukaajiriwe halmashauri ulipwe 1.5m, Wakati wenzio wanasoma B.Com+CPA unawakuta Tra wanakula 3.5m
Ndio nyumba zetu hizi DarView attachment 2630959
UPDATE: Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule ametembelea Mtaa wa Nia Njema Mei 23, 2023, baada ya kusoma post hii ya JF
DC aliambatana na Mhandisi wa Wilaya na maafisa wengine. Baada ya kukagua ujenzi wa gorofa hilo, wamebaini kuwa linajengwa bila kibali cha manispaa na chini ya kiwango, hivyo kuhatarisha maisha ya wananchi
DC ameagiza kiongozi wa serikali ya mtaa awekwe ndani kwa kushindwa kuchukua hatua
Pia DC amempa siku 1 afisa wa TRA anayemiliki jengo hilo aripoti ofisi yake
Wakazi wa Mtaa wa Nia Njema, Mbezi Juu, wanaishukuru JF kwa kusaidia malalamiko yao yamfikie DC na hatua kuchukuliwa kusitisha ujenzi wa gorofa hilo hatarishi
Afisa wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), Boniventure Pascal Madia maarufu kama Boni amezua taharuki kubwa kwa wakazi wa Mbezi Juu kwa kujenga jengo la ghorofa 4 bila kibali cha Manispaa na bila kufuata viwango vya kitaalamu vya ujenzi na kutishia maisha ya wakazi hao kwa hofu ya jengo hilo kuanguka siku zijazo.
Wakazi wa Mbezi Juu/Goba bado wana kumbukumbu ya kuanguka kwa gorofa eneo la Goba kwa Awadhi mwaka 2021 na kuuwa watu wanne na sasa wanahofia maafa mengine kwenye Mtaa wa Nia Njema eneo la Mbezi Juu kwa Sanya.
Hofu ya wakazi wa eneo hilo ni kuwa afisa huyo wa TRA anajenga magorofa hayo chini ya viwango kwa kutumia nondo zenye milimita ndogo na mafundi wa mtaani bila kibali cha ujenzi cha manispaa.
Wakazi wa Mbezi Juu wanasema Boni alinunua nyumba ya chini iliyojengwa kwa msingi hafifu halafu akaigeuza kuwa jengo la gorofa 4 kwa kupandisha gorofa juu, huku akitumia mafundi wa mtaani, bila kibali cha ujenzi na bila kujenga msingi madhubuti unaoweza kujenga jengo la gorofa 4.
Hofu kubwa ya wakazi hao ni kuwa jengo hilo la gorofa linaloendelea kujengwa chini ya viwango huenda litadondoka siku zijazo na kuuwa watu kwenye eneo hilo.
Kila siku, wakazi hao wanapigwa na butwaa kuona afisa huyo wa TRA akiongeza gorofa kupanda juu kwenye jengo hilo, huku wakijua kuwa limejengwa kwenye msingi hafifu wa nyumba ya chini.
Viongozi wa serikali ya mtaa wa Mbezi Juu Kwa Sanya na Mtaa wa Nia Njema wameshindwa kuchukua hatua yoyote kuepusha maafa hayo na wanaachia gorofa hilo liendelee kujengwa bila kibali na chini ya viwango na kuhatarisha maisha ya wananchi.
Swala siyo kulipwa swala una akili ya kusoma medicine?kuna madaktari kibao hawategemei hata mshahara na hiyo 3.5m ni takataka kwao.
Siyo kweli mkuu, wengine wanajijengea tuWivu tu unakusumbua.
Ukiona ghorofa imesimama hadi hapo jua ana kibali tayari vinginevyo ungeshakuta Alama nyekundu.
... mwenye roho mbaya angejali usalama wa watu, ndani na nje, ya jengo hilo?
JIKITE KWENYE MADA!
Umeelewa kilicholalamikiwa?
Ghorofa nne ilipaswa kuwe na bango nje la kuonyesha details za jengo. Wao wanaohoji usalama wao wapo sahihi, goba mwaka Jana limewahi kuporomoka na majirani wakafa
Dear hapanaaa, hapa nakupingaaa watu wailoko huko kwa system wanatunyonya sisi wa chinii.
Mwanzoni nilikua nna mtazamo km wako. Ila lilipokuja kunikutaaa, nilibadili akiliii.
Wanyonge tunanyonywa had jasho, afu wao wana neemeka khaaah.
Mama Bonge alikataa kuwalipa [emoji3][emoji3][emoji3]Labda kapata mgao kwenye ile bilioni 30 waliyomdai yule mama, acha apige mjengo.
Ndo kichakaa cha kujifichia, kilimo na ufugaji, aoneshee hiyo miradi yake ya kuingiza hicho kipatooo.Punguzeni roho mbaya. Vijana wanalima majaruba ya mipunga kwao usukumani. Bado mangombe kanunua kawekeza. Ameamua ajenge pagala mnamuwaza. Watanzania wanawivu sana.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Acheni wivu kwa Boni jamani,pelekeni watoto wenu wakasomee TRA lol.