Wakuu habari za Mchana huko home Tanzania,
Naomba kwenda kwenye mada husika hapo Kama kichwa Cha habari kisemavyo, Ndugu zangu mnakumbuka kwa wale mliopitia uzi wangu wa "kijana wa kitanzania nishawishi nikupe ajira" vifaa Kama camera na laptop, niliweka ule uzi sio nikiwa namaanisha kabisa na sikuwa nadanganya, baada mda nilisoma mabandiko ya vijana waliotaka niwape vifaa hivyo.
Baada ya mda fulani nilichuja mabandiko ikatokea kijana mmoja akaja kwa kilio kweli mpaka nikamwonea huruma kulingana na alivyonipa story za maisha Kama mnavyojua nami pia hapa nilipo ni kwa sababu ya msaada kutoka kwa watu na Kama mnakumbuka Kuna uzi wangu humu story ya kutoka Singida to dar kwa kutafuta kupata msaada wa elimu.
Basi kijana alitiririka vizuri nikapendwa na kufurahia nikaona isiwe tabu ngoja tuone tinawezaje kuionuana, nilifunga baadhi ya vifaa na kutaka kupima Imani yake vizuri kwanza nilichukua camera mbili laptop 1 heavy na baadhi ya taa na vitu vingine nikavifungasha kutokea Canberra ofsi ya DHL gharama zote juu yangu yeye ni kwenda kupokea tu.
Kweli vifaa vilifika salama kabisa akaenda kuvichukua na akakabidhiwa Ila kwa mtego wa Hali ya juu amekaa na vifaa hivyo week mbili sasa bila kuanza kazi na akaanza kuvitafutia soko la kuviuza, kwa bahati nzuri katika mitego yangu yote kajitokeza jamaa ambae ni moja ya watu niliokuwa nimewatega kajifanya kuvinunua nae kwa ujinga akaruhusu kumpa jamaa kwa kuahidiwa kuwa jioni ya Leo apitie pesa yote.
Baada ya kupewa ahadi hiyo jamaa akaenda kukata tiketi ya kesho kwenda Geita coz kwa Imani yake fedha ya kuanzia maisha anayo lakini mda wa kurudi Kama saa 5 na madakika akitokea kukata ticket now kawekwa mikono salama, atalipa fedha zote za usumbufu wa usafirishaji wa vifaa na Mambo mengine.
Huyu kijana ni member humu na baada ya taratibu zingine kukamilika nitapandisha uzi kwa kila hatua na mazungumzo yote jinsi ilivyokuwa Hadi kufikia Leo dogo yupo lockup.
My take: vijana mjitahidi kusoma alama za nyakati si kila mtu ni mzembe kiivyo na mpumbavu kiasi kwamba una uwezo wa kufanya chochote wengine sisi katika maisha yetu ya mateso tumejifunza mengi na kufuzu vingi kuliko elimu ya darasani, Mungu awasaidie mtoke kwenye ujinga na kwenda nuruni tupo tayari kuwasaidia lakini hatupo tayari kwa watu wazembe kiasi hiki, Mungu anawapenda mno.
"Kijana geuka"